Njozi ya Mwanakijiji: Tanzania kama Nigeria

MKURABITA

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
317
126
Njozi ya Mwanakijiji

Na M. M. Mwanakijiji

KATIKA sehemu ya kwanza, nimejikuta nikisafirishwa kutoka katika ukingo wa Mto Detroit nchini Marekani hadi ufukweni mwa Bahari ya Hindi. Niliamshwa na uwepo wa mtu ambaye sikumjua ni nani.Kiumbe yule licha ya kuwa na maumbile ya mwanadamu nina uhakika kabisa hakuwa mwanadamu. Vitu vitatu vilinifanya niamini kabisa kuwa nilikuwa nimesimama mbele ya kiumbe kutoka nje ya dunia hii tunayoishi wanadamu.

Kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza sijui kama ilikuwa ni ndoto, njozi au maono au ilikuwa ni kweli inanitokea. Ninachojua ni kuwa naweza kukumbuka kila kitu kama vile ninavyokumbuka siku ya leo.

Kwanza, ilikuwa ni rangi yake. Hakuwa na rangi kama hizi za wanadamu. Ukimuona Mchina, Mhindi, Mwarabu, Mwafrika, Mzungu au mtu aliyechangia damu unaona kabisa rangi za kibinadamu. Binadamu tunatofautiana rangi mbalimbali na hata maumbile yetu ya nje lakini rangi zetu tunazijua na tofauti yoyote ya rangi ni rahisi kuhisi mtu anatokea wapi.

Mtu yule hakuwa na rangi za kibinadamu, alikuwa na rangi ya kijivu inayong'ara au zaidi niseme inametameta. Ni sawa kama na rangi ya fedha yenye vile vidude vya mapambo vinavyometameta.

Hiyo rangi ilinishangaza kwa sababu sijawahi kuona picha, au mahali popote kuwa wanadamu wanaweza kuwa na rangi ya namna hiyo, na hivyo nilimuangalia kuanzia miguuni hadi kichwani na rangi ile ilinishangaza. Nywele zake zilikuwa kama za mtu mweusi katika mtindo wa afro; zilikuwa nyeusi tii, zikiwa zimesokotwa vizuri; zilikuwa nazo zinang'ara kama zilizomwagiwa mafuta.

La pili ilikuwa ni kimo chake. Mtu yule alikuwa ni mrefu kuliko wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani. Kwake nilisimama kama vile mtoto anavyosimama mbele ya baba yake na kumuangalia kwa juu kama kwa mbali. Ndivyo nilivyokuwa nimesimama mbele yake. Upana wa mabega yake hadii mikono upande huu na upande huu ulikuwa ni karibu upana wa doti nzima ya kanga. Rangi yake ya ngozi ilikuwa pia ni rangi ya viganja vyake.

Alikuwa amevaa vazi la rangi nyeupe inayong'ara likiwa limefanana kimshono na yale mavazi wanayovaa Wanigeria. Lilimkaa vizuri utadhani lilishonewa mwilini mwake moja kwa moja. Alichokosa ni kikofia cha kufanana nalo tu. Miguu yake alikuwa peku peku.

Kitu cha tatu kilichonigusa ni macho yake. Alivyoniangalia macho yake yalijaa ufahamu. Ninaposema ufahamu nina maana ni kama mama anavyomuangalia mtoto wake na mtoto akauelewa ule mtazamo wa mama yake kwani hata kama alitaka kusema uongo anajikuta anasema kweli. Yalikuwa macho yaliyojaa upole, kujali, na usikivu.

Yalikuwa ni macho yenye kupenya hadi siri za ndani ya moyo lakini vile vile yalikuwa yananipa ujumbe wa mtu ambaye ananifahamu undani wangu kwa muda mrefu. Nilijua kitu kimoja, sikuwa na uwezo wa kumficha kitu chochote kuhusu mimi au kuhusu kitu chochote ambacho kinahusiana na mimi. Kwa ufupi, macho yale yalikuwa yanaonesha kunifahamu undani wangu, wa nafsi na moyo wangu.

