Tufanye nini vijana waone kilimo can be a proffession too?

Hello JF,

Nimeona trends huku mitandaoni kuhusu kilimo.

Nyingi zinaonyesha, vijana 's preference of white collar jobs.

Vijana wengi wana negative attitude towards Kilimo.

This is sad, because; Vijana ndio wenye nguvu za kilimo sio wazee.

I just think, compared to wazee, vijana have got soo much potential. Yet hili group ndio ndio lenye kuwa unconcerned.

Leo let us discuss, what can be done to improve young people's attitudes towards Kilimo, for them to see Kilimo can act as proffession too.

Hii iitasaidia serikali kuformulate better Agriculture Incentives when targeting this group.

Thanks.

Becky
Mkuu wewe ni Wema Sepetu?
 
Dada nivilie tu lugha yangu.

Watunga Sera wetu na Watunga Sheria wetu ni Wapumbavu kuwahi kutokea duniani. Hao ndio wanaokatisha Tamaa Wakulima na Kilimo kwa Ujumla. Siasa imekuja kuwa kizingiti cha maisha ya watu nchini kwetu, hasa Wakulima na wakati wao ndio wapiga kura kwa asilimia zaidi ya 70.

Hakuna namna ya kukizungumza kilimo bila kuizungumza Siasa, nakupa mfano mdogo tu kihistoria. Karne ya 15 kipindi cha Merchantilism iliyoleta Agrarian Revolution namna wakulima wa ndani walivyotumika kuleta maendeleo ya Uingereza tunayoiona leo.

Mkulima hathaminiki na viongozi wala haaminiki na taasisi za kifedha. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe, baba yangu hana mtaji wa kutosha ila ana hekari zaidi ya 60 alizoachiwa na baba yake, tumeshakwenda kukopa CRDB, tukajibiwa kwa ardhi tupu mkopo hatuwez kupata, inabidi tupambane wenyewe mpaka tutoboe.

Sera Sera Sera Sera. Ni mbovu mnoo.
 
Kilimo.....
Kinafikilika na kwenye mawazo Ni rahisi sna kufanyanyika... Katika utendaji Ni tofauti Sana kuanzia uzalishaji pembe jeo ziko juu sana.. utajibana na utatoboa shughuli inaludi kwenye soko hapa ndo pasua kichwa.miundombinu mibovu kufanya stocking pia Ni changamoto.

Suala hili liko mikononi mwa serikali kuweka nguvu kwenye kilimo Kama ajira ikiwa Ni pamoja na kupunguza gharama ili mwananchi wabkipato cha chini awezea kumudu




Thanks.........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Hii biashara ngumu sana Tanzania"

Nina kila sababu ya kusema kwamba ugumu huu upo na ni matokeo ya serikali mbovu za CCM tangu 1961.

Rebeca 83 samahani kama mada yako nimeingiza siasa lakini nahisi hii ni miongoni mwa changamoto kuu.

Naamini wapo watakaokuja kusema changamoto kuu ambayo inabidi tuishughulikie ni kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi maana

"A problem can never be solved by the same mind that created it"
Hata kama natamani Magufuli arudi tena Ikulu miaka mingine mitano, nasimamia ukweli kwamba kwenye kilimo masoko na kusaidia vijana au mtanzania yeyote wa kawaida wapate mitaji ya miradi ya kilimo imekuwa tatizo upande wa serikali ya CCM.
 
Technical know-how, capital and masoko. Agricultural products need to be processed, viwanda vyenyewe tia maji, just a few weeks ago nyanya zilikuwa zinauzwa bure, bure kabisa. Nani ajiingize huko apate hasara. We should work on that first.
 
Dada nivilie tu lugha yangu.

Watunga Sera wetu na Watunga Sheria wetu ni Wapumbavu kuwahi kutokea duniani. Hao ndio wanaokatisha Tamaa Wakulima na Kilimo kwa Ujumla. Siasa imekuja kuwa kizingiti cha maisha ya watu nchini kwetu, hasa Wakulima na wakati wao ndio wapiga kura kwa asilimia zaidi ya 70.

Hakuna namna ya kukizungumza kilimo bila kuizungumza Siasa, nakupa mfano mdogo tu kihistoria. Karne ya 15 kipindi cha Merchantilism iliyoleta Agrarian Revolution namna wakulima wa ndani walivyotumika kuleta maendeleo ya Uingereza tunayoiona leo.

Mkulima hathaminiki na viongozi wala haaminiki na taasisi za kifedha. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe, baba yangu hana mtaji wa kutosha ila ana hekari zaidi ya 60 alizoachiwa na baba yake, tumeshakwenda kukopa CRDB, tukajibiwa kwa ardhi tupu mkopo hatuwez kupata, inabidi tupambane wenyewe mpaka tutoboe.

