TTCL yaomba Sh 1.7 trilioni kuboresha huduma zake

TTCL yaomba Sh 1.7 trilioni kuboresha huduma zake

Yataka moyo tutakuwa na macho lakini hatuoni tutakuwa na masikio lkn hatusikii tunapofikia ni hatua ya watawanye uwatawale Tunahitaji maombi
 
watanzania tumepatikana,yaani mtu anatoa gawio la bilioni 2.1,huku ana shida ya trilion 1.7,mr misifa umetishaaaaaaaaaaa
 
Yataka moyo tutakuwa na macho lakini hatuoni tutakuwa na masikio lkn hatusikii tunapofikia ni hatua ya watawanye uwatawale Tunahitaji maombi

Ameenen.....!
Biblia inaposema WATU WANGU WANA ANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA ni kama hivi vituko vya Shirika la Posta na Simu.......!!
 
Tuwe wa kweli kuwa TTCL ilirubuniwa ndiyo maana imekuwa ikisuwa suwa.

Hiyo safaricom unayoisifia siyo kuwa wanajua sana biashara bali serikali ya Kenya wamezuia kabisa makampuni mengine kufanya biashara ya simu Kenya.

Mawasiliano kwa sasa siyo kama zamani tulipokuwa na shirika la posta na simu, maisha ya wananchi yamekuwa yakihusika moja kwa moja na mitandao.Tunapokuwa na makampuni ya nje kumiliki sekta ya mawasiliano nchini ni hatari sana kwa Taifa. Nchi zote zinazojielewa hutumia kampuni zao wenyewe kwenye mawasiliano ziwe binafsi au za kiserikali.
ttcl wakawekeza CMDA badala ya GSM ni sabotage????
 
ttcl wakawekeza CMDA badala ya GSM ni sabotage????
Ulimaanisha kusema CDMA?
Haiwezekani zaidi ya nusu ya dunia na hasa ukanda wetu wa Afrika kutumia GSM halafu sisi tung'ang'ane na CDMA, kama siyo hujuma ni nini?
 
Ni sawa kabisa mkuu, lakini kama huna hela hata kuwa na miundo mbinu ya kukuwezesha kupapata faida hilo gawiwo unalipata wapi???
Mmhh!!? Kiongozi unajua maana ya GAWIO au unafurahisha genge!!?

Maswali yenu Mzee Mwanakijiji, amejibu kirefu zaidi ya kile nikilichokisema nyuma.

Haya ndio mambo ninayoyaita watu kujitoa ufahamu. Sasa hapa kuna uhusiano gani kati ya gawio na kutaka kuwekeza zaidi? Mtu anayeangalia kwa juu juu atasema "si wametoa gawio la bilioni 2 kwanini wasibakize hizo na kuwekeza"? Mtu mwenye uelewa atasema "wawekeze kwani fedha zao?". NI muhimu watu kuwa na hoja kama waliopita karibu na majengo ya shule. Ngoja nitoe mifano:

1. Mfanyabiashara anayepata faida ana uamuzi wa kuitumia faida ile anavyoona inafaa. Wakati mwingine faida ile haitoshi kuwekeza kwa kiasi kikubwa hivyo anaweza kuamua kuongeza mkopo (kutoka benki) au kufanya reorganization na cutbacks ili kupunguza gharama.

2. TTCL inawezekana kuwa imetoa gawio kutoka katika faida yake; lakini wakati huo huo inaona inahitaji kupata mtaji mkubwa zaidi ili ifanye makubwa. Sasa kimsingi ni lazima itoe gawio lake au faida yake kunakohusika na halafu iombe hela zaidi za kuwekeza.

3. Sasa serikali inaweza ikaona kuwa iwarudishie kiasi hicho na zaidi wakitumaini kuwa mbeleni TTCL itakuwa na uwezo mkubwa na hivyo gawio halitakuwa tena bilioni 2 bali bilioni 15! Hivyo, gawio linakuwa mbegu. Lakini serikali inaweza kuona kwa wakati huu bado haijashawishiwa kutumia trilioni 1.2 kuwekeza TTCL. Inaweza ikakaa na uongozi na bodi na kusema tufanye nini kupata kiasi hicho nje ya gawio. Ndio ubunifu na uongozi utakapoonekana.

Sasa ndugu zetu waliojitoa ufahamu wanaona kama kuna kujipinga hapa. Kuwa na faida hakuondoi ulazima wa kuongeza uwezo wa kibiashara na si lazima kuongeza huko kote kutoka kwenye kale kafaida!
 
