Huduma ya TTCL ya kutoa Internet nyumbani ni mbovu sana

incharge

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,105
3,940
Ndugu zangu ninahitaji kuunganishwa na huduma ya internet ya TTCL nyumbani kwangu.

Kwakweli ni aibu kusema nilikuwa natumia huduma ya Zantel ambayo ilikuwa nzuri na nilipopata changamoto au hitilafu walikuwa wanakuja haraka sana kunipa huduma sema gharama ilikuwa juu kwani nilikuwa nalipa 150,000 kwa mwezi.

Nilienda kwa rafiki yangu mmoja nikakuta anatumia internet ya TTCL na akanishawishi kwa kuwa gharama ni nafuu yani 50,000 kwa mwezi

Cha ajabu nimefuatilia kweli nikaunganishwa ila kwa miezi mitatu sasa imepata hitilafu na sipati huduma na nimefuatilia siku zote hizi bila ya mafanikio

Naomba wadau wa hii kampuni yetu ya kizalendo wanisaidie kwa hili, kama utendaji wenyewe ndio huu mama ana kazi kuyafanya haya mashirika yetu yakawa na tija na kushindana kwenye soko maana hao waliopewa dhamana hawajali hata kidogo
 
TTCL ni kichefuchefu yaan kubwa jinga. Sisi wanatusupply internet ofisini kwetu ni ofisi ya serikali ila mwezi ukipita tu hujalipa wanakata na tuna nunua almost 1.5mil kwa mwezi wakikata hata miezi 2 bili lazima ulipe hata ksma hawajatoa huduma.
Mimi pia niliomba fiber to home nina zaidi ya mwaka wanasema hawana fiber.
 
TTCL ni kichefuchefu yaan kubwa jinga. Sisi wanatusupply internet ofisini kwetu ni ofisi ya serikali ila mwezi ukipita tu hujalipa wanakata na tuna nunua almost 1.5mil kwa mwezi wakikata hata miezi 2 bili lazima ulipe hata ksma hawajatoa huduma.
Mimi pia niliomba fiber to home nina zaidi ya mwaka wanasema hawana fiber.
Aisee hii kampuni gani inakataa wateja jamani huyu mkurugenzi wao kakaa tu ofisini hajui hata huku wateja wake kama wanapata huduma au hawapati
 
huduma ya ttcl internet ni janga la taifa, mimi niliomba waje wanifungie ilikuwa ni kama vita mpaka wanakuja ilikuwa ni mshikemshike kama wa miezi 8 ivi, wana huduma mbovu kupindukia, ZUKU wapo vizuri sana ila tatzio lao hawajafika uku nilipo
 
TTCL ni kichefuchefu yaan kubwa jinga. Sisi wanatusupply internet ofisini kwetu ni ofisi ya serikali ila mwezi ukipita tu hujalipa wanakata na tuna nunua almost 1.5mil
sasa hujalipa usikatiwe? Hii serikali kufanya haya mashirika kama charity kwao ndio sababu yanakufa
kwa mwezi wakikata hata miezi 2 bili lazima ulipe hata ksma hawajatoa huduma.
Hio miezi miwili ambayo ulitakiwe ulipe ila haulipi ? Huenda kuna service charges kwani mkataba unasemaje
Mimi pia niliomba fiber to home nina zaidi ya mwaka wanasema hawana fiber.
kwa hili ni wazembe @TTCL
 
Yes zote ni private kama vile kukiwa na huduma mbovu amana hospital hatuwezi kukaa kimya kisa kuna agakhan hili shirika ni la watanzania lazima litoe huduma kwa ushindani akipewa muhindi akaanza kupunguza watu na kuleta wachapakazi kutoka india hao hao wafanyakazi wa sasa wataanza kulalamika ukweli na wazembe na uongozi mbovu
 
Back
Top Bottom