Trust katika Mahusiano

Halikuwa la kulinyamazia kinya rafiki...but nilihitaji energy na utulivu....sikutaka kulizungumza nikiwa na hasira.....but i told him straight to his face...siku ambayo hakutegemea
Big up. Ulifanya vizuri mwee , yaani nimeipenda hiyo hii kitu kuweka moyoni halafu unazeeka usoni haifai kabisa na haina nafac. Mimi sinaga cha kuweka moyoni aisee. Nadhani siku nyingine itambidi ajitahidi sana kutafuta uongo uliojificha ili uamini lkn sidhani kama utaweza kua na courage ya kumpa pesa na ikibidi apewe basi akirudi lazima ailipe tu.
 
Eti si umeshapenda teeena......umekufa umeoza....huoni...huambiwi....haha haaa...jamini sisiiii
Mmmh haya mapenzi yasiyokua na macho huweza kukuongoza shimoni au kwenye msitu lol. Siku hizi mapenzi yana macho na yale mambo ya kizamani ya kuzeeshana kwa kumesa vitu au kuweka kifuani no hii mbaya sana mama angu.
 

Yaani you said...ukisema uyabebe moyoni utayabeba mangapi? Utayaweza kwanza? Ili uwe na amani hunabudi kuyatoa ili yakutue....kumpa tena pesaaa...?.yaani hapo ndo ilikuwa stop.
 

Hapo hakuna tija kabisa na huo ndiyo ninaoita upuuzi...

Hata kama hakuwa na nia ovu...hilo kosa linaonesha bila chenga kwamba alikuwa anatenda dhambi...

Ni dhambi gani....hapo akili mu kichwa...!!

Exactly, hayo ndo maswali niliyouliza kabla sijasoma hii post yako, kwa nini adanganye location? kwa faida ya nani?

Hizi sasa ndiyo tunasema ni uongo wa kipuuzi.

Hata kama mtu anaamua kucheat, anaweza kueleza vizuri tu kwamba yuko Dar na bado akaendelea na uchafu wake..

Ila kufanya makosa ya kiufundi kama hayo, ni kuweka mahusiano rehani...

Babu DC!!
 
Mmmh haya mapenzi yasiyokua na macho huweza kukuongoza shimoni au kwenye msitu lol. Siku hizi mapenzi yana macho na yale mambo ya kizamani ya kuzeeshana kwa kumesa vitu au kuweka kifuani no hii mbaya sana mama angu.

Kwanza magonjwa ya moyo nje nje siku hizi...cha kufia nini mmekutana ukubwani? Kalelewa kwao umelelewa kwenu...hapanaa
 

Alijua ataenda salama na atarudi salama......jua likamuangaza....uongo ukipitiliza haufai a.k.a UPUUZI
 

Na lazima umsamehe....ili maisha yaendelee..eti dada RED
 
Hizi sasa ndiyo tunasema ni uongo wa kipuuzi.

Hata kama mtu anaamua kucheat, anaweza kueleza vizuri tu kwamba yuko Dar na bado akaendelea na uchafu wake..

Ila kufanya makosa ya kiufundi kama hayo, ni kuweka mahusiano rehani...

Babu DC!!
sikutamani kabisa kuongelea hili hapa, lakini ngoja niseme tu.
kuna siku nilipigiwa simu na mama wa dada mmoja ambaye nilimsimamia ndoa. huyo dada sipo close naye ila waume zetu ni marafiki sana. huyo mamake aliponipigia akaniambia anajua sipo close sana na mwanaye lakini anaomba tu aniulize hilo swali, kama mwanaye yupo kwangu. nikamwambia hayupo akaniuliza mara ya mwisho kumwona nikamwambia, ilikuwa muda mrefu umepita. akaniambia nimwambie kama nipo home anataka kuja, nikamwambia hapana mama, nitakuja kwako. basi nikaondoka mpaka kwa mama.
Kufika hapo mama akaanza kulia, nauliza vipi? ananiambia kapigiwa simu na mume wa huyo dada (mkwe wake) kutaka kuongea na mkewe ambaye kaaga kwake anakuja kwangu. hapo akawa kanichanganya. akasema ni hivi, jana yule binti kaaga kwa mumewe naenda kwa mama na atalala huko, kumbe sijui kaenda wapi, na mbaya zaidi kazima simu hapatikani. Mumewe usiku umefika, anataka kumpigia mkewe amwambie gudnite simu haipatikani, akajua mambo ya mitandao au charge. akalala, kesho asubuhi kapiga simu hola, mchana hola, mmmhh akaanza kuwa na wasiwasi mkewe asije ikawa yupo Muhimbili au Mwananyamala, akaamua ampigie mama mkwe.... mama anakataa sijaona binti wala hata hakunipigia kuwa anakuja home. kazi ikaanza hapo........
unajua alipatikana baada ya wiki ndo karudi home, mzima wa afya.......
hivi mtu kama huyu unamfanyaje?
 
maweeeee dah uuuwiii ujue nilikuwa nachukia sana hawa kaka zetu..unataka kunirudisha huko eeeh?
 