TTCL yaomba Sh1.7 trilioni kuboresha huduma zake

pic+ttcl.jpg

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omary Nundu amesema shirika hilo linahitaji Sh1.77trilioni kuboresha huduma zake za simu za mkononi na mezani.

Nundu ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 21, 2019 katika hafla ya shirika hilo kutoa gawio la shilingi 2.1bilioni kwa Serikali iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.

Source: Mwananchi

Hivi hiyo karibu trillion 2 si wanaanzisha shirika jingine jipya la simu.

Ukitaka vichekesho zaidi bonyeza *nyumbanikumenoga# then piga.

Tunasubiri gawio la ATCL ili tucheke zaidi.
Ha ha ha ha haaaaaa warudishiwe lile gawio walilotoa kwa kujipendekeza ...

Ha ha ha ha ha haaaaaa yaani hi nchi inavituko hiii
 
CCM njooni Basi sijaona comment zenu ...

Kwenye fimbo Kama hizi hua hamuonekani ha ha ha ha haaaaaaa

Wanyonge tunataka mtufafanulie shirika linataka 1.7 trln
 
Ipo tayari, Trump anazungumzia 6G tayari.
wakati hapa Dar kuna 4G kuna maeneo Tanzania hayana access kabisa na internet, sasa hatuwezi kusubiliana. Na nachoomanisha hasa ni kustrategize mambo ya maana sio simu za mezani.

hahahahaha
Kunasehemu nilikuwepo Jana pande za Unyambewa huku nikiwa safarini kuelekea sehemu za Bukumbi huku usumbwani kabisa yaani no network kabisaaaaa ...

Shame on CCM
 
Muwe mnaweka hoja badala ya viroja.
Kuna uhusiano kati ya tabia na umri..... Una maembe 5 unanigawia maembe 2, kisha unaniambia una shida na maembe 15!!!!.... kwanini usikae na maembe yako yote bila kunigawia kisha uombe yanayo kosekana kutimiza idadi unayo itaka??.... Common sense........
 
Ulishawahi kuendesha bishara yoyote?
 
Ninafanya biashara hata dakika hii.
Basi unatakiwa kuelewa kuwa kodi ni lazima ulipe kutaokana na faida unayopata hata kama ni ndogo. Kama utahitaji kuwekeza mtaji mkubwa itabidi utafute vyanzo vingine bila kusumbua uendeshaji wa biashara yako. Njia utakazoweza kutumia kuongeza mtaji ni pamoja na kukopa, kuuza hisa, kufanya joint venture n.k.

Mashirika ya umma nayo yanatakiwa kulipa gawio katika kile wanacho kitengeneza, hiyo ni sheria. Kama yanataka kuwekeza zaidi kwenye huduma yao yana njia zake za kuongeza mtaji ikiwa ni pamoja na kupata ruzuku serikalini, kuomba fedha hazina n.k.
 
TTCL inahitaji fedha kujenga minara yake nchi nzima badala ya kukodisha ya wengine kwa pesa nyingi. Haya mambo yangewezekana lakini kulikuwa na sabotage katika awamu zilizopita.
Waangalie walipojikwaa. Celtel scandal iliwamaliza.
 
Basi unatakiwa kuelewa kuwa kodi ni lazima ulipe kutaokana na faida unayopata hata kama ni ndogo. Kama utahitaji kuwekeza mtaji mkubwa itabidi utafute vyanzo vingine bila kusumbua uendeshaji wa biashara yako. Njia utakazoweza kutumia kuongeza mtaji ni pamoja na kukopa, kuuza hisa, kufanya joint venture n.k.

Mashirika ya umma nayo yanatakiwa kulipa gawio katika kile wanacho kitengeneza, hiyo ni sheria. Kama yanataka kuwekeza zaidi kwenye huduma yao yana njia zake za kuongeza mtaji ikiwa ni pamoja na kupata ruzuku serikalini, kuomba fedha hazina n.k.
Kodi/gawiwo????...........be specific ndugu vinginevyo unaonesha ulivyo amateur.
 
Kodi/gawiwo????...........be specific ndugu vinginevyo unaonesha ulivyo amateur.
Sijasema ni gawio ni kodi nilichosema ni kuwa mashirika ya umma yanatakiwa kutoa gawio kisheria kama vile tunavyotakiwa kulipa kodi kisheria.
 
Back
Top Bottom