Tufanye nini vijana waone kilimo can be a proffession too?

Tatizo uliloleta jukwani linachangiwa na changamoto kuu mbili ambazo ni (i) Mitaji na (ii) Soko la mazao ya kilimo.

Tutafanikiwa kutatua au kupunguza changamoto ya kwanza (i) Mitaji kwa kushughulikia na kulimaliza tatizo la pili (ii) Masoko kama ifuatavyo:

Mashariti ya mikopo ya miradi ya kilimo kama ya TADB siyo rafiki kwa wajasiriamali vijana ambao wana ndoto lakini hawana mitaji, changamoto hii inaenda mbali zaidi kwani vijana wenzao hawazielewi ndoto zao ili kuweza kuungana nao kama kikundi waweze kukopesheka kwa mashariti ya vikundi.

Changamoto ya masoko ya ndani
Mpaka sasa sijawahi kuelewa ule utaratibu wa madalali wa mazao wanao nyonya wakulima masokoni Tanzania kote. Kwanini mkulima asifike sokoni na mzigo wake kisha kuoneshwa eneo na kushusha mzigo wake bila kulazimishwa akabidhi mzigo wake kwa dalali?
Suala la ulinzi, ushushaji mzigo n.k. liratibiwe na uongozi wa soko.
Hawa viongozi wa soko wapo sokoni kufanya kazi gani?
Madalali wanatengeneza curtail masokoni na kulalia wakulima na walaji. Hawa madalali wanafanya bishara flani kama muundo wa mafia mobs wa kudhibiti eneo la soko.

Ufumbuzi tatizo la madalali wa sokoni
  • Madalali wa biashara za mazao wawe na ofisi zao wasajiriwe rasmi kama kampuni na wao wahusike kutafuta bidhaa inayotakiwa kwa jumla na wateja wakubwa wa ndani au wa nje.
  • Wahusike kupokea wakulima wanaotafuta mteja wa bidhaa kwa muundo wa mikataba ya masoko ya muda mrefu, Nasisitiza lazima wafanye kazi kwa muundo wa mikataba tu.
  • Kusiruhusiwe ule uhuni kama wa sokoni ambao mkulima anaokotewa viazi vibovu baada ya siku tatu anapokuja kuchukua pesa yake anaaambiwa hivi vimeoza hatujauza.
  • Mkulima akisaini mkataba apewe mashariti ya ubora, akikidhi mashariti anapokabidhi mzigo wake basi hasara inayofuata baada ya hapo haimhusu mkulima.

Ufumbuzi zaidi kuhusu elimu ya Masoko ya Nje na ndani kwa pamoja
Elimu ya kutafuta masoko ya nje na ndani ya bidhaa za kilimo hayaja wekewa mkazo huko mashuleni na vyuoni, na kwenye media zetu chini ya ufadhili wa wizara ya kilimo au viwanda na biashara. Kwa sasa wahitimu wa vyuo vikuu vya kilimo waliounda kampuni au vikundi wamewekeza kwenye kutuoa elimu kwa wakulima jinsi ya kulima kwa lengo la wao kuja kuwauzia wakulima pembejeo, mbegu, na huduma za consultation tu. Hawa wadau muhimu hawasaidii kutafutia wakulima masoko ya uhakika kwa muundo wa mikataba.

Kinachotokea wakimuuzia huduma hizo mkulima anaweza kupata mavuno bora lakini msimu unaofuata hawezi kuendelea na kilimo sababu amekosa masoko na kupata hasara. Hapo utaona hata hawa wahitimu wanampoteza mteja na biashara yao inayumba, hakuna muendelezo wa miradi(no sustainability).

Serikali kupitia wizara husika haisaiidii kuwajulisha wakulima wengi uwepo wa fursa ya soko la zao flani nje ya nchi na kuwaunganisha wakulima na wateja wa huko nje.
Ukisikia tangazo ukienda wizarani haupati msaada unazungushwa tu badala ya kuunganishwa na mteja na kusaidiwa kutafsiri mashariti ya mteja, akienda mwanasiasa mkubwa kama mbunge au waziri ndiyo anasaidiwa lakini hawa wengi hawana wito wa hiyo biashara, biashara zao nyingi zinakufa kwa kukosa ufuatiliaji. Huyu mwanasiasa kwake kilimo siyo shughuli kuu ya kumuingizia kipato bali ni shughuli(kazi) ya ziada hivyo hawekezi muda wake mwingi kwenye shughuli hiyo unakuta anahujumiwa na wafanyakazi wake kisha anafilisika huku akiwa amezuia fursa kwa vijana ambao wangetumia vizuri fursa hiyo ya soko na mtaji na kufanya kilimo kama ajira yao pekee.

