TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Wewe hujui unalosema,nyie ndio amabo hamjui kitu kwa sababu hujawahi fanya biashara na kulipa kodi.na hujui mchango wa biashara za kati kwenye mchango wa pato la serikali. Yaani serikali zinazoendelea dunia ninkwa kuwa na mfumo mzuri wa kodi.serikali haitakiwi kuingia kufanya biashara,inatakiwa kuwezesha watu wafanye biashara ili walipe kodi.

Ni hivi mtu ulifanyiwa tax assesment miaka mingi iliyopita na hao hao maafisa tra na kulipa chao baadaye wanakuja hawa tena wanafanya upya na kusema uli underfile,so unakokotolewa kodi nyingine na ile tofauti unapigwa fine na interest.kwa nini wasianze na hao maofisa wa nyuma waliosema kila kitu kiko cleani. yaani hapa kwa nini warudi miaka ya nyuma ambayo tayari walishaicheki wenyewe. Hii nadhani inawezekana kwa some instances siyo kila assesment.yaani wanaweza pia baadaye wakarudi pia na kusema kiasi hicho kipya nacho kilikuwa wrong.

Tunazungumzia "unpridictabe enveronment" watu wanakuwa waoga kuendelea na biashara kwa sababu TRA wenyewe kwa wenyewe kila ofisa na tafsiri kivyake sheria ya kodi.

Labda tushauri yafuatayo.

1.Kuwe na TIC,kituo cha uwekezaji kwa wafanyabiashara wadowadogo wenye mitaji midogo na ya kati,mathlani mtu anataka kufungua hardware,duka la jumla,phamacy,biashara ya usafirishaji,gereji,shule,Hotel,bar,guesthouse,lodge,uchimbaji wa madini n.k kuwe kuna kitengo mahali flani serikalini (kila wilaya) cha kwenda kuomba ushauri na kusaidiwa kukamilisha vitu mhimu na kupewa elimu muhimu ya maswala ya kodi na vibali mbalimbali na kufafanuliwa kwa sheria mbali mbali kulingana na sekta ambayo biashara husika iko

2.Lile dawati la ushauri la TRA lingekuwa linafikika na wafanyabiashara wa kawaida

3.Kuwe kuna kitengo kingine cha kuhakiki ukokotoaji kodi kabla mtu hajapewa bili yake ya kodi

3.Kuwe na idara huru(Obusman).Ili wafanyabiashara wenye malalamiko wawe wanaenda kupeleka malalamiko ya unfair tax assesment.kiwe huru na kiwezeshwe kufanya kazi.na kiwe nje ya wizara ya fedha.(kiwe kina dhibiti ubabe wa TRA).yale mabalaza (tribunal) yalishashashindwa kazi zamani

4.TRA wawe na kitengo cha kumentor biashara ndogo ili ziweze kukua.Kila oficer anayekusanya kodi,biashara anayokusanya kodi ikifa naye kazi iishe.Ila ikiweza kukua na kuongeza mapato aweze kupata promotion.kwa mfano wakati wana asses performance ya mkoa wa kikodi waangalie pia idadi ya wafanyabiashara wapya waliojisajiri.ikitokea waliojisajiri ni wengi kulikowalifunga biashara basi wapewe bonas.ila biashara zilizofungwa zikiwa nyingi kuliko mpya then wapunguziwe points za performance. so in short inatakiwa biashara zikifungwa kuwe na direct negative impact kwa TRA region ofice.yaani wafike mahali wahusike kulinda biashara kufa.so zile fine na riba wanazokokotoa wazire-flect juu ya uhai wa biashara husika

Sasa hivi TRA wanaonekana miungu watu,na kituo cha uwekezaji (TIC) wanaonekana wajinga tuu.kumbe ndiyo kitengo mhimu na kilipaswa pengine kiwe ndani ya Wizara ya fedha na mipango.Chini ya waziri mmoja.aulizwe biashara kufungwa na upande wa pili aulizwe juu ya mapato toka kwa hizo biashara
Nimeipenda point namba 4. 👍👍👍
 
Haya yote lisu alikuwa anapigia kelele kwa kujiamini kabisa sababu alishakuwa anapata taarifa sahihi tra wanaagizwa na magufuli kubambikia wafanyabiashara kodi kubwa hasa wale ambao hawaichangii ccm
Sasa jambo hili lakukamata akaunti za bank ndio baya zaidi
 
Hawa jamaa mimi nawaogopa sana. Hata kufungua bank account naogopa. Cjui pesa zangu zikiwa nyingi ntaziweka wapi.
Unaagiza gunia la mchele kutoka majuu..unalilipia kodi. Baada ya kuliuza..unawakatia chao tena. Yaani wanakula mara nyingi kwa kitu kimoja hawa jamaa.
 
Mimi walinibambikia kodi ya milioni 70. Niliwawekea mahesabu yote, lakini yupe ofisa akadai anaomba nilipe milioni 30 bila kama sitalipa kabisa, naweza kuzunguka mwaka mzima bila kupata tax clearance. Nililipa milioni 30, sasa nashughulikia kufunga kampuni. Nayo ni process. Miezi 6 imepita tangu nianze.

Kufanya biashara/kuwekeza sasa hivi hivi Tanzania ni kijitafutia stress. Kawekeze nchi nyingine, hapa ni mahali pa kulala tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni tax Consultants, nieleze tatizo ni nini nikusaidie
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.
Wewe ni miongoni mwa makasuku wa ccm hapa jf , tulikuonya kwamba shetani hana rafiki ukapuuza , sasa zamu yako imefika unamlilia nani ?
 
Mkuu tupe ushauri mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)

Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".

Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.

Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).

TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi

Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato

Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.

Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.

Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.

Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.

ITAENDELEA..
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.
KWAHIYO?
 
Leo Kuna jirani yangu ana biashara yake maskini wanasema slope 18 MILIONI sijui kivipi au afungee mgahawa
 
Daylight robbery by Zanzimana from kijani kibichi green party .
 
Ili swala ni shida Tanzania, ukienda kwenye sheria zetu taxable person ni biashara zenye turnover ya tsh 100+ million ndio lazima kujiunga na mfumo wa kulipa VAT na TRA. Surely such organisation have full time accountants vinginevyo nikijitafutia matatizo.

Ina maana wafanyabiashara wadogo ambao mauzo ya bidhaa zao yapo chini ya millioni 100 kujiunga ni swala la voluntary, sasa kwanini tunaona kwenye channel yao ya tube TRA wanaangaika na hawa watu.

Isitoshe ata wasipojiunga serikali aitakiwi kupoteza mapato ya VAT kwa sababu wafanyabiashara wadogo wanakuwa final consumers na wao awatakiwi ku charge tena. Labda kama kukimbizana nao iwe kwenye kodi ya faida (profit tax na P.A.Y.E) which are much more complicated to compute for non accountants.

Ata pale watu wanapoamua ku register voluntary ili wawe kwenye system (be it wengi wanalazimishwa ukiangalia video za TRA) awafundishwi namna ya ulipaji mfumo ni upi cash accounting au accrual accounting.

Kumbukumbu zipi unatakiwa kutunza na kwa muda gani, kuna swala la wafanyabiashara wadogo kuelewa VAT wanazotakiwa kutoza kutokana rate zake ambazo na zenyewe mara kwa mara huwa kuna mabadiliko fulani yanatokea kwenye budget ya kila mwaka.

Ni hivi kama wewe ni mfanyabiashara mdogo na umesajiliwa as taxable person (voluntary) you are better off using an EFD machine to help you calculate your output taxes and keep your receipts to claim the input taxes.

The long term solution ni wakati sasa wa Tanzania kuwa na tax services za kusaidia hizi biashara I do not see why qualified ACCA accounts don’t seize this opportunity which is presenting itself.

Binafsi nikiangalia zile video na maelezo ya maafisa wa TRA huwa najisemea these businesses are at the mercy of officers who visit them, the knowledge gap is just too wide.
Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawapendi professionalism, wengi wanaweza ajiri accountant au kumlipa pale anapokuja kumuwekea hesabu sawa Ila wengi hawawataki mwishowe wanaishia kulalamika
 
TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)

Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".

Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.

Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).

TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi

Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato

Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.

Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.

Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.

Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.

ITAENDELEA..
Mkuu ukiendelea unitag
 
Huo ndiyo ujinga wao wanaua biashara matokeo yake wanakosa kodi endelevu za mda mrefu

wamejaa wasomi bandia, wasiojua au kujari hata hesabu ndogo tu zinavyokwenda. Na kwa kweli sijui hizo ajira milion nane zitatoka wapi kama ilivyoelezwa kwenye ilani ya CCM ya uchaguzi, kama TRA itaendelea hivi.
Mitaji inakufa, biashara zinafungwa. Wao wanachojari ni rushwa tu. Wamejaa wala rushwa TRA
 
Kuna jamaa alipelekewa tax liability ya 70m.. akahoji ikabaki kama 2.7m ndo anapambana nao ailipe.
Aiseee jamaa wanapiga spana.
 
I wish Magufuli asome hii thread ,sio kusikiliza majungu ya kina msukuma sijui DED kununua Gari la million 400
Mh rais anakazi kubwa ya kufanya tax reforms ili kikuza biashara ndogo,suala la vitambulisho la wamachinga silikubali Sana,maana ukiendekeza tabaka Fulani lilisilipe Kodi ,unatengeneza kizazi kibaya Sana
 
Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawapendi professionalism, wengi wanaweza ajiri accountant au kumlipa pale anapokuja kumuwekea hesabu sawa Ila wengi hawawataki mwishowe wanaishia kulalamika
Prevention is better than cure, kama VAT tu ambayo inatakiwa kuwa rahisi inawashinda hesabu zake na kuishia kulalamika kubambikiziwa malipo.

Income tax si ndio kasheshe huko naona ndio wanatandikwa mpaka wanatia akili.

Sitoshangaa nikisikia 90% ya wafanyabiashara wakitanzania awaelewi ‘2008 income tax act’.

Hao wachache ambao wanaijua kwa kuangalia mwenendo wa malalamiko sidhani kama wanaweza tengeneza income statement sambamba na sheria kuweza kufanya expense adjustments za ‘allowed and disallowed expenditures’, uelewa wa treatments za depreciation of assets, capital allowances; etc kwa manufaa yao ili kupunguza kodi wanayotakiwa kulipa.

Solution ya haya matatizo ni accounting services na mtaalamu mmoja wa tax kutoa kitabu cha income tax kinachokuwa updated annually baada ya budget kuwasaidia accountants kwenye kufanya hesabu zao. That’s what other people do in the world.

So far kwetu kwenye maswala taxation mwerevu wa sheria ni mmoja tu “TRA” wafanyabiashara wapo at his mercy; balance inahitajika wafanyabiashara lazima na wao watumie wataalamu kuwaandilia hesabu.

Tatizo ninalo liona ‘knowing us Tanzanians’ mijitu itakayotoa hizo services itaanza tamaa kuja na charges za millions na kuwafanya watu waone gharama kwenda. Badala ya kufikiria in terms economic of scale. We ukipata wateja 300 wa kuwafanyia tax kila mmoja ukamcharge laki moja tu kwa mwaka maisha umeyapatia.
 
Back
Top Bottom