Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,563
- 28,524
- Thread starter
- #221
Mkuu asante kwa ushauri.TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)
Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".
Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.
Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).
TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi
Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato
Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.
Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.
Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.
Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.
ITAENDELEA..
Lakini nafikiri unajua fika kuwa kodi kama With Holding Tax na Provisional Tax huwa ni sehemu tu ya Annual Corprate Tax.
Na unajua madudu ambayo yanafanyika katika hili.
Kodi hizi zinakatwa (hasa WHT) kupita na kuzidi makadirio ya Corporate Tax,
Na ikishakatwa hairudishwi.
Nataka neno lako katika hili.
Halafu kwenye Invoicing.
Wafanyabiashara wengi hawalipwi in time, lakini wanapaswa kuwasilisha VAT at source and in time.
Yaani ukimpelekea Invoice na risiti ya EFD mteja wako(mara nyingi Serikali) unatakiwa ulipe a kodi uliyotakiwa kukusanywa ndani ya mwezi mmoja.
Uzoefu unaonyesha kuwa kuna wafanyabiashara hawalipwi hata ndani ya mwaka hivyo kufilisi kampuni.
Haya mambo ya vitabuni wee yaache tu, uhalisia na TRA ni kitu kingine.