Tuhuma dhidi ya Membe: Bashiru hajakurupuka, kuna ukweli

Tuhuma dhidi ya Membe: Bashiru hajakurupuka, kuna ukweli

Mie nitakuwa mtu wa mwisho kumtetea Jiwe lakini ukweli shurti usemwe hata kama kusema ukweli huko kutamnufaisha Jiwe.

Background kidogo: unajua nani alimtambulisha Kipilimba kwa Jiwe? Membe. Why this matters? Hiyo ni mada ya siku nyingine ila conduit ya kinachoendelea kwa Jiwe kumfikia Membe ni Kipilimba.

Na hizo tuhuma alizotoa Bashiru jana sio za kutunga. Na hazikutokana na tuhuma za awali kutoka kwa Musiba. Katika hili, Musiba (anayenichafua kila anapojiskia) aliandika tu kile ambacho akina sie tunaojua yanayoendelea chini ya kapeti tunakifahamu kitambo.

Tatizo la Membe ni lile lile lilomfelisha kwenye mapambano wake dhidi ya Lowassa kuwania urais kwa tiketi ya CCM. Ni hivi, Membe alikuwa Mtanzania PEKEE aliyeonekana kuwa mbadala wa dhati wa Lowassa. He had support ya familia ya JK na Mwinyi na Mkapa hawakuwa na tatizo nae.

But he messed up big time. Kwa sie alumni wa kitengo, he did let us down. Not that kufanikiwa kwake kungekuwa na manufaa kwetu bali alishindwa kabisa kutumia intelijensia kuendesha mkakati wa urais, huku akiwa na advantage hiyo kubwa ya "real alternative" ya Lowassa.

Na sasa, pilika zake anazofanya huko nje kama mmoja wa challengers wa Jiwe 2020 ndio hizo zinamwagika hadharani.

Ni hivi, Bashiru ana solid evidence ya harakati za Membe ndani na nje ya Tanzania. Ni evidence hiyo - not tuhuma za Musiba - iliyompa ujasiri wa kumvaa Membe hadharani.

How did Jiwe know kuhusu pilika za Membe? One thing for sure sio umahiri wa Kitengo (there is none) bali mapungufu ya Membe. Huwezi kuwa na mkakati wa siri wa kumng'oa Kiongozi aliyepo madarakani lakini ukazembea kwenye usiri, licha ya kuwa shushushu mzoefu.

Finally, kuna mbinu moja kwenye surveillance ambayo japo sio maarufu sana lakini ina ufanisi mkubwa: overt surveillance, yaani kumfuatilia subject bila kufanya jitihada za kujificha asijue anafuatiliwa. Mara nyingi mbinu hii hutumika kwa minajili ya kumvuruga subject, ajue kuwa "upo kwenye rada zetu" na alazimike mwenyewe kunyoosha mikono.

One last thing, kuna vita kubwa inaendelea chinichini ndani ya CCM katika harakati za kumpata "mrithi wa Jiwe" 2020.

Angalizo: SITREP hii kama zilivyo sitrep nyingine haina lengo la kumshawishi mtu aamini.

Hiyo vita ipiganwe kwa uwezo wa mtu..sio mitandao ya kuneemeshana marafiki. Mtandao kama ule wa enzi uliwanufanisha wezi na wababaishaji. Wakaamua kugawana keki ya nchi kama wanagawana pipi.
Hakuna huruma wala nia ya kutafuta maendeleo ya wananchi.
Dr. Bashiru yuko sahihi...kama Membe anafaa, aache kujenga mtandao wa kulazimisha kuwa Rais. Si watu wanamtaka...I hope na Mwenyezi Mungu pia ameongea naye na kukubaliana, maana mwisho wa siku ndiyo atakayetupa kiongozi, tupende tusipende.
 
Mi nashangaa hizi sarakasi zote sijui ni za nini!

Jamani, si aliyeko madarakani anajisemea kabisa hicho cheo ni mzigo!? Mara ngapi amesikika hadharani akisema hata anajuta kukitaka hicho cheo!

Sasa watu wakijitokeza wasiokiona ni mzigo mnawapiga Vita ya nini!? Si wanahaki hiyo!? Wao si wako tayari kulala na mafaili kitandani!? Sasa kama wao wanataka wazeeke mapema nyie mnawapigaje vita!? Mbona hamna huruma kwa kiongozi wenu jamani!!

Yeyeto anayetaka aliyeko madarakani aendelee ki ukweli mimi naona hana huruma na hamtakii mema!? Unawezaje kumlazimisha mtu aliyechoka hata kabla ya kumaliza nusu ya kazi yake asaini mkataba mpya wa nyongeza!?

Tuweni serious jamani hii ni nchi sio familia moja ambayo ikianguka sababu ya uchovu wa Baba madhara yake yanaweza kufidiwa na Mama au mtu mwingine wa ukoo!
 
MB anataka kulazimisha zitumike evidence za Musiba sababu anajua mapungufu yake, Evarist Chahali hapa anamaanisha kwamba uwezekano wa KM kuwa na very strong evidences ni mkubwa sana.

So BM ajiandae
Yap! Hata yeye shushushu mbobezi anajua hilo labda kuliko mimi na wewe. Anapaswa kujua alicho nacho Musiba na kujiandaa ku-counter. Nafikiri yuko tayari kwa kikao!
 
Nasikia MB anamkwamisha rais Mara pia nasikia anataka kupindua matokeo.. Anyway wacha niendele kusikia
 
Binafsi huwa nakuamini sana Chahali
Pia,Membe anapaswa kuwa makini vinginevyo anaweza asivuke mwaka 2019 na hiyo ni kwa muktadha wa hii thread yako!
Ndugu yangu wee kwanini unapenda kujidanganya hivi? Asivuke kwa nini? (nimesoma mawazo yako ndiyo maana nimeuliza hivi). Kuna tishio kuliko lile la Lowassa 2015? Kama alitulizwa kama tui la nazi ni nini kitakachofanya hata wamwogope Membe kiasi cha kutaka kumwondoa?
 
Ndugu yangu wee kwanini unapenda kujidanganya hivi? Asivuke kwa nini? (nimesoma mawazo yako ndiyo maana nimeuliza hivi). Kuna tishio kuliko lile la Lowassa 2015? Kama alitulizwa kama tui la nazi ni nini kitakachofanya hata wamwogope Membe kiasi cha kutaka kumwondoa?

Waliomtuliza Lowasa ni magentleman hawa wa sasa ni very rough
 
Hii Stori ya Chahali ni ya uongo Ila sasa nimeamini kweli jiwe muoga sana.Hii ya awamu moja mimi nawachia mwenyewe Maccm wapigane ila Jiwe likitaka kuongeza sijuhi awamu ya tatu? Watu wengi tutaingia kwenye hiyo vita
 
Back
Top Bottom