Wakati namalizia kupeleka taarifa za mtu huyo kwenye chembe za ubongo wangu kwa mwendo kasi kuliko kompyuta nilijikuta nimepata ufahamu wa ghafla.

Nilijua kuwa nimesimama mbele ya kiumbe toka mbinguni, utulivu wa moyo ulioniingia uliniambia kuwa niko mbele ya kiumbe cha kimbingu japo sikujua ni kiumbe gani maana kama angekuwa malaika basi nilidhania angekuwa na mabawa halafu Mzungu!

Nilijikuta nimeingiwa na hofu na kuamua kuanguka kifudi fudi mbele zake kwani muda wote huo wa kujaribu kumuelewa nilikuwa namshangaa shangaa tu. Kabla sijagusa paji la uso wangu kwenye udongo kama kumsujudia alinishika mabega yangu kuniinua.

"Usinisijudie mimi, Msujudie yule Mmoja aketiye juu ya Kiti cha Enzi" aliniamrisha. Niliinuka huku miguu yangu ikitetemeka kama miche ya mpunga ikipigwa na upepo. Nilivuta pumzi na kusimama mbele yake kama askari wa ngazi ya chini mbele ya kamanda wake. Alinishika bega la kulia na kuniangalia machoni na kuniambia.

"Kuna vitu nimetumwa kukuonyesha na kukuonya" alisema kwa sauti ile ile ya ajabu na kwa maneno ya upole sana.
"Kwanini mimi?" nilimuliiza. Swali hilo lilikuwa limenikaa kichwani tangu wakati ule aliponiamsha na kunifanya nishtuke nikiwa mbele ya habari.

Wakati wote huo niliweza kusikia mlio wa mawimbi nyuma yangu, huku upepo ukipunga kwa mbali. Kwenye ufukwe wa bahari tulikuwa ni mimi na yeye tu. Hilo lilinishangaza kwani nilitarajia kuona watu wengi ufukweni pale.

"Kwa sababu umelia sana!" alinijibu.

"Kwani niko peke yangu niliyelia?" nilimjibu na mara moja nikagundua sauti yangu ilibeba kebehi ya aina fulani.
"Wengi wanalia, wenye kulilia taifa lako, lakini wewe umependelewa" alisema. Kwa kweli sikuelewa.
"Hivi huyo aliyenipendelea ananijua mimi kweli?" nilimuuliza na sauti yangu ikiwa na mkazo kidogo maana nilijua wazi kabisa kama watu wa kupendelewa mimi sikustahili hata chembe. Nilikuwa na orodha ya watu wasiopungua kumi ambao ningeweza kuwapendekeza.
"Mwanakijiji, unajulikana kuanzia kabla ya kuumbwa kwako; ulizaliwa x, ukiwa na miezi x, na baada ya kuzaliwa ulipata matatizo haya 1,2,3."

Alipoanza kusema hivyo nilijikuta nanyong'onyea ghafla. Alianza kunisimulia historia ya maisha yangu kuanzia utoto. Alinitajia marafiki na maadui wa utotoni. Alinikumbusha yule msichana wa kwanza kumpenda kwa urafiki wa ajabu nikiwa shule ya msingi ambaye aligongwa na gari na kufa katika tukio ambalo liliacha jeraha moyoni mwangu hadi utu uzima huu.

Alinisimulia mambo ambayo nilitaka kuyafanya na yale niliyoyafanya. Nilijisikia aibu na wakati mwingine kicheko kwani alinikumbusha vitu vya kuchekesha.

"Basi inatosha!" nilimbembeleza alipoanza kugusa maisha yangu binafsi. Nilijua nikimuachia ataniumbua. Hakuacha.
"Kwa kujiingiza katika masuala ya siasa umejijengea marafiki wengi lakini umejipatia maadui wa kudumu," alisema.