Elimu ya usindikaji mazao ya shamba pia haijapewa nguvu kubwa kwa watu wa kawaida ndiyo maana nyanya zina ozea sokoni au shambani. Kwa waliopata hiyo elimu hawajapewa mitaji kwa mfumo wa ruzuku au mikopo, kisha wafuatiliwe na wasimamizi maalum kuangalia wapi wanakwama.

Uingizaji toka nje au ujengaji wa viwanda vya malighafi kama kemikali zinazotumika kwenye usindikaji bado ni changamoto, wakati wenzetu kama Kenya naona kuna Taasisi inatoa mafunzo kwa nguvu na upatikanaji wa kemikali za usindikaji ni rahisi sana. Jamaa wanasambaza vitini hadi mitandaoni. Serikali itafute wafadhili kwenye sekta ya vifaa na kemikali za usindikaji.

SIDO, TIRDO na taasisi zingine zina jitahidi kutoa mafunzo lakini hakuna muendelezo au ufuatiliaji kwa wale waliopata mafunzo ikiwezakana wawezeshwe mitaji n.k. Angalia hapa jinsi taasisi kama hiyo ya Kenya inavyofanya ufuatiliaji au mrejesho (client feedback) toka kwa wateja wao Can you spare a few moments to take my survey? .

Mrejesho unahakikisha suala la sustainability ya miradi.

Tukifanikiwa kwenye ubora na uwingi wa bidhaa zinazo sindikwa ndani tutaondoa ulazima wa kuweka mashariti mengi yasiyo rafiki ya vibali vya kupeleka bidhaa za mazao ya kilimo nje ya nchi kama ilivyo sasa. Hata tukiweka mashariti ya kusafirisha bidhaa zilizosindikwa pekee bado haitaleta hathari kwa mkulima sababu tayari tutakuwa tuna wasindikaji wengi wa ndani.

KAMA yakitekelezwa mengi ya niliyo shauri hapo juu na kuboreshwa zaidi naamini changamoto ya masoko itapungua au kuisha, nina imani hapo suala la vijana kupata mitaji litakuwa rahisi kwa maana hata watu binafsi au ndugu watakopesha vijana mitaji kwa vile wanaona kilimo ni biashara ambayo inaweza kurudisha mitaji na kuleta faida.

NB: Rebecca 83 na wasomaji mtanisamehe kwa maelezo marefu lakini nilikosa maneno machache na rahisi kueleweka, labda mods au mleta uzi mnaweza kuninukuu na ku-edit mkafupisha.
 
Kilimo manina kweli, nililima nikapata mahindi kubao, mengine nilununua zikafika km gunia 100 nikasema yes hapa natoboa.
Baada ya muda Mkulu akapiga marufuku mahindi kuuzwa nje. Loooh nilipata hasara sana.
Tataizo soko la mazao haliko stable, pia kilimo ni Cha kubahatisha sana. Pia bei haileweki.
 
Rebeca 83 jambo kubwa na la msingi kwanza ni utayari, pili changamoto za mitaji kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja maana taasisi zetu za fedha masharti yake si rafiki especial kwa vijana ambao ni beginner.

Sekta ya kilimo tukiikalia serious ni sekta inayoweza kuajiri watu wengi sana tokea wataalamu wa vipimo/udongo,wataalamu wa mbegu na pembejeo,wakulima shambani,nguvu kazi shambani,wauzaji wa mashine za shamba,mafundi kwa maana ya kutengeneza miundombinu ya uhifadhi mazao,secta ya usafirishaji,wafanyabiashara, watu wa masoko till tumfikie final consumer.
Kilimo ndio kila kitu. Kilimo ndo huleta mapinduzi ya viwanda nk.
 
Kilimo ndio kila kitu. Kilimo ndo huleta mapinduzi ya viwanda nk.
Uko sahihi kabisa sijui unafanya nini kwa sasa as instrument ya kukukwamua kimaisha, ila nataka kujua mfano wewe binafsi unaona ni namna gani utengenezewe mazingira rafiki ili uingie kwenye kilimo moja kwa moja, I mean sema kabisa ikifanyika A,B na C basi hata mimi nitaweza kuingia kwenye kilimo kwa miguu yote miwili.
 
