TTCL yaomba Sh 1.7 trilioni kuboresha huduma zake

TTCL yaomba Sh 1.7 trilioni kuboresha huduma zake

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,172
Reaction score
60,533
TTCL yaomba Sh1.7 trilioni kuboresha huduma zake

pic+ttcl.jpg

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omary Nundu amesema shirika hilo linahitaji Sh1.77trilioni kuboresha huduma zake za simu za mkononi na mezani.

Nundu ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 21, 2019 katika hafla ya shirika hilo kutoa gawio la shilingi 2.1bilioni kwa Serikali iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.

Source: Mwananchi

Hivi hiyo karibu trillion 2 si wanaanzisha shirika jingine jipya la simu.

Ukitaka vichekesho zaidi bonyeza *nyumbanikumenoga# then piga.

Tunasubiri gawio la ATCL ili tucheke zaidi.
 
Huyu Omary Nundu bado yupoga tu, ma CCM bwana hawawezi maisha tofauti na kujipachika kwenye taasisi za serikali na kuiba iba.

TZS 1.7 Trillion kwa ajiri ya kuboresha huduma za simu za mezani. Nani anatumia simu za mezani siku hizi? Yaani tutumie 1.7 Trillion kwenye obsolete life style? ndio ma strategists wa TTCL hawa?

Mi nilidhani wanaomba hela kwa ajiri ya 5G Technology?
 
Upumbavu ni pamoja na kutokutumia rasilimali zinazokuzunguka kikamilifu, hasa rasilimali fedha, muda na watu.
Huduma za TTCL ni mbovu sana, SMS characters mwisho ni 150/ SMS ukizidisha msg haiendi.
Mitambo yao most of the time IPO offline.
Sitashangaa kusikia hata hilo gawiwo wamekopa sehemu kwa tiba ili tu kumfurahisha Rais
 
Mkuu umeenda mbali sana!! 5G ndy kwanza Tramfu na Huawei wanasumbuana saiv kuhusu Launching.
4G yenyewe Aerial coverage yake kwa hapa Tz bado ni ndogo sana!! Wange-improve hapo kwanza

Ipo tayari, Trump anazungumzia 6G tayari.
wakati hapa Dar kuna 4G kuna maeneo Tanzania hayana access kabisa na internet, sasa hatuwezi kusubiliana. Na nachoomanisha hasa ni kustrategize mambo ya maana sio simu za mezani.

Very very shame! Halafu wanahitaji trl.1.7 wakati wametoa gawio.....
hahahahaha
 
Leo mmejitapa kwamb mmepata faida ya biliom 170 na imekuwa from bilion 120, basi wekezeni hizo halafu baada ya miaka mitano tuu mtapata hiyo 1.7 trillion ni simple math! Au kuna kitu nimekosea? Hahhaahaa oohhh kumbe hamna hela hizo bilion 170 mlikuwa mnamfurahisha mzee? Kazi mnayo.
 
wanahitaji hicho kiasi cha pesa kutoka kwa nani tena wakati huu ni mwaka wa pili mfululizo wao kuigawia serekali yetu pendwa?
Akili yetu Watz ni Mungu tu anayeijua!
Wakati washindani wao akina Voda, Tigo nk wanaitafuta hiyo pesa usiku na mchana kutoka kwa wateja wao TTCL wanaomba kwa serikali ambapo hizo pesa ni kodi za washindani wao. Lakini kwenye gawio hawaiombi serikali "kuwapa pesa ya kutoa gawio kwa serikali"!
 
wanahitaji hicho kiasi cha pesa kutoka kwa nani tena wakati huu ni mwaka wa pili mfululizo wao kuigawia serekali yetu pendwa?
TTCL inahitaji fedha kujenga minara yake nchi nzima badala ya kukodisha ya wengine kwa pesa nyingi. Haya mambo yangewezekana lakini kulikuwa na sabotage katika awamu zilizopita.
 
Akili yetu Watz ni Mungu tu anayeijua!
Wakati washindani wao akina Voda, Tigo nk wanaitafuta hiyo pesa usiku na mchana kutoka kwa wateja wao TTCL wanaomba kwa serikali ambapo hizo pesa ni kodi za washindani wao. Lakini kwenye gawio hawaiombi serikali "kuwapa pesa ya kutoa gawio kwa serikali"!
Sasa kama kulikuwa na viongozi wa serikali waliofanya juu chini kuiua TTCL ili makampuni ya nje waliyoyaleta yafanikiwe, unategemea itashindana vipi?
 
Huyu Omary Nundu bado yupoga tu, ma CCM bwana hawawezi maisha tofauti na kujipachika kwenye taasisi za serikali na kuiba iba.

TZS 1.7 Trillion kwa ajiri ya kuboresha huduma za simu za mezani. Nani anatumia simu za mezani siku hizi? Yaani tutumie 1.7 Trillion kwenye obsolete life style? ndio ma strategists wa TTCL hawa?

Mi nilidhani wanaomba hela kwa ajiri ya 5G Technology?

Halafu tunategemea kuwa middle income economy! Kwa akili ya namna hii??!!
 
Back
Top Bottom