Na kutoka hapo akaanza kunitajia marafiki zangu mbalimbali na kuanza kunitajia pia maadui zangu, kwa majina na vyeo vyao katika serikali, wizara ya mambo ya nje, bungeni, Uingereza, na sehemu nyingine.

Aliniambia mambo ambayo ni mbinguni tu wangeweza kuyajua. Nilitetemeka, na kutetemeka tena, baada ya kutetemeka. Nilijua ujanja tena sina.

"Lakini unanijua hivyo bado hujaniambia wewe ni nani!" nilimuuliza tena.

"Twende tutembee," aliniambia na sote wawili tukaanza kutembea mchangani kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi. Tulitembea kwa mwendo wa taratibu huku harufu ya maji ya chumvi na upepo mwanana ulikuwa kama wimbo wa kutusindikiza.

Alianza kunielezea. "Mimi naitwa Sifaeli, ni malaika mlinzi wa Tanzania" alisema. Katika kujisomea kwangu kote maandiko na vitabu mbalimbali sijawahi kusikia kuna malaika wa Tanzania. Lakini sikutaka kumletea ubishi maana nilipobisha hapo nyuma alinipa historia nzima ya maisha yangu.

"Mwanakijiji, kila binadamu ana mlinzi wake wa kimbingu; tangu unapozaliwa hadi unapokufa hulindwa," alianza kunielezea. "Vile vile kila jamii ya binadamu inao mlinzi wake na kila taifa juu ya uso wa nchi linaye mlinzi wake.

Walinzi hawa huja kulinda jamii ya watu ili kuhakikisha kuwa jamii hiyo haipotei yote. Huongoza wakatii wa shida, huwatetea wakati wa uovu na wakati wa giza la taifa au jamii hiyo walinzi hao husimama kama faraja kuwasaidia kuwainua," alisema na kuweka kituo.

"Ina maana hata Kenya wana malaika mlinzi?" nilimuuliza.
"Naam"
"Uganda"
"Naam"
"Zanzibar"
"Naam"
"Kwanini Zanzibar wawe na malaika mlinzi?"
"Kwa sababu nao ni jamii ya watu; ni taifa, hatuangalii tu mipaka ya nchi, lakini mipaka ya jamii ya watu, ndio maana hata Wapalestina wana malaika mlinzi".

Kutoka hapo akaanza kunielezea jinsi gani malaika walinzi ndio wamehakikisha karibu jamii zote za watu zimeendelea kuwepo licha ya matishio mbalimbali ya kuziangamiza. Wayahudi walilindwa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia dhidi ya jaribio la Hitler kuwaangamiza; aliniambia jinsi Waislamu wa Bosnia walivyolindwa chini ya jaribio la Milosevic kuwaangamiza; jinsi gani Watusi wa Rwanda walivyolindwa taifa zima lisiangamie.

Alinikumbusha pia hata Zanzibar mapinduzi ya Zanzibar hayakuangamiza jamii ya Waarabu wote au familia nzima ya kisultani.
"Kama walinzi ni jukumu letu kuwazuia wanadamu kuangamizana kabisa" alisema. Nilibakia na maswali mengi ya kifilosofia kama kwanini wasingezuia watu wasijaribu hata kuangamizana kabla hawajaangamizana na ni kwanini wanadamu huwa wanafikiria wana uwezo wa kuangamiza kabisa kundi jingine wakati ushahidi wote unaonesha kuwa hakuna watu walioweza kuwamaliza watu wengine kabisa? Siyo Warumi na vita vyao wala siyo Wazungu na uvamizi wao wa Afrika. Niliyabania mawazo yangu moyoni mwangu.

Sifaeli alisimama na kunigeukia.

