Tuambie sababu inayokufanya usipumzike.....

Tuambie sababu inayokufanya usipumzike.....

Aliyejiajiri kupumzika inakuwa changamoto, maana anachoingiza ndicho anachotumia, kwa mfano unataka mama ntilie apumzike siku tatu, wakat huo huo anawaza kuongezeka?? haiwezekani.

Wanyakazi wa walioajiriwa wanapenda kupumzika sababu kubwa ni uvivu na kwa sababu anajua mwisho wa mwezi mshahara utaingia aumwe asiumwe, tofauti na aliyejiajiri labda wale ambao wameshasi mama na kuweza kuajir watu katika biashara zao wana nafasi ya kupumzika
Very sad,. Kwahiyo hakuna kupumzika labda mda wa kulala tu 🤔
 
Mimi nina partner wa biashara lakini wote tunafanya kwa bidii zote
Asikuambie mtu, hela ni kama uchawi vile

Kila unapopata unataka ziada
Nilipopata 100m ya kwanza nikasema niongeze x2 kama nitaweza

Siwezi kuacha kazi ya kujituma ila napumzika pia maana right hand wangu ni mzuri kwa biashara zote anazimudu

Nae anapumzika pia
Ila ukisema kazi haziendi bila wewe je umewaza kufa?
Hongereni sana aisee,.
Ninaofanya nao hawawezi kujisimamia

Nakumbuka mwaka Jana niliumwa Kwa miezi mitatu mfululizo,. Kila kitu kilivurugika nipo napambana nirudi kwenye mfumo maana nimeanza upya
 
Wakuu habari za nyie...

Mara nyingi nimekuwa nikiskia watu wanaambizana,. "Ukijiajiri unakuwa na mda mwingi wa kupumzika Kwasabu Kila kitu unajiamulia mwenyewe ufanye au usifanye".. kiuhalisia naona kama hii kauli haina ukweli,. Ila tuachane nayo tu kwanza tujikite kwenye mada

Tukiachana watumishi wa serikali najuwa likizo wanazo na wanazotumiaje hilo wanajua wenyewe,. Haya wewe ambaye umejiajiri kwanini hupumziki??,. Kwanini hujipi mda wa kupumzika japo hata miezi miwili au mitatu utulie tu upumzishe mwili na akili Au hata wiki au hata siku kadhaa ,. Kwanini hufanyi hivyo?..

Ni kwamba unaipenda sana KAZI au biashara Yako??, Au ni kwamba wewe hupendi kupumzika ( kutulia ) ,Bado hujatimiza malengo? Na unaamini ukifanya KAZI mfululizo bila kupumzika ndio utafanikiwa??,. Unayo majukumu mengi kiasi cha kwamba usipofanya KAZI wiki au mwezi mmoja Kila kitu kinavuruguika??,. Huna mtu wa kukusaidia ?? Au shida Nini??.... Tuambizane tu kidogo huenda ukapata namna ya kujipumzisha kutokana na maoni ya wadau..

Kwa upande wangu ni kwamba Bado sijaweza kujisimamia mwenyewe na watu ninaoshirikiana nao usipowasimamia KAZI zinaweza zisiende au zikafanyika sio Kwa kiwango kile ambacho inabidi kifanyike, Na mambo mengi ambayo yanahitaji kutimizwa Kwa wakati maana umri hausimami eti🥹
Nahitaji sana kujipumzisha ila changamoto ndio hiyo..

Tuambie na wewe tatizo nini???
Kwa Mimi sipumziki sababu Sina mke.
 
Tofautisha kati ya kujiajiri, kuajiriwa na kumiliki biashara.

Wapo walio ajiriwa ila wana vipengele vya kuwa part time workers kwenye kazi zao,
Walio jiajiri wengi ni middle na low end class, ambao hata shughuli zao hazina mzunguko wa 1m per month.
-( hawa waki pumzika nothing goes on)

Wamiliki wa biashara labda ambae ana miaka mingi ya kufaidika kwenye game, maana kila uki amka you wish to be better than yesterday, and make it tomorrow than today.

Note by: mapumziko ni maamuzi tu, una weza usiwe na kingi ila uka enjoy kwa ulicho nacho.
 
