Treni yasababisha ajali

Uswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,204
Reaction score
627
Treni iliyoanza kazi jumatatu tayari imeua mtu mmoja.

Taarifa za kuaminika ni kwamba mtu huyo alikua karibu sana na reli na alikua anajaribu kuichungulia kadiri ilivokua inapita, aligongwa na behewa na kufariki papo hapo.

Source mimi mwenyewe, marehemu tulikua tunaabudu nae kanisa moja.

Wito:
Hizi treni zitasaidia sana lakini inabidi usalama ikiwa ni pamoja na elimu kwa uma viwekewe mkazo sana!
 
Huo upumbavu wa kwenda kulichungulia treni kajifunza wapi?? Kanisani au kijiweni??
 

.............. kuna watu ambao hawajawahi kusafiri na treni, pia kuna watu hata kule kuiona ni kwenye magazeti na tv.... na wapo watu ambao tangu wamekuja DSM wanaishia kwao Vingunguti hawajawahi kufika katikati ya jiji ...posta hawakujui...... sasa hapo kazi ipo.............

 
Huo upumbavu wa kwenda kulichungulia treni kajifunza wapi?? Kanisani au kijiweni??
I'm so sorry for the deceased but it his/her own fault!rest where you deserve.
 
mungu amlaze pema peponi na wengine waache kuchungulia
 
hivi hapa mjini bado tunashangaa gari moshi mpaka sasa?
 
alikuwa anaichungulia tren kadri ilivyokuwa inapita,sasa apo nani mwenye makosa!! kwanini aichungulie? watanzania tuache kushangaa ayo ni mambo ya kawaida,wakiendekeza kuchungulia tren wataondoka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…