Tsere balozi mpya Malawi (Mpinzani wa Dr.Slaa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tsere balozi mpya Malawi (Mpinzani wa Dr.Slaa)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Feb 27, 2010.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  na Marietha Mkoka, DSJ

  RAIS Jakaya Kikwete amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam, Patrick Tsere kuwa balozi mpya nchini Malawi.

  Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa vyombo habari, ilisema Tsere anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Makame Rashid ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishu wa umma. Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema Tsere ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala tangu mwaka 2006 hadi 2009.


  NB: Atakwenda tena Karatu kugombea Ubunge kama ilivyokuwa mwaka 2005??
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Whaaaaaat? Sasa JK hayuko serious...wadau hebu mwenye CV ya huyu mkuu atupe.Ambassador?
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aliwahi kuwa mkuu wa kule Arusha International conference center (AICC) kabla ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Ilala,
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Tafadhali usimuonee muungwana; he has never been serious in his life, he is always smiling!! Alinikuna juzi alipotembelea waliokumbwa na mafuriko Kilosa alipowaagiza watu wake wawajengee nyumba upesi kwani watu wazima wanachoka kuwafukaza ndani watoto waende kucheza ili wapate faragha!!! Is n't this hilarious from your commander in Chief!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  huyu jamaa ni failure mtupu, ilala wananchi walimkataa huyu, km sikosei ilikuwa sakata fulani la ardhi
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  I beg to differ hapa mkuu, Tsere ana qualities zake iwapo atapata nafasi kwenye sehemu inayomfaa, nahisi kwamba ataweza diplomacy hasa kwa nchi kama malawi ambayo kwa kweli hatuna serious issues hapo. he did relatively well kule AICC.

  Hii ya ukuu wa wilaya ndugu yangu si rahisi kupima mtu kwani ni siasa na uzandiki mtupu uko kwenye hizo position, manifesto zao za kazi na mazingira yao hayawezi kumsaidia any intelligent person ku-achieve goals zake, sanasana uwe mwanasiasa upige kelele siku ziende and Tsere is not that type of political blahblah

  nawasilisha
   
 7. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kumbe hiyo CV yake hata wewe huna, sasa kinachokupayusha 'whaaaaaat' ni kitu gani?
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  Mimi ninavyomjua huyu mkuu alikua mkuu wa wilaya,sasa kweli ni ishu gani iliyomsukuma jk aone anaweza kuwa ambassador uko malawi?Hebu tunaomba CV yake kitaaluma coz ukuu wa wilaya tu ndo umemfanya awe qualified kuwa balozi?Huoni tatizo hapo?

  Kwa anayesema malawi hatuna serious issue nayo9 simwelewi pia,unajua nchi kama malawi iko ktk strategic location?

  Tuna watanzania wanafanya biashara malawi,and there are still some more opportunities kwa watanzania kuwekeza kule

  Pia Tunahitaji wateja kwa ajili ya bandari zetu ingwa ziko hoi,pia cooperation in defence nk....usiseme hatuna ishu serious na malawi,basi ubalozi wetu huko ufungwe?
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Hakuna kazi kwenye balozi zetu zaidi ya kupiga simu, soga na kutafuna fweza za walipa kodi. Any tom dick and harry can be an ambassador. Kama JK kawa rais why not others. Ndio Tanzania hiyo hakuna lolote la maana ni blah blah za kukutana kijiweni tu na kupasiana tonge za ugali.
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,316
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  By the way kwenye ubalozi kuna kitu gani cha tija sana? bora kuwa wachapakazi watakaokuwa wilayani kusukuma maendeleo ya wananchi mbele na waliochoka wapelekwe kwenye balozi chovuchovu kama burundi, malawi, zimbwi n.k. Kwangu mimi naiona nafasi ya ukuu wa wilaya kuwa ya manufaa zaidi kwa Watanzania kama tutapata mchapakazi kuliko kuwa na mchapakazi balozi nchini malawi.Shida nyingine ni kuwa wakuu wa wilaya wapo kwa matwaka ya kisiasa na wala sio kwa ajili ya maendeleo ya watanzania husika
   
 11. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,465
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Hayo ndiyo maajabu ya JF siku hizi
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  Mkuu,

  Mtu kuongoza foreign mission ya Tanzania si masikhara.

  It's like watu hawaoni hata umuhimu wa kuwa na ubalozi huko malawi?

  Malawi tunawahitaji ktk ushirikiano wa kibiasharaespecially kama bandari zetu zitakua ktk hali nzuri katika matengenezo yatakayofanyika.

  Pia,tunawahitaji ktk ushirikiano wa kiulinzi

  Tunahitaji mtu mwenye uwezo wa kusimamia na kuongoza maslahi ya Tanzani na watanzania huko Malawi.

  Nadhani inabidi kuwa makini zaidi katika teuzi hasa za mambalozi wetu.

  By the way,CV ya Tsere kitaaluma imekaaje?hilo ndilo la msingi zaidi..si ukuu wa wilaya tu
   
 13. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,494
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 145
  Sifa za kuwa balozi ni zipi?.
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,771
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani Balozi wetu huko Malawi lazima aelewe kuwa kumekuwa na dispute ya muda mrefu kuhusu ulipo mpaka wetu Ziwa Nyasa (wao wanaita Malawi)...wakati sisi tunajua unapita kati kwa kati, wao wameona ziwa lote upande wa Tanzania ni la kwao.

  je huyu ataweza kusukuma suala hilo pamoja na mengine yakiwamo ya detention za gafla gafla za wafanyabiashara wa TZ huko Malawi?
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Hasa katika defence cooperation,yaani kuwa mkuu wa wilaya ambaye kiitifaki ndiye mwenyekiti wa kamati za ulinzi za wilaya ndiye anapelekwa kuwa head of our mission abroad?

