Je, Rais kavunja Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023 kwa kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama kuwa Balozi?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,586
17,694
Nawasalimu Kwa jina la JMT...🇹🇿

Jana katika pita pita zangu nilikutana na Taarifa kutoka ikulu ikisema kuwa Rais amemteua Bw Hussein Massoro Kuwa balozi na kumuweka Balozi Ali Idi Siwa kuwa DG mpya TISS. (kongole kwake).

Japo jambo hilo lilizua mijadala mingi ikiwemo uwepo wa Tengua tengua Ya Wakurugenzi wa TISS kwa kipindi kifupi cha miaka mitano Ambapo mpaka sasa Wakurugenzi wapatao 3 tayari wamekwisha badilishwa, Na wengi wakahoji kuhusu Usalama wa Taarifa za kiulinzi za nchi na Kusema Huko TISS kuna siri gani Inayofanya kubadilishwa kwa Wakurugenzi mara kwa mara?.

Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6(6) Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.

Au ilipotungwa sheria hiyo ilikuwa Tamu sehemu ya mamlaka ya TISS ila sehemu ya upande wa utawala haikuonekana?
 
Hamna Jambo hunikera kama kumwita raisi mama,mama ni nyumbani kwake,acheni uchawa ulopitiliza
Au we ngumbaru,ukiingia kwenye ofisi za watu badala ya kuadress watu kwa vyeo vyao unakela kujikombakomba,na shemeji,shangazi,mjomba🤣🤣
Mama ni neno lenye heshima linalodhihirisha Heshima kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke mwenye umri Mkubwa kumzidi au mpaka na hilo swala Niwaite BAKITA au nimuita Sigara akufundishe.....
Kwa mfano kwa Wazungu huitana Ma'am (Au madam) kwa kiswahili Mama...
miss ,Mr,Mrs na mengineyo hizo ni prefix za heshima nenda ujifunze boss
kingine...

vyao unakela kujikombakomba,na shemeji,shangazi,mjomba🤣🤣
Sio unakela ni Unakera...

Kifupi watu kumuita Rais Samia mama haijaanza leo akiwa Rais imeanza Tangu akiwa katika Harakat za kugombea akiwa makamu wa Urais wa Jiwe kama utarejea kumbukumbu zako vizuri Kipindi cha kampeni na sio hapo tu kama una umri mkubwa utagundua kuwa ilianza zamani tangu akiwa waziri na hata alivyokuwa katika bunge la katiba so I think kam huna heshima basi baki nayo mimi mtu yyte ambaye nampea heshima hata kama kanizidi miaka mitano mbele bila kujali Hadhi yke ya pesa awe maskini au Tajiri humpa heshima hiyo
 
Raisi wa Tanzania yupo juu ya sheria. Hata akiamua leo kijazi intechange ibomolewe inabomolewa tu.

Nafikiri ndiye Raisi anayeongoza watu wajinga zaidi Duniani kwa sasa.
Ujinga wetu unajidhihirisha pale umeme unapokata from saa kumi na mbili asubuhi ukirudi jioni tunapiga kelele huooooooo!!! Kama mazombi!

Watoto nao utasikiaa huoooooooo!

Mtaa wa pili huooooo
 
Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6 ibara ya 6 Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa...
Duh!!! Kwamba ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali imelala fofofoo!
 
Nawasalimu Kwa jina la JMT...🇹🇿

Jana katika pita pita zangu nilikutana na Taarifa kutoka ikulu ikisema kuwa Rais amemteua Bw Hussein Massoro Kuwa balozi na kumuweka Balozi Ali Idi Siwa kuwa DG mpya TISS. (kongole kwake).

Japo jambo hilo lilizua mijadala mingi ikiwemo uwepo wa Tengua tengua Ya Wakurugenzi wa TISS kwa kipindi kifupi cha miaka mitano Ambapo mpaka sasa Wakurugenzi wapatao 3 tayari wamekwisha badilishwa, Na wengi wakahoji kuhusu Usalama wa Taarifa za kiulinzi za nchi na Kusema Huko TISS kuna siri gani Inayofanya kubadilishwa kwa Wakurugenzi mara kwa mara?.

Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6 ibara ya 6 Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.

Au ilipotungwa sheria hiyo ilikuwa Tamu sehemu ya mamlaka ya TISS ila sehemu ya upande wa utawala haikuonekana?
Si amemtengua kama DG ndio akamteua kuwa balozi, labda kama Sheria hiyo inasema hata kama akitenguliwa wadhifa huo.
 
kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6 ibara ya 6 Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.
... Mkuu, hebu c&p kifungu husika cha hiyo sheria.
 
Back
Top Bottom