Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.
1. POSTA



Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.
2. KARIAKOO



Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.
3. UPANGA



Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.
4. MAGOMENI



Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.
5. KIJITONYAMA



Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.
6. OYSTERBAY



Barabara ya Haile Selassie.
7. UBUNGO



Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.
8. MBEZI BEACH



Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.
9. TABATA



Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.
10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.



Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.
11. BARABARA YA PUGU



Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.
12. WAGENI



Uwanja wa ndege.
13. PUGU



Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.
14. KISUTU



Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.
15. TEGETA SHOP



Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.
16. MWANANYAMALA SHOP



Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.
17. KURASINI



Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.
Wasiliana nasi:

022 210 0100

0738 151 511
www.ttcl.co.tz
#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645
Karibu.
Rudi Nyumbani Kumenoga