TTCL ni mtandao unaotumiwa zaidi na matapeli

mangiTz

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,552
2,619
Habari wana JF,

TTCL kampuni ambayo ipo chini ya usimamizi wa serikali una changamoto ya kutumiwa zaidi na matapeli wanaojaribu kutapeli watu kupitia call/sms.

Kampuni kama hii ambayo ipo chini ya serikali tungetarajia kubwa ingefanya vizuri zaidi kwasababu chombo kinachosimamia pia (TCRA) ni chombo cha serikali, lakini imekuwa tofauti katika udhibiti, tofauti na makampuni mengine ya simu.

Wananchi wamepewa utaratibu wa kuripoti namba kama hizi kwa kutuma ujumbe mfupi wa meseji kwenda 15040 kutoka mtandao wowote lakini inaonekana mtandao wa TTCL udhibiti wake upo chini sana.

Ingawa tatizo bado lipo mitandao yote lakini ukiripoti mitandao mingine hulifanyia kazi kushinda huku kwenye TTCL japo mara nyingine inaonekana kama hawafanyi hivyo kwa kuhofia kupoteza wateja sababu hata tapeli huweka vifurushi ambayo ndio sources of income ya kampuni.

TCRA bado kuna kazi ya kuwasidia Watanzania.

Screenshot_20240211-120522.jpg
 
Habari wana JF
TTCL kampuni ambayo ipo chini ya usimamizi wa serikali una changamoto ya kutumiwa zaidi na matapeli wanaojaribu kutapeli watu kupitia call/ sms.

Kampuni kama hii ambayo ipo chini ya serikali tungetarajia kubwa ingefanya vizuri zaidi kwasababu chombo kinachosimamia pia (TCRA) ni chombo cha serikali ,lakini imekuwa tofauti katika udhibiti , tofauti na makampuni mengine ya simu.

Wananchi wamepewa utaratibu wa kuripoti namba kama hizi kwa kutuma ujumbe mfupi wa meseji kwenda 15040 kutoka mtandao wowote lakini inaonekana mtandao wa TTCL udhibiti wake upo chini sana. Ingawa tatizo bado lipo mitandao yote lakini ukiripoti mitandao mingine hulifanyia kazi kushinda huku kwenye TTCL japo mara nyingine inaonekana kama hawafanyi hivyo kwa kuhofia kupoteza wateja sababu hata tapeli huweka vifurushi ambayo ndio sources of income ya kampuni.


TCRA bado kuna kazi ya kuwasidia watanzania
umewatag ili waondoke na watu.?😂
 
Naona hapo ttcl anaongoza kwenye msimamo wa ligi ila wanakimbizana kidogo na airtel.
 
Siku hizi jamaa wa "Ile hela tuma kwenye namba hii" Wanatumia TTCL kwa asilimia 90.

Kama ilivyo kawaida Serikali ni ngumu sana kuendesha biashara ndivyo ilivyo TTCL na ndugu zao Tanesco haya mashirika yauzwe tu ufanisi ni zero.
 
Haishangazi kwa wafanyakazi wa mashirika ya umma.Wanakwenda kqzini kupiga soga na kusubiri mishahara tu sio kufanya kazi tofauti na wafanyakazi wa makampuni binafsi. Utakuta TTCL wameajiri lundo la Cyber security experts ila ndio hivyo tena hakuna wanachofanya na matapeli wameona ni ngumu zaidi kukamatwa ukitapeli wateja wa TTCL kuliko ukijaribu kutapeli wateja wa makampuni mengine hivyo wameona wajikite hapo hapo.
 
Back
Top Bottom