"Mwanakijiji kuna mtu ambaye unatakiwa uonane naye umuulize maswali mengi kuhusu nchi yako naye atakupa majibu mengi, lakini kuna vitu vingine ambavyo mimi tu nimepewa jukumu la kukuonyesha na kukufanulia ili uweze kuandika kwa upana zaidi matatizo ya nchi yako na uchaguzi mkubwa ambao taifa na watu wako itawapasa kuchukua muda si mrefu ujao," aliniambia.

"Nani huyo ninayetakiwa kumuona mwenye majibu ya maswali yangu" Nilimuuliza kwa unyenyekevu mkubwa.
"Utamjua utakapomuona," aliniambia. "Lakini kwanza twende nikuoneshe kitu ambacho umekuwa ukikiwaza kwa muda na kukiandika kwa mbali lakini sidhani kama umeweza kukiona vizuri kwa kukisia," aliniambia.

Tulikuwa tumesimama mbele yetu kuna mwamba mkubwa ambao umejitokeza na kugusana na maji. Mawimbi ya bahari yalikuwa wanajibimamiza kwenye mwamba ule kama yaliyokuwa yakijaribu kuusogeza nyuma taratibu bila mafanikio. Mwamba ulikuwa uko imara usiosogea wala kutikisika. Sijui hata kama ulijua kuna maji. Alinielekeza upande wa kulia wa bahari. Akaniambia "twende"!

Nikaanza kumfuata kuelekea majini. Tulikuwa bado kwenye mchanga mara Sifaeli alisimama ghafla; nami nilimfuata kama behewa nyuma ya kichwa cha treni. Sikujua huyo mtu mwingine alitokea wapi, na alifikaje mbele yetu lakini kufumba na kufumbua mbele yetu alikuwa amesimama mtu mwingine ambaye kimo chake kilikuwa karibu sawa na Sifaeli, japo yeye mfupi kidogo.

Hakuwa wa rangi ya kijivu bali nyeupe hafifu inayokaribiana na rangi ya maziwa. Mkono wake wa kulia alikuwa amenyanyua upanga mrefu wenye makali kuwili, ulikuwa unang'ara kama uliopakwa mafuta. Mlio wa mawimbi ya bahari na kuvuma kwa upepo kulikoma. Nadhani kulikoma au ni mimi sikuweza kusikia milio hiyo tena.

"Unampeleka wapi huyo!?" Alihoji kwa sauti kali, ya juu sana na yenye mikwaruzo. Ilikuwa ni sauti kama ya mtu anayekwaruza debe bovu. Lakini ilikuwa pia kama imechanganyika na mtu anayekwangua chupa. Kama sauti ya Sifaeli ilikuwa ni nzuri, sauti ya hilo dude (nikimuita mtu nitampa sifa) ilikuwa ni kinyume cha kila kitu kinachoitwa kizuri.

Macho yake yalikuwa ya moto. Hapana sijasema yenye joto bali ndani ya macho wake moto ulikuwa unawaka. Yalikuwa yanawaka moto, fikiria unavyoweza kuchukua chupa, halafu washa mshumaa, na weka ile chupa angavu mbele ya mshumaa utaona moto unavyoonekana ndivyo macho ya yule kiumbe yalivyoonekana. Kama hakuwa shetani mwenyewe basi alikuwa ni ukoo mmoja naye kama si mjukuu wake.

"Nampeleka alikoamriwa kwenda" alisema Sifaeli kwa sauti yake bila kupaza sana wala bila kuonesha woga. Alikuwa amesimama mkono wake wa kushoto ukiwa umeushika mkono wangu wa kulia. Nilijihisi amani na utulivu japo kwa macho yangu nilikuwa naona hofu.

"Hatoenda, hataruhusiwa, na akomeshwe!" alisema kiumbe yule. Kabla sijajua kilichoendelea alipiga ukelele "kwa Lusifaaaa!!" alinyosha upanga wake na kwenda kwa kasi ya ajabu kutuelekea, upanga wake ukiwa umeelekezwa kwenye utosi wa kichwa changu. Nilijua cha moto nitakiona. Nilifumba macho yangu kukubali hatima yangu, nilijua ndoto yangu basi itakatika hapo niamke nigundue kuwa nilikuwa naota tu!