Hello JF,

Nimeona trends huku mitandaoni kuhusu kilimo.

Nyingi zinaonyesha, vijana 's preference of white collar jobs.

Vijana wengi wana negative attitude towards Kilimo.

This is sad, because; Vijana ndio wenye nguvu za kilimo sio wazee.

I just think, compared to wazee, vijana have got soo much potential. Yet hili group ndio ndio lenye kuwa unconcerned.

Leo let us discuss, what can be done to improve young people's attitudes towards Kilimo, for them to see Kilimo can act as proffession too.

Hii iitasaidia serikali kuformulate better Agriculture Incentives when targeting this group.

Thanks.

Becky
Dada mbona kizhungu kingi hueleweki au hujui kiswaili chake
 
Uko sahihi kabisa sijui unafanya nini kwa sasa as instrument ya kukukwamua kimaisha, ila nataka kujua mfano wewe binafsi unaona ni namna gani utengenezewe mazingira rafiki ili uingie kwenye kilimo moja kwa moja, I mean sema kabisa ikifanyika A,B na C basi hata mimi nitaweza kuingia kwenye kilimo kwa miguu yote miwili.
Nikipata mtaji na uhakika wa soko basi,
Naingia porini
 
Nikipata mtaji na uhakika wa soko basi,
Naingia porini
Asante lakini kilimo tunafanya kwenye ardhi, na kama ujuavyo ardhi ni mali ya serikali,hudhani bila kuwa na policy nzuri ya kilimo bado unaweza kuwa na mtaji ukaingia porini ila ukajutia muda na rasilimali zako? Hudhani hapa tuna tatizo kubwa kuliko mtaji?
 
Vijana hawaogopi kilimo ila kama serikali ingetambua mapendeleo ya vijana na kuyaweka vijijini. Mfano kumbi za starehe, muziki, disco, viwanja vya michezo nk unadhani kijana gani angeenda mjini
Vijana wengi tunapenda kuwa na sehemu ya kwenda baada ya kumaliza shughuli.
Mfano nchi ya Denmark ambayo ni miingoni mwa mataifa yanayoongoza kwa ufugaji wa ng'ombe walitumia njia hii
yaaap kazi na baaaata!!!!
 
Rebeca 83 Kikubwa ni kubadilisha sera za kupewe kipaumbele kwa Kilimo, Sababu wataalam wapo wa kutosha na Kila siku wanaongelea kilimo biashara lakini ni siasa tu.

Kilimo kina value chain kubwa hivyo kutufanya vijana tukipende serikali lazima iweke sera rafiki kwenye kilimo kufeva vijana kupewa ardhi ya kilimo, vifaa vya kisasa, masoko imara, viwanda vya kisasa kwa ajili ya zana za kilimo na uchakataji, n.k.

Siyo kila siku tunaadaiwa tuna viwanda kibao hapa nchini afu juzi jamaa akichukua fomu unasikia "eeh ili tuwe na viwanda inabidi tuwe na umeme wa kutosha ilihali kila siku ni kusifia viwanda vipo", Sasa hizi asymmetrical infos. inaonyesha kwa kiasi fulani hakuna usiriaz.
 
Asante lakini kilimo tunafanya kwenye ardhi, na kama ujuavyo ardhi ni mali ya serikali,hudhani bila kuwa na policy nzuri ya kilimo bado unaweza kuwa na mtaji ukaingia porini ila ukajutia muda na rasilimali zako? Hudhani hapa tuna tatizo kubwa kuliko mtaji?
Hiyo policy unayosema wewe wala haitubani, mashamba yapo, ukienda Vijijini huko unaenda ofisi ya kijiji basi mashamba ya kukodisha utaonyweshwa, mashamba ya uwekezaji pia utaonyeshwa
 
Rebeca 83 Kikubwa ni kubadilisha sera za kupewe kipaumbele kwa Kilimo, Sababu wataalam wapo wa kutosha na Kila siku wanaongelea kilimo biashara lakini ni siasa tu.

Kilimo kina value chain kubwa hivyo kutufanya vijana tukipende serikali lazima iweke sera rafiki kwenye kilimo kufeva vijana kupewa ardhi ya kilimo, vifaa vya kisasa, masoko imara, viwanda vya kisasa kwa ajili ya zana za kilimo na uchakataji, n.k.

