TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.

Naona wameanzia walipoanzia 2015.
 
ukiona wanakimbili huko maana yake kuna loopholes za kukwepa kodi nakufanya biashara zisizo nyooka,wakibana na huko watakibia tena. ukinyooka TRA HAWANA HATA SHIDA NA WEWE
Ushawahi kufanya biashara na ukanyooka au unàfikiria tu.Tanzania inahitaji Tax Reforms aisee iyo haikwepeki kabisa ingia ndani ya mchezo ndio utajua.Kwenye makaratasi ya SHERIA za kodi utaona ni rahisi sana na utaona wafanyabiashara ni wazembe lakini kwa ground mambo ni tofauti kabisa kodi za Tanzania haziko transparent kabisa na pakujitetea hakuna.
 
ukiona wanakimbili huko maana yake kuna loopholes za kukwepa kodi nakufanya biashara zisizo nyooka,wakibana na huko watakibia tena. ukinyooka TRA HAWANA HATA SHIDA NA WEWE
Kurudi si leo. Halafu kwa nini ukiwa kama mkusanya kodi wa serikali kwa nini ukikose kilichopo kivuje kwa wafanyabiashara kukimbilia nje,huku ukijipa matumaini mfu kwamba watarudi?. Lini watarudi?. Kwa hiyo kwa muda wote unaowasubiria huoni kwamba unakosa?. Na ndio uamue kuwajazia kwa kuwaumiza waliobaki ili kuziba gape la waliokimbilia nje?. Mbona tunanyooka tu vizuri T.R.A. Na tulikuwa tunaenda nao tu vizuri. Ni miaka tu ya hivi karibuni tu ndio wameona wawalazimishe wafanyabiashara walipie zaidi ya biashara zao zilivyo.
 
Wametumwa hao na kinachofanyika kinafahamika vizuri sana. Sasa hivi mabeberu wamegoma kutoa hela kutokana na rekodi mbaya ya utawala bora na demokrasia. Hivyo kinachofanyika ni kupora hela za watu kinguvu. Rejea uporaji wa hela za Bureau de change.
comred Lisu alishatutahadharisha kwamba wafanya biashara kwa sasa wananyanganywa pesa zao benki kupitia kitu kinaitwa agency notes hatukumwelewa sasa tupambane na hali zetu kwa mi 5 tena
 
Walimfanyia hivyo SAPNA electronic akafunga biashara na kuuza eneo kwa MTU akajiendea marekani
 
View attachment 1650432View attachment 1650433

Mpaka sasa kashapoteza uhalali wa malalamiko yake. Kweli waafrika wabinafsi sana. Ili ujue maumivu ya wengine mpaka yakupate wewe
Una matatizo ya kimsingi, na pengine hata uwezo wa kudadavua kwako ni duni kiasi.
Kwamba nashabikia chama tawala haina maana kubariki madudu ya watendaji.
Na unajaribu kuingiza siasa uchwara mahali pa kutumia akili ya kiutendaji.
Kama umesoma Mzumbe tukupe pole tu.
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
Nakumbuka haya Mambo yalimkuta. Kaka yangu. Yalitafutwa makosa ya kiuhasibu ya miaka 5 iliyopita, ilipaswa kulipa 150m, kwenda kule TRA, kurekebisha walihitaji 20m.

Kama hujawajua TRA unaweza dhani wanapakaziwa, ni watu hatari Sana Aisee. Unafunga duka huku unaona
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
TRA watausoma watatafuta namna ya kupenyeza kodi
 
Hata mimi pia nategemea kufunga biashara yangu mwezi huu wa 12 kutokana na mazingira magumu ya biashara, ikiwemo kodi isiyolipika, mazingira ya rushwa toka kwa baadhi ya watendaji wa serikali hasa maafisa Afya.
 
Asante kwa kuleta mfano hai mkuu.
Kuna watu wanafikiri tunaleta majungu kumbe mifano hata mikoani ipo.
Ukiona mtu kajitoa fahamu kuwatetea TRA kufunga Account kufunga biashara ujue moja kwa moja ni mnufaika wa uonevu wa TRA au ni Ofisa wa TRA kinara wa huo uonevu wa kuwabambikia kodi wafanyabiashara
 
Na kwa kweli wengi wao misheni kubwa ni kuona wote tunakuwa maskini. Nina shaka sana kama hiyo ndio kazi waliyopewa.
Haya maandishi yetu hayaendi bure. Wakae mkao wa kula. Ilani ya CCM imeeleza wazi umuhimu wa private sector. Wao wanaivuruga kwa manufaa ya nani?
Wanaivuruga kwa manufaa yao binafsi ( Rushwa)
 
TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)

Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".

Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.

Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).

TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi

Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato

Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.

Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.

Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.

Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.

ITAENDELEA..
Ndio elimu hii , na mnakubali kabisa kufundishwa huu ujinga

1. Kama mfanyabiashara sii mlipa kodi, kwann watu wa kodi wanamfuata, kwann wasimfute mhusika moja kwa moja?

2. Kama yeye si mlipa kodi, kwann kodi hizo zinaondoka hadi na mtaji wake na kuua biashara na kumwacha na madeni?

3. Kama yeye sii mlipa kodi hiyo, kwann hiyo pesa ikiondoka anai feel kwenye mzunguko wake wa pesa kwamba kuna kitu kimepungua??

Acheni kujificha kwenye vichaka vya ajabu ajabu, wekeni mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi, kateni kodi za halali sehem halali
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
WAO HAWAWEZI KUSHITAKIWA KWA KUWAMBIKIZA/KUGUSHI? IFIKE MAHALI TUWE WAWAZI NA WAKWELI! TRA NI MUMIANI.
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
WATAANZISHA MPANGO WA "KUWATAMBUA NA KURASIMISHA" BIASHARA ZISIZO RASMI. KILA MMOJA ATAONJA KIKOMBE HICHO!
 
Mimi walinibambikia kodi ya milioni 70. Niliwawekea mahesabu yote, lakini yupe ofisa akadai anaomba nilipe milioni 30 bila kama sitalipa kabisa, naweza kuzunguka mwaka mzima bila kupata tax clearance. Nililipa milioni 30, sasa nashughulikia kufunga kampuni. Nayo ni process. Miezi 6 imepita tangu nianze.

Kufanya biashara/kuwekeza sasa hivi hivi Tanzania ni kijitafutia stress. Kawekeze nchi nyingine, hapa ni mahali pa kulala tu.
 
Back
Top Bottom