Hongereni sana aisee,.
Ninaofanya nao hawawezi kujisimamia

Nakumbuka mwaka Jana niliumwa Kwa miezi mitatu mfululizo,. Kila kitu kilivurugika nipo napambana nirudi kwenye mfumo maana nimeanza upya
Tafuta mtu awekeze kiasi cha hela hata 30% ya mradi ili akusaidie
 
Yani ukisikiliza maneno ya wafanyabiashara na wajasiriamali wa bongo unaweza kudhani waliojiajiri wote ni matajiri na walioajiriwa wote ni masikini, kuna ukweli mwingi sana unafichwa sema ndio vile tena kila mtu anataka aonekane motivational speaker ila ukweli ni kwamba kwenye biashara, kama kweli unautaka huo utajiri basi hakuna huko kupumzika wanakokusema vinginevyo utaishia kuwa mid class au masikini kabisa, ni kama tulipokuwa shule tulikuwa tunaambiwa mkifika chuo mtakuwa na uhuru mnaoutaka hakuna wa kuwapangia maisha tofauti na shule lakini cha ajabu ukifika huko chuo, ni kweli hakuna wa kukuingilia ila hayo masomo tu yenyewe yatakuingilia na yatakupangia maisha hivyo ili ufaulu kihalali utalazimika kujiwekea ratiba kama ya mwanafunzi wa shule tu kiasi kwamba hata hiyo raha ya huo uhuru unaosemwa huioni
Yeah ni kweli,. Kuna mambo mengi sana wafanyabiashara hawayasemi na ukiingia Kwa kusikiliza maneno ya watu walahi cha moto utakiona
 
uwiano kati ya kazi na kupumzika ni jambo la msingi. Kupumzika kwa kiasi kunaweza kuwa njia ya kuongeza ufanisi, lakini kupumzika kupita kiasi kunaweza kuzuia maendeleo.

Mwisho wa siku, kila mtu ana njia yake ya kugundua kipimo sahihi cha mapumziko kulingana na malengo yake maishani. 😊
Hizo njia ambazo Kila mmoja anazo zake ndio inabidi tuelekezane mkuu,.

Nimegundua maisha hayahitaji u serious sana aisee
 
Miili na akili zetu hazijaumbwa kuwa idle..

Yani hatujaumbwa kupumzika continuously km tunavyowazaga..

Pia hatujaumbwa kufanya kazi bampa to bampa...

Ndo maana unatakiwa ufanye kazi kwa kiasi, upumzike kwa kiasi..

Chochote kikizidi kipimo kinakuwa sumu..
Hapo nimekupata
 
Tofautisha kati ya kujiajiri, kuajiriwa na kumiliki biashara.

Wapo walio ajiriwa ila wana vipengele vya kuwa part time workers kwenye kazi zao,
Walio jiajiri wengi ni middle na low end class, ambao hata shughuli zao hazina mzunguko wa 1m per month.
-( hawa waki pumzika nothing goes on)

Wamiliki wa biashara labda ambae ana miaka mingi ya kufaidika kwenye game, maana kila uki amka you wish to be better than yesterday, and make it tomorrow than today.

Note by: mapumziko ni maamuzi tu, una weza usiwe na kingi ila uka enjoy kwa ulicho nacho.
Umenena vyema..

Ila hapa kwenye kuenjoy na ulichonacho ndio kwenye kamzozo,.huwezi kuwa na laki eti useme unataka kuenjoy lazima uendelee kukaza walau upate laki2 na ukiipata laki2 utasema ngoja nipige Tena walau ifike milioni ndio nitulie ndo hapo unajikuta mwaka unaisha hujapata chance ya kurest
 
Kama hapa nikiwa Jf napumzika Ila kusema nikadhulule Serengeti ama niende FUKWE MBALI MBALI ZA BAHARI HAPANA.

KIBARUANI THEN NYUMBANI USIKU NDIO RATIBA YANGU 24/7/365
Nadhani wewe uko kama Mimi mkuu,. Humu ndio sehemu ya kupumzikia na jumapili labda😃😂😂,.

I wish nipate mda hata mwezi simu imezimwa,. Niko tu mahali nimetulia napunga upepo,.kusoma some books , meditation yaani nipate utulivu wa mwili na nafsi
 
Umenena vyema..

Ila hapa kwenye kuenjoy na ulichonacho ndio kwenye kamzozo,.huwezi kuwa na laki eti useme unataka kuenjoy lazima uendelee kukaza walau upate laki2 na ukiipata laki2 utasema ngoja nipige Tena walau ifike milioni ndio nitulie ndo hapo unajikuta mwaka unaisha hujapata chance ya kurest
Kwenye kitabu cha magic of thinking big by David Schwartz ana sema
" the mind is a place it's self, you can make a hell out of heaven, or a heaven out of hell.

Nyashinski kwenye nyimbo ya hayawani, kaimba " tuna ongezea nini bidii, na roho ya mwanadamu haitosheki haki.

Kiranga ali sema the right time to stop, is not to start.

Mimi Intelligent businessman nasema jifunze kuwa na kiwango Cha kuridhika katika kila uki fanyacho.
 
Back
Top Bottom