Siyo kila siku tunaadaiwa tuna viwanda kibao hapa nchini afu juzi jamaa akichukua fomu unasikia "eeh ili tuwe na viwanda inabidi tuwe na umeme wa kutosha ilihali kila siku ni kusifia viwanda vipo", Sasa hizi asymmetrical infos. inaonyesha kwa kiasi fulani hakuna usiriaz.
Shida ni kuwa Viongozi wetu wa kiafrica ni wanafiki wapo pale kwa ajili ya matumbo yao na familia zao na ukoo wao, ndo mana hata Huko ulaya wazungu hawapendi watu weusi kwasabu ya tabia zetu na ndio maana hili bara bado no. Maskini kwasabu ya Viongozi tulio nao
 
Hiyo policy unayosema wewe wala haitubani, mashamba yapo, ukienda Vijijini huko unaenda ofisi ya kijiji basi mashamba ya kukodisha utaonyweshwa, mashamba ya uwekezaji pia utaonyeshwa
Unazungumziaje mtu aliyeamua ku sacrifice kila kitu kisha akawekeza say kwenye kilimo cha zao la biashara mfano korosho then itokee drama kama iliyotokea mtwara karibuni, utasema kweli policy haikubani kama mkulima?
Hukumbuki kuna watu fulani fulani waliachishwa kazi Kagera kisa tu kuna wakulima walikuwa wanapitisha kahawa...kahawa imagine! Kwenda kuuza Uganda kwa sababu kule soko ni rafiki, policy hapa haihusiki ndugu mjumbe? Asante
 
Asanteni kwa mawazo yenu mazuri ila tungejikita kwenye tufanye nini vijana wavutiwe na kilimo?
Kuna haha ya kuwa na Somo la kilimo kuanzia elimu ya msingi.
Watoto wafundishwe basics Kama ufuhaji kuku ,Kilimo Cha mboga mboga kwa scale ndogo hata ngazi ya familia Tuu.
Set nzuri za Kilimo...Kilimo kipewe kipaumbele Maana NI uti wa mgongo was taifa hili..
 
Unazungumziaje mtu aliyeamua ku sacrifice kila kitu kisha akawekeza say kwenye kilimo cha zao la biashara mfano korosho then itokee drama kama iliyotokea mtwara karibuni, utasema kweli policy haikubani kama mkulima?
Hukumbuki kuna watu fulani fulani waliachishwa kazi Kagera kisa tu kuna wakulima walikuwa wanapitisha kahawa...kahawa imagine! Kwenda kuuza Uganda kwa sababu kule soko ni rafiki, policy hapa haihusiki ndugu mjumbe? Asante
Sawa mjumbe subir kidogo nimalizie hii Kvant nakuja
 
Shida ni kuwa Viongozi wetu wa kiafrica ni wanafiki wapo pale kwa ajili ya matumbo yao na familia zao na ukoo wao, ndo mana hata Huko ulaya wazungu hawapendi watu weusi kwasabu ya tabia zetu na ndio maana hili bara bado no. Maskini kwasabu ya Viongozi tulio nao
Kwakweli ni unafiki wa hali ya juu, kikubwa ni kuweza kutenganisha siasa na mambo mengine ya kitaaluma, Shangaa Profesa mwenyewe anafundishwa kazi na mwanasiasa na ametulia tuli{hahahahaha}, kuna mambo mengine yanasikitisha Tanzania hii.
 
Shida ni kuwa Viongozi wetu wa kiafrica ni wanafiki wapo pale kwa ajili ya matumbo yao na familia zao na ukoo wao, ndo mana hata Huko ulaya wazungu hawapendi watu weusi kwasabu ya tabia zetu na ndio maana hili bara bado no. Maskini kwasabu ya Viongozi tulio nao
Kanuni inalinda dakika zako ukirudi unaendelea ulipoishia!
Ukisoma hapo juu vizuri utapata jibu la swali lako mjumbe
 
Hii inaweza kuwa useful na refference nzuri

9 ways to engage youth in agriculture


In Africa over 200 million people are aged between 15 and 24, the youngest population in the world. This age group according to the African Economic Outlooks is expected to double in number by 2045. Low profitability, poor security of land tenure, and high risks are just some of the reasons Africa’s youth are leaving rural areas to seek jobs in cities, a migration that could see Africa with a shortage of farmers in the future. Given that agriculture is one of the continent’s biggest economic sectors, generating broad economic development and providing much of the population with food, this poses a serious threat to the future of farming and to meeting the demands of a rapidly growing urban population. Growing youth unemployment, ageing farmers and declining crop yields under traditional farming systems mean engaging youth in agriculture should be a priority.

