KERO Zimamoto ni Huduma, Biashara au Mradi wa Kitapeli?

KERO Zimamoto ni Huduma, Biashara au Mradi wa Kitapeli?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Jeshi la Zimamoto lina jukumu la kuokoa maisha na mali. Lakini kwa muda sasa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya maafisa kujihusisha na utapeli na rushwa wakiwa na sare rasmi za zimamoto na wengine gari ya zimamoto ambayo ikitokea maafa ya kweli hilo gari hutoliona.

images.jpg


Kuna tozo zisizo rasmi wakati wa huduma za zimamoto—hasa kwenye biashara na fremu hasa katika miji midogo Hakuna risiti, hakuna maelezo ya kisheria. Je, hizi pesa zinaenda wapi?

Kuna madai kuwa baadhi ya wafanyabiashara majirani zangu wanatishwa kufungwa au kutozwa faini endapo hawatalipa “makubaliano ya chini kwa chini”. Hii ni huduma ya umma au biashara binafsi?

Wengine wanasema kuna vyeti vya ukaguzi wa zimamoto vinavyodaiwa kutolewa bila ukaguzi halisi—mradi pesa itolewe.

Mimi binafsi nafahamu fremu ya duka inapaswa iwe na Fire Extinguisher ambayo ina gharama ya shilingi 60,000/= . Hizo ada zisizo na maelezo ambazo zimekuwa zikichangishwa kwenye mafremu 200,000-400,000 kutegemea polisi wa zimamoto wamekuona Ng'ombe kwa kiwango gani sizitambui.

Ni wakati wa uchunguzi huru na wa wazi. Taasisi husika zitoe majibu:
– Ada zipi ni halali?
– Nani anazisimamia?
– Kwanini hakuna uwazi wa malipo?

Maafisa waadilifu wa Zimamoto wapo wachache na wanafanya kazi kwa moyo. Lakini wengi wanaharibu taswira ya taasisi nzima

Natoa wito kwa hao maafisa waadilifu wachache Kuchukua hatua. Haya si maneno ya mitandaoni tu—ni sauti za wananchi.

Kero hii inatoka Wilaya ya Kilombero ila nadhani kuna Watanzania wengi wamefikiwa na changamoto hii.
 
Tanzania Kuna Uhuni Sana Kila Eneo Ni Fursa Kuchota Kiwi
 
Hawa jamaa wakikaa ofisini wakaona hawana hela ya bia mfukoni, hao wanakuja kwenye fremu ya kuuza vimaji vya kunywa kudai yanaweza kuja kusababisha moto ulipie garama za fire extinguisher.

Wilaya ya MVomero Morogoro pia hii kero iko juu.
 
Hutaki Abdul aendeshe Rolls royce? Watakuteka wakulawiti na baadae wakuue!
 
Back
Top Bottom