Chaaa!! Mlio wa upanga ukasikika juu tu ya kichwa changu; sikuwa nimeguswa hata unywele wangu mmoja. Nilifumbua jicho moja la kushoto kwa woga. Sifaeli alikuwa amenyosha na yeye upanga wake kunikinga kichwa changu.

Upanga wa kiumbe yule mwingine ulipokuwa unakaribia kutua ulijikuta unapiga kwa nguvu upanga wa Sifaeli na kusababisha cheche za moto ambazo harufu yake iliingia kwenye pua zangu na kunifanya niamini kabisa kuwa ile haikuwa ndoto.
"Rudi nyuma Mharibifu" alisema kwa mkazo Sifaeli huku akinyanyua upanga wake na kwa kufanya hivyo kumlazimisha Mharibifu kuvuta tena upanga wake.

Macho ya Mharibifu yalizidi kuwa mekundu na hasira yake ilikuwa wazi. Fikiria macho ya mlevi, mwenye hasira, halafu mwenye uchungu na kisasi. Mboni ya macho yake ilikuwa inacheza cheza upande upande kwa kasi ya ajabu, sijui alikuwa anaweza kuona vipi.

"Huyu haendi kokote leo, mrudishe anakotoka!" Mharibifu alipiga kelele na safari hii alijivuta nyuma kidogo na kunyosha mkono wake wenye upanga upande wa kushoto kwangu.

Badala ya kushusha upanga kutoka juu kulenga utosi, aliuzungusha kama anayefyeka kuelekea shingo yangu. Sifaeli alikuwa upande wangu wa kulia na hakukuwa na jinsi kwa kadiri nilivyoona ya kuweza kukwepa upanga ule wa Mharibifu.

Kwa mara nyingine nilifumba macho yangu nikisubiri kichwa kidondoke kutoka kwenye shingo yangu. Nilisali sala yangu ya mwisho.

Nilisikia kitu kama upepo umepiga kwa kasi na nilipofumbua macho yangu, Sifaeli alikuwa amezunguka hewani, akiruka kwa kasi miguu ikiwa juu kichwa chake kikiwa sana na kichwa changu akizungukia upande wa pili, upanga wake ukiwa umelengwa usawa wa wima wangu na sekunde hiyo hiyo nikasikia tena ‘chaaa!' upanga wa Mharibifu ukagota tena kwenye upanga wa Sifaeli na cheche nyingine zikaruka. Nikajisema moyoni, yamekuwa makubwa sasa.

Sifaeli alipotua tu upande wangu wa kushoto mkono wake wa kushoto nao ulikuwa umeshika upanga mwingine, msiniulize hizo penge zilikuwa zinatokea wapi kwani mimi nilizishtukia mkononi mwake, hakuwa na ala pembeni ya kiuno chake kwa kadiri ninavyokumbuka.

"Mharibifu, kwa mamlaka ya Kiti cha Enzi, rudi!!!" kwa mara ya kwanza nilimsikia Sifaeli akipaza sauti yake. Kama kungekuwa na barafu ingeyeyuka kwa ukali wake na uthabiti wake. Ilikuwa ni sauti iliyosababisha kila kitu kisimame kwa sekunde chache, kila kitu kilionekana kuganda kwa sekunde kama watoto wanavyochezeana ule mchezo wa kuitana majina na kuambiana "ganda, ganduka".

Vitu vyote viliganda! Mharibifu ni kama alikutwa hakujiandaa na kabla hajapepesa kope zake, Sifaeli alizielekeza panga zake zote mbili ambazo niliweza kuona kwenye ncha zake zinawaka moto, kwenye kifua cha Mharibifu na kama kisu kinavyoingia kwenye sabuni ndivyo zilivyojichomoka, lakini mara moja Mharibifu alipiga kelele na kurudi nyuma. Alichelewa. Alinyanyua upanga wake juu na kupiga kelele, "Sifaeli nitarudi!!" na akatoweka pale pale!

