Mchango wa Serikali Kwenye Michezo: Kwanini Usitambulike?

Mchango wa Serikali Kwenye Michezo: Kwanini Usitambulike?

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
532
Reaction score
506
Kuna jambo ambalo kwa kweli linanifanya nijiulize kwa nini mtu anaweza kuumia kabisa kusikia hata jina la Rais likitajwa kwenye mchezo wa mpira eti kwa sababu Serikali imepongezwa ?

Hapa tunahitaji kutenganisha siasa na uhalisia wa maendeleo ya michezo.

Kumtaja Rais katika hafla au mashindano ya michezo si maana kwamba mpira umegeuzwa kuwa mkutano wa kisiasa chandimu sijui wanatumia akili gani🙌.

✍🏻Kama Serikali imehusika kuweka mazingira ya michezo kujenga au kuboresha viwanja kuimarisha miundombinu kuwezesha mashindano na kuhakikisha usalama na maandalizi yanafanyika kwa nini mchango huo usitambuliwe?

Mashirika makubwa ya soka kama FIFA na CAF yenyewe yanaposhirikiana na nchi mwenyeji wa mashindano makubwa hayawezi kufanya kazi bila Serikali.

Serikali ndiyo yenye mamlaka na wajibu katika maeneo mengi kama miundombinu usalama usafiri afya uhamiaji na maandalizi ya kitaifa.

Ndiyo maana katika mashindano makubwa duniani Serikali za nchi mwenyeji hupewa nafasi na kutambuliwa kwa mchango wao.

📌Hata Uingereza ambayo mtu anaweza kuitumia kama mfano wa Serikali kutokuwa inaendesha mpira moja kwa moja bado Serikali ina nafasi katika sera sheria usalama miundombinu na mazingira ya maendeleo ya michezo.

Kwa hiyo kusema kwa nini mumtaje Rais kwenye mpira? bila kuangalia mazingira yaliyofanya mashindano hayo yawezekane ni kupunguza jambo kubwa kuwa siasa za chuki.

✍🏻Rais si mchezaji wa timu Serikali si kocha na Waziri si mshambuliaji anayefunga goli.

Lakini Serikali inaweza kuwa imejenga uwanja ambao mechi inachezwa ikaweka miundombinu usalama na mazingira ya mashindano.

Mchezaji apewe sifa kwa kufunga goli kocha apewe sifa kwa mbinu TFF au CAF apewe sifa kwa maandalizi na Serikali nayo itambuliwe kwa sehemu yake.

Hiyo siyo propaganda ni kutambua mchango wa kila upande.

Na kinachoshangaza zaidi ni pale chandimu wanaumia kabisa hata jina la Rais likitajwa kwa pongezi kana kwamba kulitamka jina hilo ni kosa.

Huo tayari si mjadala wa michezo ni hisia za kisiasa zinazomfanya mtu ashindwe kutenganisha kile anachokipenda na kile asichokipenda.

Unaweza usikubaliane na Rais unaweza kuikosoa Serikali unaweza kuwa na mtazamo tofauti kisiasa lakini hilo halikupi sababu ya kukataa hata jambo jema lililofanywa na Serikali.

Ukiona uwanja umejengwa sema umejengwa.

Ukiona timu imecheza vizuri sema imecheza vizuri.

Ukiona Serikali imechangia sema imechangia.

Na kama kuna sehemu Serikali imekosea ikosolewe Kwa kufuata sheria.

Huo ndiyo mtazamo wa mtu anayesimamia ukweli si mtazamo wa mtu anayesimamia chuki kama wafanyavyo chandimu.

✍🏻Kwa sababu mwisho wa siku kumpongeza Rais kwa mchango wa Serikali katika michezo hakumfanyi Rais awe mfungaji wa bao wala hakumfanyi mchezaji apoteze sifa yake.

📌Ni utambuzi tu kwamba mafanikio ya michezo yanajengwa na mfumo mzima.

Tatizo ni pale tunapofikia hatua ya kusema Mimi sitaki hata jina la Rais litajwe hata pale anapotajwa kwa jambo ambalo Serikali yake imelifanya.

✍🏻Hapo tunapaswa kujiuliza hasa chandimu tunapinga kosa au tumefikia hatua ya kuchukia mtu kiasi kwamba hata jambo jema likihusishwa naye hatutaki kulisikia?

Tuache chuki Tanzania ni yetu sote na Rais wetu tutaendelea kumtaja kupitia mafanikio yake na maendeleo anayotuputaia mungu amlinde Raisi wetu.
 
Back
Top Bottom