lukindo
JF-Expert Member
- Mar 20, 2010
- 8,470
- 9,053
Kwani TTCL kama shirika si unajua ni watu!? Unaposema lilirubuniwa, ni nani hao na walimrubuni nani!? Je, una uhakika hao watu waliohusika kurubuni kama walikuwepo kwa sasa hawapo!?Tuwe wa kweli kuwa TTCL ilirubuniwa ndiyo maana imekuwa ikisuwa suwa.
Hiyo safaricom unayoisifia siyo kuwa wanajua sana biashara bali serikali ya Kenya wamezuia kabisa makampuni mengine kufanya biashara ya simu Kenya.
Mawasiliano kwa sasa siyo kama zamani tulipokuwa na shirika la posta na simu, maisha ya wananchi yamekuwa yakihusika moja kwa moja na mitandao.Tunapokuwa na makampuni ya nje kumiliki sekta ya mawasiliano nchini ni hatari sana kwa Taifa. Nchi zote zinazojielewa hutumia kampuni zao wenyewe kwenye mawasiliano ziwe binafsi au za kiserikali.
Angalizo: Sijasifia safaricom kama unavyosema lakini nilisoma sehemu juzi nikaona turn over yao ni zaidi ya kuunganisha makapuni yote ya simu Tanzania kwa pamoja na bado wasiifikie wakati sisi population yetu ni kubwa kuwazidi!
Pia usisahau kuwa Kenya kuna shirika linaitwa Telecom Kenya ambayo ndio 'TTCL yao', tungeweza kujifunza mengi kama tungetafiti nao wanafanyaje ....wanatoa gawio au wanapewa ruzuku kiasi gani!