Nilianguka chini nikiwa nimeishiwa nguvu, nilianza kutetemeka kwa woga kwani sikujua hii safari ilikuwa na maana gani.
Sikutaka kuendelea nilichotaka ni kuamka kutoka katika ndoto hiyo ambayo kwa kadiri ilivyoendelea ndivyo ilivyozidi kunitisha na kunifanya nitamani niamke kando ya Mto Detroit. Haikuisha na sala yangu ya kuamshwa njozini haikusikilizwa. Nilikaa chini nimekunja miguu yangu na kuivuita kifuani huku kichwa changu nimekiweka kati ya magoti yangu nalia.

"Hakuna muda wa kulia mwanakijiji, Mharibifu atarudi tena, twende!" alisema Sifaeli na kwa mkono wake mmoja aliniinua nikawa wima bila hata kutafuta kibali.

"Tunaenda wapi sasa"
"Kumuona yule mtu ambaye atajibu maswali yako"
"Wapi?"
"Nifuate mbona maswali mengi hivyo!?"
"Nimezoea kuuliza maswali"
"Maswali mengine hayana muda"
"Kama hayana muda na mimi siendi!".
"Unajua una kiburi sana, sikukuambia hilo hapo nyuma"
"Hapana sina"
"Halafu mbishi"
"Hapana"
"Twende tunachelewa"
"Siendi hadi uniambie tunaenda wapi!"

Kweli kabisa nilijua nina matatizo. Nimezoea kuwabishia watawala na watu wengine lakini sikutarajia ubishi wangu hadi kwenye mambo mazito kama hayo. Sijui ni kitu gani kilinifanya nimbishie maana jamaa alikuwa na panga mbili angeweza kuniwekea mmoja shingoni ningemfuata kokote ambako angetaka kwenda tena huku namuimbia nyimbo za sifa.

Aliniangalia machoni. Alinyosha mkono wake na kunigusa kwenye paji langu la uso kwa kiganja chake tena. "Fetala feta, zimula zemo," alisema. Sijui nini kilitokea, sijui tuliondoka vipi, tulisafiri wapi, na kwa namna gani. Ninachojua tuliondoka pale ufukweni kwa namna na kasi ambayo ni mbinguni peke yake wanajua.

Nilipofumbua macho, tulikuwa nje ya jumba kubwa, kulikuwa na geti kubwa na nje yake kulikuwa na kibanda cha polisi walinzi. Walikuwepo walinzi sita. Hakuna aliyeonyesha kutuona wala kujali uwepo wetu.

Nililijua jengo lile kwani nilipita pale mara kwa mara, sikuwahi kudhania ningeweza kuingia kwani sikuwa na sababu hata mara moja.

Geti halikufunguliwa lakini tulipita kama hakukuwa na geti, tulipenya moja kwa moja kama hewa tu inapita. Tulijikuta tuko ndani ya jengo hilo kubwa. Moyo ulinidunda. Sikutarajia kufika hapo. Tulitembea taratibu kuelekea mlango wa nyumba hiyo kubwa.

Mlango ulifunguliwa. Nikamuona mtu mwenyewe kama nilivyohisi. Aliponiangalia alitabasamu. Niligundua Sifaeli ametoweka. Nikaangaza kila kona sikumuona. Nikajiambia tena, kasheshe.

"Karibu mwanakijiji."
(Itaendelea wiki ijayo).

Fuatilia Njozi ya Mwanakijiji
 
Kwa heshima kubwa sana, namtambua Mwanakijiji kama Mmoja ya watu makini,
mwenye bidii ya kipekee katika usomaji na utafutaji wa ukweli na zaidi, mwenye machungu
ya kipekee kabisa juu ya usitawi wa Nchi yetu Tanzania.