Hivi kupiga mtu chini ukaanza upya ni jambo gumu sana kiasi cha kujiuliza mara mbili mbili??

May be kwa sababu hayajanikuta...ila kama akili yangu hii bado iko intact..not compromised kwa mizizi au vidonge...

Haki ya nani nitakuwa tayari kuishi kama mtawa...

Ila na wewe uwe unamalizia hadithi basi FP ...

Babu DC!!
 
maweeeee dah uuuwiii ujue nilikuwa nachukia sana hawa kaka zetu..unataka kunirudisha huko eeeh?


Kuwachukia haiwezi kukusaidia kitu Smile...

Bora kuwaelewa na kutafuta mbinu za kuishi nao.....


Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
ha haaaa, na mimi nilijua tu babu utatamani hadithi imaliziwe, umegundua ndo mtindo wangu? isije ikawa wenye stori wakawa wanapita humu halafu wakaona mimi ndo namwaga stori zao huku......nilichotaka kukisema kimeeleweka.
Ila babu kupiga mtu chini pia ni ujasiri, siyo wote wanao huo ujasiri.
na ndo maana Mungu anampangia kila mtu na wake, kwa uvumilivu wako wewe ndo maana akakupa bibi maana alijua angekupa kama huyo basi kila siku kungekuwa na harusi yako, lol!
 

Harusi kila siku ya nini bwana?

Ningeamua tu kuishi kama Mtawa wa kiume na kuelea wanangu basi....

Kwa nini nisumbue akili zangu kwa sababu ya watu wengine???....

Babu DC!!
 
ha haaaa, kwanza salamu zako nyingi sana kwa snowhite, eti alikumiss sana....... na wewe anajua ulimmiss.
eti.... unadhani nikimwambia ukweli teja kuwa nina mpango wa kando naweza kesho yake onekana huku JF just sababu nilisema ukweli?
FP hapa hutaonekana manake nahisi utakuwa ICU kwa kipigo...ukweli gani huo unasema kwa teja? Si nimesikia kuwa huhesabiwi mwongo kwa kukataa kusema ukweli wenye.madhara zaidi kuliko faida.

Asante kwa salam snowhite, nimemmiss kweli sijui amepatwa na nini....homework zotr nshamalia
 
Last edited by a moderator:
Harusi kila siku ya nini bwana?

Ningeamua tu kuishi kama Mtawa wa kiume na kuelea wanangu basi....

Kwa nini nisumbue akili zangu kwa sababu ya watu wengine???....

Babu DC!!
we unafikiri utawa mchezo...... jela tu mtihani sembuse utawa!
acha kabisa kusikia hizo habari
 
hawezi kunibakisha nifikishwe ICU, yaani kesho yake kutakuwa na mabandiko ya RIP hapa.....
kabisa, nimwambie nina mpango wa kando halafu atoe kipigo, kwani ile bastola alishaisalimisha kwa Kova?
 

Kisa chako hapo juu kimenikimbusha class mate wangu afu alikuwa wa kwetu pia, so mama ya te nilikuwa namwita shangazi. Tulimaliza wote primary secondary tukaachana, but likizo tukawa tunaonana, tukamaliza o level tukaenda advance but shule tofauti but kizamani zamani tukawa tunaandikiana baru.

Sasa kumbe kule shule alikoenda alianza tabia mbaya...i mean A level...likizo akawa haji nyumbani kwetu tena, na hata tukienda kwao anakuwa na nyodo nyodo flani....mie tena nikaamuka kukata urafiki mazima.

Kumbe yeye ana ishu zake...so anaaaga kwa shangazi kuwa anakuja kwetu akati haji, kipindi hicho no cell phone..ukitaka taarifa lazima uchape lapa, TZ 11 ili ukazipate. So alikuwa analala anakokujua akiulizwa anasema kalala kwetu.

Mama mtu akashuka....mboma mwanae ndo anakuja kwetu but sisi mda mrefu umepita hatukanyagi kwao? Wakatuma mtoto wao mwengine kuja kuliza....nyumba nzima tukashangaa...maana hatujawah kumtia machoni....basi wazazi wke wakazani tunatania.

Wakaja, intentionally kunisakama mimi nieleze mtoto wao alipo maana eti siku zote akiaga anasema anakuja kwa KOKUTONA mmmh eti ni siku ya 3 hajarudi na wao wanajua yuko huku.....ikabidi liongelewe kwa mapana na marefu na wakagundua mtoto wao amewaingiza mjini....lakini ndo nilikuwa nimeigizwa kwenye janga nisilolijua.....kisa UONGO.

Wlikuja kumpata mahali ambapo walikuwa shoaked
 
hawezi kunibakisha nifikishwe ICU, yaani kesho yake kutakuwa na mabandiko ya RIP hapa.....
kabisa, nimwambie nina mpango wa kando halafu atoe kipigo, kwani ile bastola alishaisalimisha kwa Kova?
FP lol kumbe ana kamguu ka mtoto? Mubaya huyo? Hahahahaha

So the rules must be respected...kuna.aliyesema apa kwen uzi kwamba turipoti iyo makitu for the sake of truth?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…