Tufanye nini vijana waone kilimo can be a proffession too?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,232
2,000
Hello JF,

Nimeona trends huku mitandaoni kuhusu kilimo.

Nyingi zinaonyesha, vijana 's preference of white collar jobs.

Vijana wengi wana negative attitude towards Kilimo.

This is sad, because; Vijana ndio wenye nguvu za kilimo sio wazee.

I just think, compared to wazee, vijana have got soo much potential. Yet hili group ndio ndio lenye kuwa unconcerned.

Leo let us discuss, what can be done to improve young people's attitudes towards Kilimo, for them to see Kilimo can act as proffession too.

Hii iitasaidia serikali kuformulate better Agriculture Incentives when targeting this group.

Thanks.

Becky
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,146
2,000
Rebeca 83 jambo kubwa na la msingi kwanza ni utayari, pili changamoto za mitaji kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja maana taasisi zetu za fedha masharti yake si rafiki especial kwa vijana ambao ni beginner.

Sekta ya kilimo tukiikalia serious ni sekta inayoweza kuajiri watu wengi sana tokea wataalamu wa vipimo/udongo,wataalamu wa mbegu na pembejeo,wakulima shambani,nguvu kazi shambani,wauzaji wa mashine za shamba,mafundi kwa maana ya kutengeneza miundombinu ya uhifadhi mazao,secta ya usafirishaji,wafanyabiashara, watu wa masoko till tumfikie final consumer.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,412
2,000
Lawama zoote comes down to capital and market for farm produce.

Hayo mengine ni zao tu la changamoto hizo kuu mbili yaani MTAJI na MASOKO ya bidhaa za KILIMO.
 
Kashaija72

JF-Expert Member
May 18, 2020
389
1,000
Saa nane usiku hii!

Anywy, mchango wangu ni huu:

Cha kufanya ni kuhubiri ukweli kwa vitendo na matokeo. Kuna watu wengi wanahubiri kilimo wakati wao hawana shamba. Nna rafiki yangu ambaye Ni mwajiriwa kwenye halmashauri kama Afsa Uvuvi, lakini hata bwawa moja la samaki hana. Hii si sawa (kwa muono na Imani yangu). Naamini ni vizuri tukawa mfano halisi, example can change the world not opinions.

Kuna suala la vijana kupenda kazi nyepesii zisizo na shuruba nalo Ni tatizo. Vijana wamekuwa legelege, easy to go, kupenda mafanikio ya haraka kuliko uhalisia. Ukimwelekeza kilimo anaona ni kuchafuana. Ila hili litazidi kupungua kadiri Hali inavyozidi kuwa ngumu, kwani Hakuna mwalimu mzuri kama shida.

Ngonjera za wanasiasa zinapumbaza Sana watu. Mfano kwa sasa kuna kauli nyiingi za kisiasa za "serikali haijaajiri tangu 2015". Anapokuja mwanasiasa uchwara na kusema "nitatengeneza ajira kwa vijana" basi vijana wanaona huyo atawatengenezea njia ya kupata ajira rasmi za ofisini. Ndio maana unaskia....."huyu ni mkombozi.....". Vijana wanashindwa kuona kwamba hakuna mwanasiasa yeyote yule ataweza kutengeneza ajira za watu wote......

Jambo jingine linawahusu mabalizi wa nchi.

Usiku mwema!
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,204
2,000
Mada nzuri sana.

Wacha nijipe matumaini kwamba policy makers as well as decision makers wapo humu na wataona yatakayojadiliwa.

By the way katika umri wangu wa early 30s tayar mimi ni mkulima mdogo mwenye shamba la ekari 5 ninaepitia changamoto kadhaa za kilimo hususan soko. Pia mtoto wangu wa miaka miwili ni mfugaji mwenye mbuzi watano sasa.

Nasubiria kujifunza kupitia michango ya wadau
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,204
2,000
Namimi nashika nafasi ili nipate notification nione mawazo ya wadau kabla ya kuchangia hii biashara ngumu sana Tanzania.
"Hii biashara ngumu sana Tanzania"

Nina kila sababu ya kusema kwamba ugumu huu upo na ni matokeo ya serikali mbovu za CCM tangu 1961.

Rebeca 83 samahani kama mada yako nimeingiza siasa lakini nahisi hii ni miongoni mwa changamoto kuu.