Kuna ndoto ameota, na inachapishwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima Jumatano,
Ninatambua kwamba Ndoto hiyo itakuwa imebeba ujumbe mkubwa sana na wakipekee
kwa watanzania hasa ukizingatia aina ya mwaswali ambayo inaeonekana Mwanakijiji
amebahatika kupata majibu yake kutoka kwa Marehemu Mwalimu Nyerere.

Mpaka hapo Mwanakijiji atakapoeleza yeye Mwenyewe kama ndoto hiyo ni Hadithi,
ama ni ndoto ya kweli naomba nitoe angalizo kwamba Majibu ya aina yoyote yale
atakayoyatoa hayatakuwa Majibu ya Nyerere sababu, Nyerere alikwisha fariki/kufa
na hana uwezo wa kupata, achiliambali ufahamu bali uhai kwa namna yoyote ile.
Kaburi lake liko Butiama, na bila shaka atakuwa ameisha oza na kuwa mavumbi.

Na kwa sababu hiyo, Haiwezekani ndoto hiyo ikawa ni ya ukweli hata kidogo,
kama Mwanakijiji ameamua kutumia style ya aina hiyo katika kuleta ujumbe wake mzuri by any means,
sina Mamlaka ya kumuambia abadilishe bali yeye Mwenyewe popote alipo, ajinyenyekeze
na Aombe Msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa upotoshaji ambao tayari amekwisha ufanya,
kwamba "The dead, Actually Lives"
 
[h=2]Ndoto ya mwanakijiji sio ya kweli[/h]
Kwa heshima kubwa sana, namtambua Mwanakijiji kama Mmoja ya watu makini,
mwenye bidii ya kipekee katika usomaji na utafutaji wa ukweli na zaidi, mwenye machungu
ya kipekee kabisa juu ya usitawi wa Nchi yetu Tanzania.

Kuna ndoto ameota, na inachapishwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima Jumatano,
Ninatambua kwamba Ndoto hiyo itakuwa imebeba ujumbe mkubwa sana na wakipekee
kwa watanzania hasa ukizingatia aina ya mwaswali ambayo inaeonekana Mwanakijiji
amebahatika kupata majibu yake kutoka kwa Marehemu Mwalimu Nyerere.

Mpaka hapo Mwanakijiji atakapoeleza yeye Mwenyewe kama ndoto hiyo ni Hadithi,
ama ni ndoto ya kweli naomba nitoe angalizo kwamba Majibu ya aina yoyote yale
atakayoyatoa hayatakuwa Majibu ya Nyerere sababu, Nyerere alikwisha fariki/kufa
na hana uwezo wa kupata, achiliambali ufahamu bali uhai kwa namna yoyote ile.
Kaburi lake liko Butiama, na bila shaka atakuwa ameisha oza na kuwa mavumbi.

Na kwa sababu hiyo, Haiwezekani ndoto hiyo ikawa ni ya ukweli hata kidogo,
kama Mwanakijiji ameamua kutumia style ya aina hiyo katika kuleta ujumbe wake mzuri by any means,
sina Mamlaka ya kumuambia abadilishe bali yeye Mwenyewe popote alipo, ajinyenyekeze
na Aombe Msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa upotoshaji ambao tayari amekwisha ufanya,
kwamba "The dead, Actually Lives"

tusiandikie mate na huku wino upo...............
 
Kama 'inachapishwa' basi usianze kumhukumu la hasha labda nawe pia unaota
 
Mmmh!!!!! Wewe unataka kusema nini sasa? Wewe ni mhariri na umeiona au unataka tukueleweje?
Mnajuana nyie! Na taarifa yako kiwete...yaani nusu viungo!
 
Kuna ndoto ameota, na inachapishwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima Jumatano,
Ninatambua kwamba Ndoto hiyo itakuwa imebeba ujumbe mkubwa sana na wakipekee
kwa watanzania hasa ukizingatia aina ya mwaswali ambayo inaeonekana Mwanakijiji
amebahatika kupata majibu yake kutoka kwa Marehemu Mwalimu Nyerere.