Recent articles highlight this key challenge and suggest solutions for making agriculture more attractive to younger generations.

1) Link social media to agriculture
The rise of social media and its attraction among young people with access to the appropriate technologies could be a route into agriculture if the two could be linked in some way. Mobile phone use in Africa is growing rapidly and people are now much more connected to sources of information and each other. Utilising these channels to promote agriculture and educate young people could go a long way in engaging new groups of people into the sector.

2) Improve agriculture’s image
Farming is rarely portrayed in the media as a young person’s game and can be seen as outdated, unprofitable and hard work. Greater awareness of the benefits of agriculture as a career needs to be built amongst young people, in particular opportunities for greater market engagement, innovation and farming as a business. The media, ICT and social media can all be used to help better agriculture’s image across a broad audience and allow for sharing of information and experiences between young people and young farmers.

3) Strengthen higher education in agriculture
Relatively few students choose to study agriculture, perhaps in part because the quality of agricultural training is mixed. Taught materials need to be linked to advances in technology, facilitate innovation and have greater relevance to a diverse and evolving agricultural sector, with a focus on agribusiness and entrepreneurship. Beyond technical skills, building capacity for management, decision-making, communication and leadership should also be central to higher education. Reforms to agricultural tertiary education should be designed for young people and as such the process requires their direct engagement.

4) Greater use of Information and Communication Technologies (ICT)
Not only can ICT be used to educate and train those unable to attend higher education institutions but it can be used as a tool to help young people spread knowledge, build networks, and find employment. Catering to a technologically savvy generation will require technological solutions. Such technologies can also reduce the costs of business transactions, increasing agriculture’s profitability.

5) Empower young people to speak up
If we are to enable youth to transform agriculture then the barriers to their engagement, such as access to land and finance, need to be addressed. National policies on farming and food security need to identify and address issues facing young people. As such youth need to become part of policy discussions at the local and national levels, whether as part of local development meetings, advisory groups or on boards or committees.

The Young Professionals’ Platform for Agricultural Research for Development (YPARD) aims to provide a platform for young people to discuss opportunities in agricultural development, share experiences and advocate for greater youth engagement and representation.

6) Facilitate access to land and credit
Land is often scarce and difficult to access for young people, and without collateral getting credit to buy land is nigh on impossible. Innovative financing for agriculture and small businesses is needed. For example soft loans provided to youth who come up with innovative proposals in agriculture or microfranchising.

7) Put agriculture on the school curricula
Primary and high school education could include modules on farming, from growing to marketing crops. This could help young people see agriculture as a potential career. Farm Africa run a project aiming to help school children discover more about agriculture as a profession.

8) Greater public investment in agriculture
Young people may see agriculture as a sector much neglected by the government, giving farming the image of being old fashioned. Investment in agriculture is more effective at reducing poverty than investment in any other sector but public expenditure on agriculture remains low. Regional and continent-wide programmes such as the Comprehensive Africa Agriculture Development Programme (CAADP) may go some way in transforming the prominence and reputation of agriculture in Africa but national efforts and public investments are also needed.

9) Make agriculture more profitable
This is an easy statement to make but a difficult one to realise. Low yields and market failures in Africa reduce the potential of agriculture to be profitable and to provide people with a chance of escaping poverty and improving their quality of life. Making agriculture profitable requires that the costs of farming and doing business are reduced while at the same time productivity increases. Although large-scale commercial farming springs to mind, this is not necessarily the case, and small farms can be highly productive with low labour costs.

Of course all of these solutions come with their own hurdles: access to education and technologies, rural development, land rights etc. But as one article states “Africa has the highest number of youth in the whole world, and some of the most fertile soils – the two combined could be a force to promote agricultural development!“ Foregoing engaging youth in agriculture and the potential for transformation this could bring because of the complexities of modernising agriculture would be a huge opportunity lost.

Note. This article was originally published at the Can we feed the world website
 
Huu uzi nimeuona usiku huu,

Ni masaa kadhaa toka mchana wa leo Jamaa yangu Niliyesoma naye primary akazingua,
KAINGIZA MJINI FUSO ZA VIAZI MBILI kutoka lushoto,

Sijawahi kuamini katika kilimo, ila huyu mwamba kanifanya nijifikirie upya, sio kama naona hakilipi, la hasha ila nimekua niki calculate risk zake sana, hasa nikikumbuka mzee alivyochezea za uso Ifakara, Mbeya na Huko lushoto japo Alikua akikiotea basi ni hela ya kusimamisha nyumba.