Naamini wapo watakaokuja kusema changamoto kuu ambayo inabidi tuishughulikie ni kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi maana

"A problem can never be solved by the same mind that created it"
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,146
2,000
Mimi si mtaalamu wa fedha ila kama niwazavyo ni sahihi nadhani mabenki na taasisi za fedha na mikopo badala ya kukaa ofisini kusubiri wafanyabiashara wakubwa kuwafuata kuchukua mikopo mikubwa mikubwa kwenda nje ya nchi kuagiza vyakula ambavyo wanakuja kustore kwenye magodown basi wafanye yafuatayo.
 • Mosi zifanyike semina za kuwahusisha vijana kila mikoa/kanda kama itakavyoonekana inafaa kutokana na tabia nchi na aina ya kilimo kitakacholeta tija kwa kanda husika.
 • Viundwe vikundi tofauti tofauti baada ya zoezi la semina na vikundi hivi kila kimoja kichague aina ya kilimo/zao watakalokua wanadeal nalo.
 • Watafutiwe ardhi ya kutosha ambayo kwa ajili ya kuiplement aina ya zao watakalokua wamechagua kila kundi.
 • Wawekewe miundombinu wa maji na barabara za kuwawezesha kufika maeneo ya uzalishaji/mashamba husika.
 • Kwakuwa tayari vikundi husika vitakuwa vimeshatambulika basi vitafanya chaguzi ambazo pamoja na mambo mengine vitasajiliwa kisheria ili viweze kukopesheka.
 • Hatua itakayofuata ni kutafutiwa wataalamu wa kilimo kwa kila kundi hapa nikilenga kwa wenye aina inayofanana ya kilimo awepo mtaalamu wa kilimo husika ili aweze kuapply utaalamu wake kwenye mambo ya soil, mabadiliko ya tabia nchi na mbegu bora.
 • Wakati vikundi hivi zikiwa kwenye shughuli za uzalishaji basi kazi ya maafisa wa taasisi hizi za fedha ni kutafuta masoko na bei ya mazao ili mkulima atakapotoka shamba akute soko la bidhaa yake ,aweze kuuza ,kurejesha mkopo na kuendelea na process nyingine za kufanya maandalizi ya mzunguko mwingine wa uzalishaji.
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,232
2,000
Rebeca 83 jambo kubwa na la msingi kwanza ni utayari, pili changamoto za mitaji kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja maana taasisi zetu za fedha masharti yake si rafiki especial kwa vijana ambao ni beginner.

Sekta ya kilimo tukiikalia serious ni sekta inayoweza kuajiri watu wengi sana tokea wataalamu wa vipimo/udongo,wataalamu wa mbegu na pembejeo, wakulima shambani,nguvu kazi shambani,wauzaji wa mashine za shamba,mafundi kwa maana ya kutengeneza miundombinu ya uhifadhi mazao,secta ya usafirishaji,wafanyabiashara, watu wa masoko till tumfikie final consumer.

Mkuu ni kweli kuna employment opportunities nyingi kwenye Kilimo, kwenye proposal yangu iliyoibiwa Na Stellian Russu ;)🤣🤣nili identify we have 44 Million hectares of Arable Land in Tanzania;but only 33% of this is put into effective use, imagine tuki exploit fully this land,si uchumi wetu watanzania utapanda?

Kuhusu Beginners, ingependeza kupewa mkopo wa Kilimo but kuwe na Mentors wanao wa coach as they progress.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
56,310
2,000
Mkuu ni kweli kuna employment opportunities nyingi kwenye Kilimo, kwenye proposal yangu iliyoibiwa Na Stellian Russu ;)nili identify we have 44 Million hectares of Arable Land in Tanzania;but only 33% of this is put into effective use,Imagine tuki exploit fully this land,si uchumi wetu watanzania utapanda?

Kuhusu Beginners, ingependeza kupewa mkopo wa Kilimo but kuwe na Mentors wanao wa coach as they progress...
We ushawahi kufanya kilimo?

