Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kueleza changamoto ya kuunganishwa na Huduma ya TTCL Fiber, kupitia ukurasa wa Instagram baadhi ya waliotoa maoni wamedai kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa na tabia ya kuwataka wateja kulipia gharama (Rushwa) za miundombinu ikiwemo nguzo ili waweze kupata huduma.
Kusoma zaidi alichoandika Mdau bonyeza hapa ~ TTCL Fiber kuweni 'serious' na huduma zenu; kama mnaelemewa leteni wawekezaji
Hata hivyo, TTCL wamejibu hoja hiyo kwa kueleza kuwa malalamiko hayo wanayachukua uzito huku wakidai kwamba watachukua hatua kwa yoyote aliyeshiriki, vilevile wamesisitiza kuwa mteja hatakiwi kulipia gharama yoyote ya miundombinu isipokuwa kifurushi kulingana na mahitaji yake.
Ikumbukwe kuwa Mdau wa JamiiForums, kupitia hoja yake alidai kumekuwepo na ucheleweshaji wa kupatiwa huduma kwa zaidi ya miezi sita tangu alipokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Aidha, alidai kuwa wapo wateja ambao tayari wamekamilisha taratibu na kuunganishwa na huduma hizo, lakini intaneti imekuwa ikikosekana kwa wiki nzima licha ya kulipiwa.