Japo pia inapaswa kuelewa HUPASWI kufanya eti kisa yeye katusua, maana pia kwa madai yake hakuanza leo...

Elimu mda mwingine inatudanganya sanaaaaaaa, huyu mwamba hata hakuwazia hasara, Sema Nilipopata ukakasi ni kwamba anasema hela almost yote anataka anunue boda akazijaze Kijijini, hapa kidogo nikashtuka manake hii biashara nayo sijawahi kuiamini, lakini nikakumbuka hata hiki kilimo sikua nikikiamini, leo ndio kimempa hela ya kununua boda 6, Nikaona Sina confidence ya kumshauri, zaidi ya kimoja ambacho amekiitikia kwa moyo wote nimemwambia abakize pesa ya kuandalia shamba tena maana ndio wanaanza taena Asubiri December.

Siandiki futuhi hapa, huyu Millionaire nimelala naye hapa, Asubuhi Nampeleka Mjini akanunue vyake apandishe kwenye Tandamu Aliyokuja nayo Arudi Kijijini,

Sasa uliza kazi yake Kubwa iliyompa pesa ya kuandaa mashamba?

Kuendesha Magari ya Magogo ya kuchana mbao, sijui kama ataendelea nayo, na sitaki kujua.
Muone alivyo sasa.

Tukienda kununua hizo boda mimi naweza onekana ndio Tajiri, kumbe escort.

Ila mwisho wa siku, hatuwezi wote kufanya kitu kimoja, hasa ukizingatia ugumu wa soko letu, mara nyingi watu wanatusua ila soko linawaangusha, ila mwisho wa siku kilimo Kinalipa, ingia shambani, sio hiki cha ku type.

Huku kwingine tunatoboa ndio, ila kunahitaji akili nyingi zaidi na mtaji unapanda taratibu sana.

Naweka kambi hapa.
😂😂😂😂nimecheka lakini umenikumbusha mbali saana
 
Nguvu za mwili hazina tija kwenye kilimo, kilimo kinahitaja overhaul kiwe cha kutumia teknologia dunia nzima ndio kitapendwa.

Kilimo sio mali ya vijana ni for the whole society, lakini kiwe kilimo chenye manufaa, sio kuumizana.

Vijana ni kundi kubwa linahitaji technologia kufanya kila kitu sio kilimo pekee.

Kwanini unaona vijana ndio hufaa kulima na sio wazee?! Hata nchi zilizoendelea wakulima wakubwa yani wale wanaofanya kilimo cha technologia ni wazee.

Kigeuze kilimo kwanza kama sekta, iwe na tija kisha waite vijana.

Vijana kiuchumi hawahitaji kilimo kabisa, vijana rika dogo uhitaji kuwa mashuleni wakiwa trained kwenye maeneo tofauti, wale Rika la kati wakizalisha kuhudumia familia zao na jamii, wale vijana wa Rika la juu waki watrain hawa new force kushika hatamu wao wakizeeka.

Kilimo chetu hakipendwi, hakina tija. Mfano, unaanza kuandaa shamba la pamba october unaanza kulima November hadi December unapanda, unakuja kuvuna may au June, unauza July hadi August pengine uuze kwa MKOPO yani uwape pamba wakulipe baadaye.

Unaanza kujiandaa kutafuta mbegu na pembejeo na kuanza maandalizi ya msimu ujao huna kitu.

Unakula nini, unavaa nini na ukiugua au mkeo au mtoto unamtibu vipi, hakuna bima au insurance za matibabu za wakulima au familia za wakulima.

Watoto wanahitaji kwenda shule huna kitu,bado hujalipwa na hujui utalipwa lini.

Kwa ujumla kilimo Tanzania hii ni ujinga, bora ufanye uchuuzi wa mazao. Nunua uza move on.

Acha kazi kalime kisha utuletee mrejesho hapa, nasi tujifunze kutoka kwako.

Nawashauri vijana wasilime, watafute elimu vizuri, waelimike vizuri wafanye mambo yenye tija kwenye maisha yao, sio kilimo chetu hiki cha kutegemea mvua.
God forbid.

Walime wazee, sisi tunajiandaa na safari ya kwenda Mars.
 
Back
Top Bottom