Naam

Mpaka hapo Mwanakijiji atakapoeleza yeye Mwenyewe kama ndoto hiyo ni Hadithi,
ama ni ndoto ya kweli naomba nitoe angalizo kwamba Majibu ya aina yoyote yale
atakayoyatoa hayatakuwa Majibu ya Nyerere sababu, Nyerere alikwisha fariki/kufa
na hana uwezo wa kupata, achiliambali ufahamu bali uhai kwa namna yoyote ile.
Kaburi lake liko Butiama, na bila shaka atakuwa ameisha oza na kuwa mavumbi.

Napiga mluziiiii

Na kwa sababu hiyo, Haiwezekani ndoto hiyo ikawa ni ya ukweli hata kidogo,
kama Mwanakijiji ameamua kutumia style ya aina hiyo katika kuleta ujumbe wake mzuri by any means,
sina Mamlaka ya kumuambia abadilishe bali yeye Mwenyewe popote alipo, ajinyenyekeze
na Aombe Msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa upotoshaji ambao tayari amekwisha ufanya,
kwamba "The dead, Actually Lives"

koh koh koh...
 
Hyo ni lugha ya fasihi mkuu,mbona inaeleweka? Though havent read the dream yet

Naomba tuwe serious, nina mdogo wangu nyumbani anaifuatilia ile ndoto,
hivi sasa anaamini asilimia mia kwamba nyerere yupo hai nata kama muharibifu na
wenzake wamemtorosha lakini lazima atarudishwa na sifaeli na kumjibu mwanakijiji.
na anamaanisha
 
Mwanakijiji tunaomba muono wako, jinsi huyu jamaa anavyosafiri na ndoto yako.
 
Wanahaha za kutafuta muujiza wa kumfanya Nyrere kuwa mtakatifu. Wapii ? muujiza wake ulikuwa mmoja tu! Kudhulumu mali za watu huku anacheka.
 
Wanahaha za kutafuta muujiza wa kumfanya Nyrere kuwa mtakatifu. Wapii ? muujiza wake ulikuwa mmoja tu! Kudhulumu mali za watu huku anacheka.

Ukiwa kilaza basi unakuwa na chuki ,mchawi , mdhalimu , mshenzi , roho mbaya nk.Nyerere anauwamiza sana na kutaka kutangazwa mt.Waachie wakatoliki na mambo yao nyie mnaweza kuyafanya hayo muda wenu ukifika .Jadili hoja acheni vioja nyie wapuuzi .Mtu kafa kila siku kejeli angalikuwa dhuluma leo mnaliweza hata kusoma nyie ? Alichukua shule zetu akawapa hadi za kusoma wakati .............................wewe usiniudhi nikasema maneno ya kuwaudhi wengi kumbe uko mpuuzi peke yako .
 
Wanahaha za kutafuta muujiza wa kumfanya Nyrere kuwa mtakatifu. Wapii ? muujiza wake ulikuwa mmoja tu! Kudhulumu mali za watu huku anacheka.

Unamjua JKN au umehadithiwa? Kuna nani wacha Tanzania,Africa unaweza kumlinganisha na Mwl?

Mwacheni Mwl MZALENDO Mtanzania wa damu.....
 
Wanahaha za kutafuta muujiza wa kumfanya Nyrere kuwa mtakatifu. Wapii ? muujiza wake ulikuwa mmoja tu! Kudhulumu mali za watu huku anacheka.
sweetheart, kwa hili naomba nitofautiane na wewe kidogo, yes he made a fwe suffer, like any other national leader, hata bosi wa idara tu huumiza baadhi achilia mbali imam au padre au mchungaji

He preserved our treasure, unfortunately hiki kizazi cha nyoka kimeamua kuuza hadi underwear za baba na mama!!!

BTW, karibu Quito
 
Back
Top Bottom