Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Ushauri huu hapaaa...January nenda veta...kasomee welding...Ada 400000...ni miezi mitatu Tu.....ni short kozi...uzuri NI kwamba inaanza mchanaa miss ya saw Tisa....so kwa asubuhi tafuta kijiwe cha kuuza miogo.,......mpaka Sasa Saba utakuwa umepata pesa ya nauli na hata ya Kula...pia na Kodi juu ndani ya miezi mitatu...baada ya kupata ujuzi wako... Kumbuk wakati huo pesa nyingine ilipaki uliyopewa umeweka benk....baada ya kumaliza kozi.....Rudi kwenu mkoani ukiwa tayali na ujuzi wakoo....au Baki bongo uanze Maisha....ninja mashine yako ya welding na vifaa vyote.....utakuwa umetumia kama 70000....tafuta eneo la wazii anzisha hudumaa ya welding.......faida yake.....utakuwa umepata ujuzi wa kudumu....pili Maisha ya uwakika....umejiajilii....mtaji hautopotea....lakinii ukienda tofauti hapoo biashar hauna uzoefu nayo na mtaji utapoteaaa.....wape salaaaaamm...
kingkongtz sijui kama umesoma ukaelewa hiyo comment niliyoi quote kama hujaisoma nakushauri

rudia kuisoma hii comment herufi kwa herufi neno kwa neno ukimaliza nenda kaingie katika utendaji.

nakusihi ndugu yangu usiwe na haraka ya pesa,fata huu ushauri Trust me siku 1 utakuja kumkumbuka TEMBO WANGU
 
Zaidi mwamba watakutisha tuu, usikilize moyo unasemaje. Kama hisia zinakuongoza kwenda dar, nenda mkuu ukapambane. Kwani saivi dar hakuna wanaoanza chini wanafanikiwa? Cha msingi usipoteze focus; nidham, juhudi na uwe na kiu ya mafanikio, trust me chochote utakachoamua ufanye alihali pesa inatosha Fanya, hakuna cha dar sijui kuna changamoto. Changamoto ipo popote, chamsingi uwe na ngozi ngumu na usiendekeze mambo yatakayokutoa kwenye msingi kama starehe. Kila LA kheri mkuu.
 
Kwa pesa hiyo nakodisha shamba hekari 5 nalima mahindi na maharage, Kukodisha shamba Tsh 200,000/=
Naandaa shamba kwa Tsh 300,000/=
Mbolea nanunua kwa Tsh 300,000/=
Mbegu nanunua Tsh 200,000/=
Gharama za kupanda Tsh 200,000/=
Kupalilia ×2 Tsh 200,000/=
Kuvuna Tsh 200,000/=
Jumla kuu 1,600,000/= unabaki na laki nne ya kulinda mfuko.
Ndani ya miezi 3 utavuna maharage si chini ya gunia 5 @Tsh120000~150000/=kwenye maharage utapata Tsh 500,000/=~700,000/=
Baada ya miezi 4 kwa hekari 5 utavuna gunia 70~90 kutegemeana na eneo la shamba.
Tufanye upate gunia 75 yaani kila hekari moja itoe gunia 75, gunia moja uuze kwa Tsh 50,000/= unapata million 3.5 ndani ya miezi 4 faida Tsh 2M.
Umesahau kuweka gharama za pump ya kumwagilia na kuchimba kisima.

Vv
 
Habari.

Nahitaji mchango wako wa ufafanuzi wa kazi ambayo anaweza kuifanya kijana mlemavu kwa mtaji wa Tsh 2,000,000 pasipo kumletea madhara au kushindwa kuisimamia kazi yake. Tuchukulie mfano wa mlemavu wa miguu lakini mwenye uwezo wa kutumia mikono (wote: msomi, sio msomi)

Nikimaanisha kwamba ushauri wa kazi kwa mlemavu anayefahamu matumizi ya Computer kwa kaz za kiofisi na kwa mlemavu asiyefahamu matumizi ya Computer kwa kazi za kijasiriamali (wote wanaweza kutumia mikono lakini sio miguu).

Ushauri unaweza kuwa kazi ya aina gani afanye, ataweza kuifanyia mahali gani (nyumbani, ofisini, nk) mchanganuo wa mtaji (na faida, hasara), na changamoto za kazi hiyo ikiwa unazifahamu.