Ova
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,232
2,000
Mimi si mtaalamu wa fedha ila kama niwazavyo ni sahihi nadhani mabenki na taasisi za fedha na mikopo badala ya kukaa ofisini kusubiri wafanyabiashara wakubwa kuwafuata kuchukua mikopo mikubwa mikubwa kwenda nje ya nchi kuagiza vyakula ambavyo wanakuja kustore kwenye magodown basi wafanye yafuatayo.
 • Mosi zifanyike semina za kuwahusisha vijana kila mikoa/kanda kama itakavyoonekana inafaa kutokana na tabia nchi na aina ya kilimo kitakacholeta tija kwa kanda husika.
 • Viundwe vikundi tofauti tofauti baada ya zoezi la semina na vikundi hivi kila kimoja kichague aina ya kilimo/zao watakalokua wanadeal nalo.
 • Watafutiwe ardhi ya kutosha ambayo kwa ajili ya kuiplement aina ya zao watakalokua wamechagua kila kundi.
 • Wawekewe miundombinu wa maji na barabara za kuwawezesha kufika maeneo ya uzalishaji/mashamba husika.
 • Kwakuwa tayari vikundi husika vitakuwa vimeshatambulika basi vitafanya chaguzi ambazo pamoja na mambo mengine vitasajiliwa kisheria ili viweze kukopesheka.
 • Hatua itakayofuata ni kutafutiwa wataalamu wa kilimo kwa kila kundi hapa nikilenga kwa wenye aina inayofanana ya kilimo awepo mtaalamu wa kilimo husika ili aweze kuapply utaalamu wake kwenye mambo ya soil ,mabadiliko ya tabia nchi na mbegu bora.
 • Wakati vikundi hivi zikiwa kwenye shughuli za uzalishaji basi kazi ya maafisa wa taasisi hizi za fedha ni kutafuta masoko na bei ya mazao ili mkulima atakapotoka shamba akute soko la bidhaa yake ,aweze kuuza ,kurejesha mkopo na kuendelea na process nyingine za kufanya maandalizi ya mzunguko mwingine wa uzalishaji.

Asante kwa maelezo mazuri,Ardhi tunayo kubwa tu, ni jinsi ya kuitumia ndio tatizo....i guess wale wote uliowataja ambao wanaweza kuwa employed kwenye kilimo ungeongeza na RESEARCHERS!.. hawa wata continuously identify maeneo mbali mbali yenye potential ambayo watu tunaweza kulima ambayo ita improve our living standards.
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,146
2,000
Asante kwa maelezo mazuri,Ardhi tunayo kubwa tu, ni jinsi ya kuitumia ndio tatizo....i guess wale wote uliowataja ambao wanaweza kuwa employed kwenye kilimo ungeongeza na RESEARCHERS!.. hawa wata continuously identify maeneo mbali mbali yenye potential ambayo watu tunaweza kulima ambayo ita improve our living standards.
Point yangu namba sita nimetaja wataalamu wa kilimo nikijumuisha watafiti ama researchers wako kama ulivyotaka.
 • Kusema tuwe na makundi makundi natambua kuna kanda ambazo aina fulani ya kilimo si rafiki mathalani ukanda ambao kilimo cha mpunga ni rafiki nitashangaa ukaamua kulima mahindi and vice versa,na wenye kutambua kanda hizo ni wataalamu wa kilimo.
 • Kwa mlolongo wangu ule unaweza kuona changamoto hapa ni mtaji,na ili kuwa na security ya capital taasisi za fedha zihusike moja kwa moja kama nilivyoshauri ili uhakika wa soko pia upatikane.
 • Muhimu suala la kuwa na muongozo bora kisheria ni la muhimu kuepuka mikanganyiko isiyo ya ulazima.
 
reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,743
2,000
Huu uzi nimeuona usiku huu,

Ni masaa kadhaa toka mchana wa leo Jamaa yangu Niliyesoma naye primary akazingua,
KAINGIZA MJINI FUSO ZA VIAZI MBILI kutoka lushoto,

Sijawahi kuamini katika kilimo, ila huyu mwamba kanifanya nijifikirie upya, sio kama naona hakilipi, la hasha ila nimekua niki calculate risk zake sana, hasa nikikumbuka mzee alivyochezea za uso Ifakara, Mbeya na Huko lushoto japo Alikua akikiotea basi ni hela ya kusimamisha nyumba.

Japo pia inapaswa kuelewa HUPASWI kufanya eti kisa yeye katusua, maana pia kwa madai yake hakuanza leo...

