Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,563
- 28,524
- Thread starter
- #241
Mkuu pale Bungeni ni wabunge siyo misukule kama unavyosema.Hawa jamaa kuanzia kamishina ni ndumi la kuwili sana. Wanapoongea katika vyombo vya habari juu ya taasisi hii na majukumu yake utasema hawa wafanyabiashara ni wakorofi sana na sio waelewa. Ila ukipewa rekodi ya madudu yao wanayofanya ndipo unajua kuwa haujui......
Tazama tu hata makadirio ya kodi ya bidhaa zinazopita bandarini. Yaani magharama yapo juu kweli kweli kuliko hata bei ya bidhaa. Unanunua gari Us dola 2,500, kodi inakuja milioni saba..... Sasa unajiuliza imekuwaje kodi ni zaidi ya 100% ya original price ya bidhaa?!
Tunahitaji kiwakazia wale misukule pale bungeni kujadili upya hizi kanuni za TRA.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na Wabunge wana kazi kubwa ya kubadili sheria ya Kodi ili indane na uhalisia.
Sasa ndio wakati wa wabunge wa chama tawala kuonyesha kuwa wanaweza kwenda sambamba na serikali ili kubaoresha sekta ya biashara ambayo sasa hivi inadidimia kutokana na kodi zisizoelewela.
Nimefurahia msimamo wa Rais Hussein Mwinyi katika hili.
Yeye amesema wazi hapendelei kodi za kuumiza mfanya biashara , bali kodi ndogo ili zilipike kirahisi na kwa wingi.