Tuache lawama! Kila mtu hupokea kulingana na Mchango wake katika jamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
Kumekuchwa!

Ukitoa Mia utapokea Mia.
Ukilima mahindi bila Shaka utavuna mahindi!
Maisha ni mfano wa kioo, ukicheka yanacheka ukinuna yananuna!

Taikon siku zote atasema ukweli hata Kama unauma, ukweli ni ukweli tuu.

Hili la Profesa Jay kuchangiwa limezua minong'ono kwenye jamii, hata hivyo hii sio mara ya Kwanza Kwa watu mashuhuri kuchangiwa na kuleta minong'ono, wapo wengi tuu wengine sasa hivi walitangulia mbele za haki.

Siku zote najaribu Kueleza ukweli mchungu kuwa binadamu hatufanani ingawaje tunaweza kuwa Sawa. Halikadhalika tunaweza kufanana lakini tusiwe Sawa.

Hatuwezi kujifariji Kwa kujifanganya kuwa tupo Sawa ilhali maisha tumeyakuta yanapendelea, dunia inapendelea wengine na kuwaumiza wengine. Kusema tupo Sawa ni kujiongopea na Dalili ya kurukwa na akili.

Sitaki kutaja mambo ya Imani wala dini za watu, lakini hata huko kwenye dini na Imani upendeleo upo, Mungu anayetajwa kuna viumbe wake aliowapendelea na wapo walioonewa na kukasirikiwa vibaya mno. Labda tuwe wanafiki lakini upendeleo ni Jambo halisi lisiloepukika.

Ukifanya makubwa utalipwa makubwa
Ukifanya madogo utalipwa madogo.

Ukifanya mambo makubwa mazuri utaepushwa na mabaya makubwa endapo utayafanya au yatakutokea.
Pia ukifanya madogo Kwa udogo dunia itakuadhibu Kwa madogo na kukuzidishia mabaya makubwa ili uangamie.sio ajabu mwizi wa kuku WA elfu tatu akachomwa Moto au kufungwa jela miaka mitatu na wakati huo huo jizi la mamilioni ya pesa likiepushwa na adhabu Kali na kulindwa na walimwengu.

Hayo ndio maisha, ndivyo yalivyo yapo hivyo hivyo.
Hayakuanza Jana mambo Kama hayo,

Maisha yanatulazimisha kila mmoja wetu kufanya kitu Kwa ubora ili yamlipe mambo Bora Kabisa.
Wote waliofanya vitu Kwa ubora wa juu kabisa walilipwa sifa njema na maisha. Iwe ubora wa Mema au mabaya.

Maisha hayahitaji mtu legelege, mvivu, mzembe na duni ajitiaye dhaifu. Maisha yanahitaji mtu wakuyatumikia,maisha ni Mfalme yanahitaji kutumikiwa.
Watu wote wanayoyatumikia maisha, maisha huwapa taji.
Lakini wale wenzangu na miye ambao hutegemea kudra na bahati, ati maisha yawatumikie alafu wao wapate huishia kuwa watumwa wa wanaoyaheshimu maisha.

Ni kweli maisha hayana fomula ya moja Kwa moja lakini zipo kanuni chache za muhimu ambazo lazima uzijue;
Mosi; maisha yanakufundisha ujiamini mwenyewe na usimuamini mtu, ukifanya hivyo utaishi Kwa Amani.

Lapili, maisha yanakufundisha usiweke matatajio Wal usiwe na matarajio makubwa yaani USIUAMINI MUDA Isipokuwa kila guess uipatayo ifanye Kama haitotokea tena.

Mwisho; maisha yanahitaji uyatumikie sio yakutumikie.

Kuchangiwa na kutochangiwa ni matokeo ya mtu mwenyewe jinsi alivyojitoa kwenye jamii husika.

Jinsi utoavyo ndivyo upokeavyo, hiyo ni kanuni.

Wanaosema mbona kuna masikini wapo mahospitalini huko hawachangiwi wanashindwa kuelewa kuwa Mchango wao ndani ya jamii ni mdogo mno ndio maana nao hupata kidogo Sana.

Maneno haya yanatia uchungu Sana ingawaje ndio ukweli wenyewe.

Hatuwezi kulingana katika matokeo ilhali kwenye mchakato hatukulingana.
Mchakato ukiwa Sawa basi matokeo huwa Sawa.

Maisha hayana huruma, kusema wewe au Mimi ni masikini au fukara hakubadilishi lolote katika falsafa ya maisha.
Maisha yatakucharaza hata Kama ni Yatima, mjane au fukara. Ndivyo yalivyo.

Maisha ukitaka uende nayo Sawa, usijihurumishe kwayo, yakirusha ngumu nawe rusha, maisha yanahitaji yakulaumu Kwa kipigo unachoyapa, sio uyalaumu Kwa kipigo yanachokupa.

Watu mashuhuri, viongozi, Wasanii na wakubwa wote wataendelea kuneemeka na kuchangiwa kwani ndivyo kanuni ilivyo.

Sio CCM
Sio CHADEMA
Sio ACT au Vyama vitakavyoundwa baada yetu. Mambo yataenda Vivi hivi.

Sio ajabu Tundu Lisu alichangiwa pesa
Sio ajabu Mbowe na wenzake wanachangiwa pesa
Sio ajabu mara hii ni Profesa J anachangiwa.

Sio Kama hakuna masikini wenye matatizo Kama hayo, wapo Ila Mchango wao ni mdogo kiasi kwamba hawastahili return ya namna hiyo.

Tutalaumiana, tutakwaruzana na kuonana Wabaya lakini ndivyo ilivyo na hayo ndio Maisha.

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwa Mh. Lissu walitaka kuchangia hadi damu...roho mbaya ya mwendazake akazima zoezi....ila Mungu mkubwa kamwacha Lissu anahema yeye kasepeswa dadadeq.

Watanzania wenzangu Mungu yupo tenda haki ili usife kifo cha AIBU.
 
Kwa Mh. Lissu walitaka kuchangia hadi damu...roho mbaya ya mwendazake akazima zoezi....ila Mungu mkubwa kamwacha Lissu anahema yeye kasepeswa dadadeq.

Watanzania wenzangu Mungu yupo tenda haki ili usife kifo cha AIBU.
Vipi imani yako kifo ni heri au ni adhabu?na Kama adhabu mnufaika nani?na msherekea kifo ni Nani?
 
Maisha hayana huruma, kusema wewe au Mimi ni masikini au fukara hakubadilishi lolote katika falsafa ya maisha.
Maisha yatakucharaza hata Kama ni Yatima, mjane au fukara. Ndivyo yalivyo.
Tycon wa falsafa nimekukubali sana.

Huu ndio ukweli
 
Back
Top Bottom