Elimu mda mwingine inatudanganya sanaaaaaaa, huyu mwamba hata hakuwazia hasara, Sema Nilipopata ukakasi ni kwamba anasema hela almost yote anataka anunue boda akazijaze Kijijini, hapa kidogo nikashtuka manake hii biashara nayo sijawahi kuiamini, lakini nikakumbuka hata hiki kilimo sikua nikikiamini, leo ndio kimempa hela ya kununua boda 6, Nikaona Sina confidence ya kumshauri, zaidi ya kimoja ambacho amekiitikia kwa moyo wote nimemwambia abakize pesa ya kuandalia shamba tena maana ndio wanaanza taena Asubiri December.

Siandiki futuhi hapa, huyu Millionaire nimelala naye hapa, Asubuhi Nampeleka Mjini akanunue vyake apandishe kwenye Tandamu Aliyokuja nayo Arudi Kijijini,

Sasa uliza kazi yake Kubwa iliyompa pesa ya kuandaa mashamba?

Kuendesha Magari ya Magogo ya kuchana mbao, sijui kama ataendelea nayo, na sitaki kujua.
Muone alivyo sasa.

Tukienda kununua hizo boda mimi naweza onekana ndio Tajiri, kumbe escort.

Ila mwisho wa siku, hatuwezi wote kufanya kitu kimoja, hasa ukizingatia ugumu wa soko letu, mara nyingi watu wanatusua ila soko linawaangusha, ila mwisho wa siku kilimo Kinalipa, ingia shambani, sio hiki cha ku type.

Huku kwingine tunatoboa ndio, ila kunahitaji akili nyingi zaidi na mtaji unapanda taratibu sana.

Naweka kambi hapa.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,905
2,000
Hakuna mipango madhubuti ya kumhakikishia mkulima soko la mazao yake. Kuna vijana wanalima nyanya msimu wa mauzo ndoo ni Tsh200.

Ajabu ni kuwa Afrika hii hii Kuna nchi zinahitaji bidhaa hii.

Ujenzi wa viwanda vya kusindika nyanya kwenye makopo kwa matumizi ya baadae na kusafirisha nje ni muhimu.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,905
2,000
Huu uzi nimeuona usiku huu,
Ni masaa kadhaa toka mchana wa leo Jamaa yangu Niliyesoma naye primary akazingua,
KAINGIZA MJINI FUSO ZA VIAZI MBILI kutoka lushoto,
Sijawahi kuamini katika kilimo, ila huyu mwamba kanifanya nijifikirie upya, sio kama naona hakilipi, la hasha ila nimekua niki calculate risk zake sana, hasa nikikumbuka mzee alivyochezea za uso Ifakara, Mbeya na Huko lushoto japo Alikua akikiotea basi ni hela ya kusimamisha nyumba.

Japo pia inapaswa kuelewa HUPASWI kufanya eti kisa yeye katusua, maana pia kwa madai yake hakuanza leo...

Elimu mda mwingine inatudanganya sanaaaaaaa, huyu mwamba hata hakuwazia hasara, Sema Nilipopata ukakasi ni kwamba anasema hela almost yote anataka anunue boda akazijaze Kijijini, hapa kidogo nikashtuka manake hii biashara nayo sijawahi kuiamini, lakini nikakumbuka hata hiki kilimo sikua nikikiamini, leo ndio kimempa hela ya kununua boda 6, Nikaona Sina confidence ya kumshauri, zaidi ya kimoja ambacho amekiitikia kwa moyo wote nimemwambia abakize pesa ya kuandalia shamba tena maana ndio wanaanza taena Asubiri December.

Siandiki futuhi hapa, huyu Millionaire nimelala naye hapa, Asubuhi Nampeleka Mjini akanunue vyake apandishe kwenye Tandamu Aliyokuja nayo Arudi Kijijini,
Sasa uliza kazi yake Kubwa.....?
Kuendesha Magari ya Magogo ya kuchana mbao.
Boda boda sita watamletea 10,000 kila mmoja, kila siku . Hii ni hela ya kuwalipa vibarua wanaotaarisha shamba. Kwakifupi huyo ameshauwaga umasikini.
 
reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,743
2,000
Boda boda sita watamletea 10,000 kila mmoja . Hii ni hela ya kuwalipa vibarua wanaotaarisha shamba. Kwakifupi huyo ameshauwaga umasikini.
Yaaaps, Katika kutafuta pesa ukijifanya unawaza mbali sanaa, mda mwingine ndio unaharibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom