TRA valuation system ya magari haiko fair

TRA valuation system ya magari haiko fair

Uwezekano upo ingawaje ni mdogo sana kwa gari yenye umri zaidi ya miaka 8 kutembea km 30 000 tu! Na isitoshe Volvo V50 iliyotembea km 30 000 tu kuuzwa dola 4 000 hapo hapana, labda kama umepewa zawadi lkn kwa bei ya sokoni siyo kweli!
kama ya mwaka 2005 inauzwa dola 1400 kwanini hiyo isiwe hiyo bei
 
Mkuu calculator yao hakuna sehemu inapokwambia ujaze bei uliyonunulia gari. Hivyo basi moja kwa moja ni kwamba kodi yao haitokani na cif/bei uliyouziwa gari.
Unachojaza ni aina ya mafta, model ya gari, mwaka na cc za gari.
Halafu anayesema gari mpya kodi ndogo anadanganya jaribu kuchukua gari mfano allion ya mwaka 2002 na ya mwaka 2008 utakuta ya mwaka 2008 ina kodi zaidi.
Kiongozi, TRA calculator haina bei ya kununulia lakini kuna CIF(Cost, Insurance and Freight) elekezi, wao wamepiga mahesabu ya gharama za manunuzi, bima na usafiri hadi bandarini.

Tatizo watu wananunua magari bila kupitia CIF elekezi ya TRA. Kama umenunua mf. Runx CIF $2,500 wakati CIF ya TRA ni $,2000, TRA watakulima kodi hadi ulie. The best thing ni kuhakikisha kuwa CIF ya gari yako ni sawa na ya TRA au ndogo zaidi.
 
Kiongozi, TRA calculator haina bei ya kununulia lakini kuna CIF(Cost, Insurance and Freight) elekezi, wao wamepiga mahesabu ya gharama za manunuzi, bima na usafiri hadi bandarini.

Tatizo watu wananunua magari bila kupitia CIF elekezi ya TRA. Kama umenunua mf. Runx CIF $2,500 wakati CIF ya TRA ni $,2000, TRA watakulima kodi hadi ulie. The best thing ni kuhakikisha kuwa CIF ya gari yako ni sawa na ya TRA au ndogo zaidi.
Ndilo nalojaribu kumwambia kuwa hawatumii bei uliyonunua wewe. Naskia wakati wanatumia bei ya mnunuaji watu walikuwa wanachakachua kuonyesha cif iko chini ili kuziba hilo wakaja na cif elekezi.
Hivyo kabla ya kununua gari ni bora mtu ukacheki ushuru kwenye calculator yao na ni user friendly.
Ila hili halifuti ukweli kuwa kodi ya magari Tanzania iko juu sana
 
Pole jamaa yangu. Ushauri ungepitia website ya TRA wanaonyesha bei ya gari kulingana mwaka wa kutengenezwa na siyo bei uliyonunulia. Wanatumia retail selling price ambayo hiyo V50 ni kati ya dola 60,000 mpaka 67,000. Hapo ndiyo kukokotoa kunaanzia hapo na dhamani ya gari yako haitumiki uliyonunulia na itakuwa retail selling price kutoka kwenye list ya TRA na hapo unajikuta unalipa VAT peke yake karibu dola 8000. Kama alivyoshauri jamaa hapo before kuagiza angalia online calculator ya TRA
ipo haja ya kungalia upya huu upigaji hesabu, mfano kichwa cha scania (tractor) kinauzwa uero elfu 3000 spain hadi kukifikisha tanzania kitafuka kwa tshs 10m ushuru tra wanakwambia ulipe 46m hii haiko sawa kabisa.
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !

Soko la magari JP ni soko huria, watu huuza magari yao kupitia hawa ma ajent (kampuni za kuuza magari) na baadhi ya kampuni hununua magari na kuyauza wao. So swala la gari imetembea kilometer ngapi si la kulihusanisha na bei moja kwa moja (100%). Unaweza kupata gari iliotembea km nyingi kwa bei kubwa na pia ukapata la km chache kwa bei ndogo.
 
Magari mazuri tunaendesha katika Ardhi ya South Africa tuu bongo mwendo wa ist na passo na pick up ford bantam gari za zamani 2005,2007 bongo kodi ni hatari inaendana bei na gari hilo hilo la 2016...Sijui nani alitutupia sumu hii magari yaonekane anasa wakati moja ya mahitaji muhimu kwa binadamu...
 
