TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Tatizo TRA wanafanya kazi kwa hofu.

Bwana yule kawapa targets ambazo hazina uhalisia, na wasipo fikia targets hizo wanaonekana wameshindwa kazi na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kutumbuliwa.

Kwa maana hiyo basi wanalazimika kukusanya kodi kwa mabavu haijalishi hata kama wanawaumiza walipaji, mradi tu waendane na matakwa ya bwana yule.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
I wish Magufuli asome hii thread ,sio kusikiliza majungu ya kina msukuma sijui DED kununua Gari la million 400
Mh rais anakazi kubwa ya kufanya tax reforms ili kikuza biashara ndogo,suala la vitambulisho la wamachinga silikubali Sana,maana ukiendekeza tabaka Fulani lilisilipe Kodi ,unatengeneza kizazi kibaya Sana
Maneno ya busara mkuu.
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Hii ni kweli kabisa,fanya mpango uanzishe huo Uzi maana bila hivyo wengi tutakufa mapema kwa upuuzi wa Jiwe na TRA yake.
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Mkuu, ni zipi hizo?
 
Pole zake nyingi.
Haya ndio yanayoendelea na yamekuwa common nchi nzima kwa kuwabambikia kodi wazalendo kiasi kwamba kuna ambao wanafunga hizi biashara na rushwa wanailamisha sana.

Rafiki yangu wa AR walimwambia kwa miaka kumi anadaiwa 70M akaonyesha mahesabu yake yote yaliyovyokuwa (tax clearance) lakini wapi walibanana nae hadi ikawa 30M hapo wakakomaa alipe. Hadi sasa hajui anazipata wapi!
 
Ukiwa maskini mara nyingi unakua mchawi, shida yke watu wote wawe kama yeye, hizi roho mbya na husda sijui huwa zinamsaidia nn
Easier say than do. Unalipa na nini? Wala sio kulia. TRA iko kwa mujibu wa sheria. Na hawako juu ya sheria. Msijidanganye. Mwenzako akinyolewa, wewe tia maji
 
Ni kweli mkuu.
Tatizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawazijui haki zao kutokana na kutoelewa sheria.
Na wafanyakazi wengi tu TRA hawazijui sheria za kodi.
Watu wa system wakiamua kuna cha sheria...mwendo wa ubabe tuu
 
Wewe ni miongoni mwa makasuku wa ccm hapa jf , tulikuonya kwamba shetani hana rafiki ukapuuza , sasa zamu yako imefika unamlilia nani ?
Screenshot_20201215_073017.jpg
Screenshot_20201215_072816.jpg


Mpaka sasa kashapoteza uhalali wa malalamiko yake. Kweli waafrika wabinafsi sana. Ili ujue maumivu ya wengine mpaka yakupate wewe
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
So mliambiwa muandamane Kura zimeibiwa za lisu mdai haki yenu mkatuona wasenge. Sasa mlinywe mnalialia ili iweje sasa. Mlidhani sisi watoto wa maskini ndo tutaumia tu kwa kukosa ajira. Mana ajira imekuwa issue sasa hivi na zilizopo zinayeyuka kila kukicha..

Jifunze I kudai haki kwa migomo na kuandamana Kama ilivyokenya bila kujali kupigwa mabomu. Otherwise mtabinwa Sana na lisu Yuko zake ughaibuni aliwawatete Sana mkamuona kachanganyikiw
 
Ukiwa maskini mara nyingi unakua mchawi, shida yke watu wote wawe kama yeye, hizi roho mbya na husda sijui huwa zinamsaidia nn

Na kwa kweli wengi wao misheni kubwa ni kuona wote tunakuwa maskini. Nina shaka sana kama hiyo ndio kazi waliyopewa.
Haya maandishi yetu hayaendi bure. Wakae mkao wa kula. Ilani ya CCM imeeleza wazi umuhimu wa private sector. Wao wanaivuruga kwa manufaa ya nani?
 
Haya ndio yanayoendelea na yamekuwa common nchi nzima kwa kuwabambikia kodi wazalendo kiasi kwamba kuna ambao wanafunga hizi biashara na rushwa wanailamisha sana.

Rafiki yangu wa AR walimwambia kwa miaka kumi anadaiwa 70M akaonyesha mahesabu yake yote yaliyovyokuwa (tax clearance) lakini wapi walibanana nae hadi ikawa 30M hapo wakakomaa alipe. Hadi sasa hajui anazipata wapi!
Akalipe, kodi ina sehemu mbili mapato(mauzo ghafi)/matumizi mapato yako msotly TRA wanakuwa nayo. ni wajibu wako kuthibitisha matumizi yako kwa risiti/viambatanisho kinyume cha hapo utaona ni wa kuonewa.
 
Akalipe, kodi ina sehemu mbili mapato(mauzo ghafi)/matumizi mapato yako msotly TRA wanakuwa nayo. ni wajibu wako kuthibitisha matumizi yako kwa risiti/viambatanisho kinyume cha hapo utaona ni wa kuonewa.
Mtabaki wenyewe sasa. Tutaona mtakusanya wapi kodi. Mwenzenu wa Zanzibar kashashtuka baada ya kuchungulia bara kinachoendelea kwa wafanyabiashara na biashara kwa ujumla zinavyofungwa. Kwa sasa nina imani ili kufikia malengo ndio imefikia sasa kuwabambikiza watu kodi kubwa ili kufidia gape ya wale waliofunga,hayo ndio matatizo yake,mzigo mkubwa wameanza kubeba watu wachache. Nina uhakika ikiendelea hivi miaka hata miwili mbele,hakuna biashara itabaki,mtakusanya hela zenu mfukoni
 
T.R.A ni tatizo kubwa kwa sasa ustawi wa nchi. Wafanyabiashara wengi wanakimbilia nje ya nchi. Ukitaka kujionea hili,nenda mpaka wa tunduma. Mamlaka za Zambia baada ya kuona wafanyabiashara wananyanyaswa sana upande wa Tanzania wakakaaa nao wamewatengea eneo upande wa zambia,kwa hiyo wengi wanahamia upande wa zambia kujenga maduka. Soon Tunduma upande wa Tz itakufa kabisaaa. Ona kariakoo inavyotia huruma kwa sasa. Kipindi miaka 6 tu nyuma kariakoo ilikuwa ni kitivo cha biashara kwa nchi za DRC,Malawi,Zambia,Mozambique n.k,kariakoo ndio ilikuwa dubai yao. Baada ya kuona bidhaa ziko juu kariakoo sbb ya T.R.A wafanyabiashara hizo nchi nao wamejiongeza wanaenda nao mbele. Lakini T.R.A wakijisahihisha bado tuna nafasi ya kuzikamata hizo nchi
ukiona wanakimbili huko maana yake kuna loopholes za kukwepa kodi nakufanya biashara zisizo nyooka,wakibana na huko watakibia tena. ukinyooka TRA HAWANA HATA SHIDA NA WEWE
 
Back
Top Bottom