  Ndo maana nikahitaji hata CV yake ili tuone ana nini huyu mkulu otherwise Jk atakua incompetent in appointing our foreign envoys!

  Kwanza amekua foreign ministers for ten years bila shaka anajua foreign policy yetu kwa malawi ni nini,na pia foreign policy ya malawi kwetu ni nini.

  Pia i hope amezingatia maslahi yetu huko SADC na maslahi ya watanzania kiujumla huko Malawi.So,kama alifikiria haya yote ndipo alipomteua mkuu wa wilaya Patrick Tsere akaona uwakilishi wake ktk wilaya ya ilala ni sawa na kuongoza foreign mission yetu nje!
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,771
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  mkulu, hizo ni 'assumptions' tu lakini unaweza kukuta wala hajagusa any of the criteria.

  ndo maana ni muhimu CV yake ikapatikana hapa, lakini sishangai kama haitapatikana manake sidhani kama Balozi mpya amekuwa so influential manake kama mkuu wa wilaya kuna yule mh Mnali...alichapa walimu viboko hadi leo wanamkumbuka. huenda tunamhitaji kama huyu
   
 17. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wana JF mliochangia Patrick Tsere ninayemjua mimi si huyo ambaye baadhi yenu mmekuwa mkimuelezea with an exception of De Novo. Tsere ambaye Baba yake mzazi alikuwa miongoni mwa madaktari wa awali hata kabla Tanzania haijapata uhuru, alipata formal education kuanzia primary, middle school, secondary (O level) na High School (A level). Baadaye akaenda IDM Mzumbe alikopata Diploma in Public Administration na baadaye akapata Post Graduate Diploma in Management. Aidha anayo MA in Diplomacy.

  Amefanya kazi kama Afisa Mipango Wilaya ya Iringa; Manpower Officer Wizara ya Mipango na Uchumi; Wizara ya Mambo ya nchi za Nje (mwaka 1983 hadi 1996 kama Afisa wa Ubalozi ubalozini nchini Zambia wakati huo Ubalozi wa Tanzania ulikuwa pia unatuwakilisha nchi ya Malawi na Botswana); Akaja kuwa in charge of operations idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 1997 to 2002; 2002 to 2005 akawa CEO wa AICC Arusha baadaye akaenda kugombea ubunge kwao Karatu. 2006 hadi 2009 akawa DC Ilala.

  Kwa ufupi hiyo ndiyo CV ya Tsere. Sasa kama inakidhi hizo concerns zenu ninaamini ndani ya CV hii mtapata majibu. Kwa mfano tatizo la mpaka kati ya Malawi na Tanzania hilo ni tatizo tangu enzi za Mwalimu. Sitaki kuamini kuwa Tsere halijui kwa vile akiwa afisa ubalozini Lusaka, nchi ya Malawi ilikuwa sehemu ya brief ya ubalozi wetu na sina shaka tatizo hilo atakuwa analifahamu vizuri sana.

  Bila shaka CV hii itakupeni picha ya kuwa Tsere hakubebwa. Ni dhahiri he is fit for the job as he has the required qualifications as well as the expertise, na aliempa hiyo kazi hakukosea. Ninawaomba wanaJF wenzangu kumbukeni ule usemi "No research no right to speak"
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280

  Mkuu nashukuru sana.Hiki ndicho nilichokitaka

  Mimi sijamuongelea huyu mkulu kwa mabaya ila nilikua concern na suala la CV yake na hasa kitaaluma.

  Ndiyo maana nikashangaa kama ni uku wa wilaya tu uliompeleka huko Malawi.so hizo post ni relevant coz hakuna mantiki ya kuwa na balozi asiyeweza kubeba au kuongoza mission yetu nje,vinginevyo hata huo ubalozi hauna maana.

  Nashukuru sana ila ili kuweka record clear alisomea wapia MA diplomacy?hebu tuwekee katika mtirirko unaofa kama unaweza mkuu.
  Respect sana
   
 19. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,396
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  labda baadhi ya wachangiaji wangefanya utafiti wao kuhusu hili vyema
  hata tone ya michango yao ingebadilika.

  binafsi niliamini kabla ya kumpiga madongo wachangiaji wangekuja na ushahidi/tuhuma za bw.tsere kushindwa kutekeleza majukumu aliyokabidhiwa kwa ufanisi.
   
 20. tru rasta

  tru rasta JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 259
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Nono it seems hujui how the system is,practically ukuu wa wilaya na mkoa in this country umebaki kuwa position zisizowasaidia wananchi wa wilaya au mkoa husika since they are not put in power na wananchi.Wanateuliwa na Rais to do wat he wants!kwenye balozi thats where real issues are n dont b fooled kuwa hawahitajiki watu walio makini huko,tatizo kubwa tu kwenye kipindi hiki cha uongozi fadhila ndio sababu ya kuteuliwa na sio uwezo.Jk is nat serious
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...