Sera Sera Sera Sera. Ni mbovu mnoo.
Haswaaaaa
 
Hata kama natamani Magufuli arudi tena Ikulu miaka mingine mitano, nasimamia ukweli kwamba kwenye kilimo masoko na kusaidia vijana au mtanzania yeyote wa kawaida wapate mitaji ya miradi ya kilimo imekuwa tatizo.
Juu ya changamoto zote zilizopo nchini mimi binafsi ntaendelea kutamani magufuli abakie kuwa rais kwa sasa. At least for the next 5 years
 
Hello JF,

Nimeona trends huku mitandaoni kuhusu kilimo.

Nyingi zinaonyesha, vijana 's preference of white collar jobs.

Vijana wengi wana negative attitude towards Kilimo.

This is sad, because; Vijana ndio wenye nguvu za kilimo sio wazee.

I just think, compared to wazee, vijana have got soo much potential. Yet hili group ndio ndio lenye kuwa unconcerned.

Leo let us discuss, what can be done to improve young people's attitudes towards Kilimo, for them to see Kilimo can act as proffession too.

Hii iitasaidia serikali kuformulate better Agriculture Incentives when targeting this group.

Thanks.

Becky
Tatizo ni serikali.

Hivi kilimo kwanza iliishia wapi?

Je bajeti ya kilimo ilitengwa kiasi gani?

Je kwanini licha ya uhaba wa wataalam wa kilimo tulio nao yet wachache waliopo hawaajiriwi ili kuwasaidia wakulima huko vijijini?
 
Saa nane usiku hii!

Anywy, mchango wangu ni huu:

Cha kufanya ni kuhubiri ukweli kwa vitendo na matokeo. Kuna watu wengi wanahubiri kilimo wakati wao hawana shamba. Nna rafiki yangu ambaye Ni mwajiriwa kwenye halmashauri kama Afsa Uvuvi, lakini hata bwawa moja la samaki hana. Hii si sawa (kwa muono na Imani yangu). Naamini ni vizuri tukawa mfano halisi, example can change the world not opinions.

Kuna suala la vijana kupenda kazi nyepesii zisizo na shuruba nalo Ni tatizo. Vijana wamekuwa legelege, easy to go, kupenda mafanikio ya haraka kuliko uhalisia. Ukimwelekeza kilimo anaona ni kuchafuana. Ila hili litazidi kupungua kadiri Hali inavyozidi kuwa ngumu, kwani Hakuna mwalimu mzuri kama shida.

Ngonjera za wanasiasa zinapumbaza Sana watu. Mfano kwa sasa kuna kauli nyiingi za kisiasa za "serikali haijaajiri tangu 2015". Anapokuja mwanasiasa uchwara na kusema "nitatengeneza ajira kwa vijana" basi vijana wanaona huyo atawatengenezea njia ya kupata ajira rasmi za ofisini. Ndio maana unaskia....."huyu ni mkombozi.....". Vijana wanashindwa kuona kwamba hakuna mwanasiasa yeyote yule ataweza kutengeneza ajira za watu wote......

Jambo jingine linawahusu mabalizi wa nchi.

Usiku mwema!
Sasa bila kutoa ajira utaajiri vipi wataalam wa kilimo?
 
Tuanze kurekebisha mitaala, tufufue shule zetu za Kilimo, kuna shule zilikua specific kwa kilimo, Ufundi, etc. Tukianzia huku chini kabisa kuwajenga basi itakua rahisi wao wenyewe kuja kujiendeleza baadae.

Pili, Bank ya Kilimo ilegezee masharti sana ili vijana wengi waweze kukopesheka, kusiwe na siasa kwenye hii bank. Leo hii wanufaika wa bank hii ni the big fish na sample ndogo ya chambo ya kudanganyia...

Tatu, serikali iondoe siasa kwenye mambo haya, kuna taarifa za watu kupewa misaada based on their political affiliation. Hii ni mbaya sana
 
Mimi si mtaalamu wa fedha ila kama niwazavyo ni sahihi nadhani mabenki na taasisi za fedha na mikopo badala ya kukaa ofisini kusubiri wafanyabiashara wakubwa kuwafuata kuchukua mikopo mikubwa mikubwa kwenda nje ya nchi kuagiza vyakula ambavyo wanakuja kustore kwenye magodown basi wafanye yafuatayo.
  • Mosi zifanyike semina za kuwahusisha vijana kila mikoa/kanda kama itakavyoonekana inafaa kutokana na tabia nchi na aina ya kilimo kitakacholeta tija kwa kanda husika.
  • Viundwe vikundi tofauti tofauti baada ya zoezi la semina na vikundi hivi kila kimoja kichague aina ya kilimo/zao watakalokua wanadeal nalo.
  • Watafutiwe ardhi ya kutosha ambayo kwa ajili ya kuiplement aina ya zao watakalokua wamechagua kila kundi.
  • Wawekewe miundombinu wa maji na barabara za kuwawezesha kufika maeneo ya uzalishaji/mashamba husika.
  • Kwakuwa tayari vikundi husika vitakuwa vimeshatambulika basi vitafanya chaguzi ambazo pamoja na mambo mengine vitasajiliwa kisheria ili viweze kukopesheka.
  • Hatua itakayofuata ni kutafutiwa wataalamu wa kilimo kwa kila kundi hapa nikilenga kwa wenye aina inayofanana ya kilimo awepo mtaalamu wa kilimo husika ili aweze kuapply utaalamu wake kwenye mambo ya soil, mabadiliko ya tabia nchi na mbegu bora.
  • Wakati vikundi hivi zikiwa kwenye shughuli za uzalishaji basi kazi ya maafisa wa taasisi hizi za fedha ni kutafuta masoko na bei ya mazao ili mkulima atakapotoka shamba akute soko la bidhaa yake ,aweze kuuza ,kurejesha mkopo na kuendelea na process nyingine za kufanya maandalizi ya mzunguko mwingine wa uzalishaji.
Idara za fedha hazichukulii kilimo kama zao la kuwezesha wakulima na wao pia kupata faida! Ugumu wa mtaji huanzia hapa