Asante.
 
Maoni yangu ni kuwa kazi nyingi zinazoweza kufanywa na watu wasio na ulemavu zinaweza pia kufanywa na walemavu. Ni dhamira na nidhamu ya anayefanya tu.
 
Kuna mlemavu wa miguu yuko Dodoma pale eneo la duka la cityboys kama sikosei,anauza chumvi za pakti 3 buku,anauza kweli yaani Mimi nilikuwa mteja wake wa kudumu!!!
Ushauri wangu asitafute biashara kubwa saana,aangalie tu biashara ndogo inayouzika kwa wingi eneo lenye muingiliano mkubwa wa watu!!!!
 
Asante sana, ni kweli kabisa! Kunao vijana watatu wenye ulemavu lakini wanaakili sana na wazazi wao wapo tayari kuwapatia mtaji wa mil. 2 kila mmoja, nitazungumza nao juu ya jambo hili walau kuwatia moyo wapate uthubutu wa kufanya kazi.
 
Kuna mlemavu wa miguu yuko Dodoma pale eneo la duka la cityboys kama sikosei,anauza chumvi za pakti 3 buku,anauza kweli yaani Mimi nilikuwa mteja wake wa kudumu!!!
Ushauri wangu asitafute biashara kubwa saana,aangalie tu biashara ndogo inayouzika kwa wingi eneo lenye muingiliano mkubwa wa watu!!!!
Asante sana, ushauri mzuri. Naamini kijana yeyote mlemavu na mwenye uthubutu bado ana uwezo wa kufanya kitu kizuri ikiwa ataamua.
 
Auze duka dogo la accessories za simu na electronics ndogo kama saa, Bluetooth speaker, radio, headphones, etc. Hizi hazimzungushi sana mtaani tofauti na kuuza vitu perishable kama vyakula ambavyo huisha haraka ila vinataka kuagiza mara kwa mara na vinaharibika. Hapa anacheza na inventory control.

Auze vipodozi kidogo ila hapa atatakiwa mtaji wa hata 4M ila akianza na 2M sijui. Hivi anatakiwa ajue maelezo yake na kujua ushauri wa matumizi maana Washahili huwa hawasomi maelezo ila uuliza muuzaji. Kichaka cha kuanzia huwa ni perfume, Vaseline, mafuta ya nywele, etc vile ambavyo si complicated.

Mwingine aongeze
 
Mtoa mada chukua huu ushauri.
Hizi ndizo biashara zinamfaa ongezea na Mpesa/Tigopesa/Airtel money.
Hizi zinamfaa kwa sababu haimfanyi kuzunguka mitaani na pia habebi vitu vizito.

Basi hadi umewaza biashara , ni wazi ulemavu si kikwazo kwako. Fanya mradi wa kukaa sehemu moja kisha uwe na mtu kama bodaboda,ukimpigia simu alete mzigo, fasta anakufatia duka la jumla ulomwelekeza. The rest is history
 
Aisee! Huu ni ushauri mzuri sana, nimependa sana hii idea ya duka la accessories za simu ndogo na electronics kwasababu kwa mtaji wa 2M inawezekana kuanzia, na ni kazi ya kukaa tu sehemu moja. Hili wazo nitalifanyia kazi 🙏
 
Mtoa mada chukua huu ushauri.
Hizi ndizo biashara zinamfaa ongezea na Mpesa/Tigopesa/Airtel money.
Hizi zinamfaa kwa sababu haimfanyi kuzunguka mitaani na pia habebi vitu vizito.
Ndio, asante sana. Katoa ushauri mzuri na nitaufanyia kazi, asante kwa ushauri wako pia 🙏
 
Basi hadi umewaza biashara , ni wazi ulemavu si kikwazo kwako. Fanya mradi wa kukaa sehemu moja kisha uwe na mtu kama bodaboda,ukimpigia simu alete mzigo, fasta anakufatia duka la jumla ulomwelekeza. The rest is history
Ni ushauri wenye maneno machache lakini very powerful ukiutafakari kiundani. Asante sana ndugu, hii nitafanyia kazi pia 😍
 
Back
Top Bottom