analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 729
- 612
Habari ya leo wadau.
Leo nina kilio juu ya kampuni yetu ya TTCL. Kwa kipindi kirefu kampuni hii imeshindwa kabisa kushindana na makampuni binafsi yanayotoa huduma ya mawasiliano. Kushindwa huku binafsi nilitarajia waliopewa wajibu wa kuliongoza na kusimamia uendeshaji wake wangekuwa wabunifu na aggressive kutafuta huduma ambayo wangeweza kuisimamia na kuendesha shirika kwa mafanikio.
Kuna hii huduma ya Internet ya majumbani na maofisini ya T-fiber, binafsi baada ya TTCL kuianzisha hii huduma niliona ndio chaka lao la mafanikio. Lakini kwa masikitiko makubwa, TTCL wameshindwa kabisa kuendana na kasi ya ukuaji wa mahitaji ya huduma hii kwa watanzania. Katika ulimwengu wa sasa, watu wengi wenye vipato vya kati wangependa kuwa na huduma hii majumbani mwao kwa ajili ya kutumia kusupport devices zinazohitaji mtandao wenye speed, lakini ni huzuni kuona kwamba kampuni yetu hii imekwama kabisa kuendana na kasi ya uhitaji wa huduma hii majumbani.
Kwa masikitiko makuba, imekuwa ni jambo la kawaida kabisa kwa TTCL Dodoma mtu au watu kuwasilisha maombi ya kuunganishiwa huduma, lakini ukakaa miezi mitatu hawajaja kuunganisha huduma, huku wakisema hakuna vifaa, vifaa vimeisha tusubiri mpaka vije.
Hii ni aibu na binafsi ninaona kabisa watendaji hawa wanahujumu kwa maksudi jitihada za muheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan na waziri za kuhakikisha huduma ya internet inawafikia watanzania waliowengi iwezekanavyo. Lakini pia, kwa maksudi wanakosesha mapato serikali, maana hawa watu wanaoomba kuunganishiwa huduma wapo tayari kulipia huduma hii kila mwezi.
Natoa wito kwa Mh. Waziri, angalia watendaji wako katika hili shirika, wengi ni goigoi, wavivu, wasiokuwa na morale ya kuhakikisha shirika linajiendesha kwa faida. Fanya mabadiliko ya haraka ya uongozi hapa Dodoma, jiji linakuwa kwa kasi huku proportion ya middle class ikipanuka kwa kasi sana, watu hawa wanahitaji hii huduma, weka watendaji watakaoweza kuendana nah ii kasi ya ukuaji wa Jiji.
Ni mimi muhitaji wa huduma ya T-fiber, ambae nina miezi mitatu karibu na nusu tangia nimeomba kuunganishiwa huduma bila mafanikio. Nimepigia simu wahusika mara kadhaa nimekuwa nikipewa ahadi, mara vifaa vimeisha, mara vimekuja lakini kwa sasa hatuna ratiba ya kuunganisha huko unakoishi.
Naomba niseme kwamba, nikirudi tena kutoa taarifa hapa, nitataja majina ya watumishi wote ambao kwa nyakati tofauti tofauti nimekuwa nikiwaomba waniunganishie huduma lakini wamekuwa wakinipa majibu ya kukatisha tamaa.