Changamoto kubwa ni wataalam na masoko! Kuwa na mazao mapya na kupunguza utegemezi katika mazao ya kitamaduni kama mahindi, mpunga, ngano na nk.

Kifupi nchi yetu hatuna utamaduni wa kuinua kilimo kwa wataalam wetu kwenda kujifunza na kuibuka na mazao mapya yenye faida kubwa! Ili kuvuta vijana kwenye kilimo, hivi utalimaje wakati unamuona baba yako miaka yote analima mahindi na faida haipo clear!?

Inapotokea ukaibua zao wewe binafsi baada ya kuliona nchi za watu au mitandaoni tarajia utakufa naolo bila soko, ni ngumu sana kupata soko na mabwana soko wetu waliopo wizara ya kilimo kazi yao kusoma magazeti tu!
 
....inapotokea fursa za kujiajiri Vijana wengi huwa tunatafuta wapi risks zilipo jificha tukisha ziona tunatafuta ways za kuzikwepa...mwisho wa siku ndo tunaingiwa na hofu/uoga wa kufeli au kushindwa na kuacha fursa iende.

Vijana wengi ambao tumepitia elimu either vyuoni au elimu ya chini,tumejengewa hofu ya kudhubutu na kuaminishwa serikali ndo kimbilio letu (kuajiriwa)....yaani elimu imetufanya kuona kushindwa au kupoteza ni makosa makubwa sana ktk kutafuta mafanikio.
WHEREVER THERE IS AN OPPORTUNITIES THERE IS A RISKS.

Mzazi yupo tayari atupe pesa nyingi mashuleni/vyuoni ili mwanake apate elimu Bora Ila hayupo tayari kumpa mwanae pesa kidogo aanzishe biashara kwa kuhofia atashindwa au atapoteza pesa zake bure....anaridhika kabsa kumuona mwanae yupo tu nymban Hana kazi na anasahau kabsa Kama amepoteza pesa nyngi ili mwanae apata elimu bora,elimu ambayo angeweza kuitumia endapo angempa huo mtaji...
WAZAZI PEKEE NDIO SOLUTION KWA VIJANA KUTOBOA HAYA MAISHA,NA SIO SERIKALI SABABU SERIKALI YENYEWE NI TATIZO AMBALO KILA KUKICHA WAHESHIMIWA WANAHANGAIKA NAYO.

KAMA BABA/MAMA MAISHA YAKE YOTE AMEISHI KUITUMIKIA SERIKALI NI VIGUMU KUAMINI KWAMBA MWANAE ANAWEZA KUTOBOA LIFE KWA KUJIAJIRI,HILI NMELISHUHUDIA KWA WAZAZI WENGI....MZAZI YUPO TAYARI AKAHONGE SERIKALINI MWANAE APATE KAZI KULIKO KUMPA PESA AKAFANYE BIASHARA .

NATAMANI NIATUNGE KITABU NA NIKITOE BURE KUWAKUMBUSHA WAZAZI NA VIJANA KWAMBA WAKATI UMEBADILIKA MIAKA HII SIO MIAKA HII,MIAKA ILE AJIRA ZLIKUWA NYINGI KULIKO KULIKO WAAJIRIWA ILA MIAKA HII WAAJIRIWA NI WENGI KULIKO AJIRA SO NINI TUTARAJIE,APO NDO KIPINDI MAHUSUSI KWA VIJANA KUUNDA AJIRA NA KUJIAJIRI.

NAOMBA NIISHIE HAPA NINA MENGI YA KUZUNGUMZA.
 
Vijana hawaogopi kilimo ila kama serikali ingetambua mapendeleo ya vijana na kuyaweka vijijini. Mfano kumbi za starehe, muziki, disco, viwanja vya michezo nk unadhani kijana gani angeenda mjini
Vijana wengi tunapenda kuwa na sehemu ya kwenda baada ya kumaliza shughuli.
Mfano nchi ya Denmark ambayo ni miingoni mwa mataifa yanayoongoza kwa ufugaji wa ng'ombe walitumia njia hii
 
Back
Top Bottom