Kwa TRA kukomoa hivyo wanajaribu kutuma ujumbe gani? Tusiagize magari/vitu kutoka nje au ndo mambo ya ‘kumfanya kila Mtanzania haishi kama shetani”?

it would make sense kama humu ndani kuna viwanda vya kuzalisha magari..Kodi kama hizo huwa za ku discourage Imports
 
Hiyo ni gari KUU KUU na hapo unadanganya/umedanganywa haiwezekani gari ya miaka zaidi ya 8 iwe imetembea km 30 000 tu!
Huo ni uongo mweupe hizo km inazimaliza kwa mwaka mmoja tu na isitoshe kama ni kweli imetembea km 30 000 haiwezi ikauzwa
Dola 4 500 hilo haliwezekani, hivyo TRA wetu wako sawa kabisa kwa maana wewe ni muongo/ umedanganywa!

TRA wanashangaza sana.....Kwanza kuweka kodi kubwa kama hii lengo huwa ni ku discourage imports

It would make sense endapo kungekuwa na viwanda humu nchini

Lakini cha ajabu zaidi gari Jipya linapigwa kodi kubwa zaidi kuliko gari la zamani......Angalia mfano wa hiyo KLUGER hapo chini...Model Moja....Ipo ya mwaka 2003 na ya mwaka 2009...Ya mwaka 2009 Ni kodi kubwa zaidi......


upload_2016-8-31_10-2-41.png


upload_2016-8-31_10-3-38.png
 
TRA wanashangaza sana.....Kwanza kuweka kodi kubwa kama hii lengo huwa ni ku discourage imports

It would make sense endapo kungekuwa na viwanda humu nchini

Lakini cha ajabu zaidi gari Jipya linapigwa kodi kubwa zaidi kuliko gari la zamani......Angalia mfano wa hiyo KLUGER hapo chini...Model Moja....Ipo ya mwaka 2003 na ya mwaka 2009...Ya mwaka 2009 Ni kodi kubwa zaidi......


View attachment 390823

View attachment 390824
mkuu, huyo jamaa ni kada na mtetezi wa kila kitu na ataendelea kubisha tu koz hana gari anabebwa na kuruza ya chama,juu huko alisema kodi ya gari inatokana na km ilizotembea,usijichoshe kumuelekeza.
 
TRA wanashangaza sana.....Kwanza kuweka kodi kubwa kama hii lengo huwa ni ku discourage imports

It would make sense endapo kungekuwa na viwanda humu nchini

Lakini cha ajabu zaidi gari Jipya linapigwa kodi kubwa zaidi kuliko gari la zamani......Angalia mfano wa hiyo KLUGER hapo chini...Model Moja....Ipo ya mwaka 2003 na ya mwaka 2009...Ya mwaka 2009 Ni kodi kubwa zaidi......


View attachment 390823

View attachment 390824
hii hatari
 
Barbabosa,

Kama kudanganya basi aliyedanganya ni yule aliyeniuzia. Mimi nimenunua gari online, na hiz ndizo details nilizopatiwa. Na hiyo valuation na kodi husika ilikokotolewa ka kutumia TRA Valaution Calculator. Ninavyozungumza hivi hata Shipping docs za hiyo gari zijazishika mkononi. Vinginevyo ninaweza kukutumia docs za manunuzi hujionee mwenyewe details za gari na manunuzi.

Ahsante kwa kunichallenge though...
Malalamiko yako ni ya msingi sana. Kuna jamaa kama watatu wana thread kama hii ya kwako, wote wanalalamikia kadhia hiyo hiyo (unfair calculation system). Nadhani kuna shida mahali ambayo TRA hawataki kwa makusudi kuifanyia kazi. Haiwezekani gari uingize kwa milioni 9 then ulipe kodi milioni 15.
 
Usiwe mbishi wenzetu gari wanatumia kutokana na toleo sio mpaka gari lizeeke. Gari ndani ya mwaka inatoka toleo jingine kwa hiyo mtu anauza na kuchukua model mpya. Usifikiri kwao gari wanatumia mpaka kiti cha dereva kinakuzoea kama huku kwetu.
Umenena sawa kabisa mkuu. Wenzetu wanakwenda kwa fashion na si vinginevyo. Nawala sio kwenye magari tu bali nikaribia kila kitu. Nilikuwa word cup Brazil 2014 niliona mambo ya ajabu sana kwa wenzetu. Jezi za nchi mbali mbali zenye majina ya stars wao kabla ya mechi utakuta jezi moja ni USD500-1500. Lakini baada ya mechi ikitokea timu husika imefungwa, keshoyake ukiingia duka hilohilo ulilopita Jana utakuta bei imepolomoka mpaka dola50.
 
Kila tukisikia TRA imevuka lengo kwenye makusanyo yake ya mwezi tunashangilia, kumbe huku ndo wanakotubambika!

Ngoja tuisome number.
 
kinachotumika katika kukokotoa kodi ni vitu vifuatavyo:

1. Retail Price ya gari (Ikiwa mpya)

2. Mwaka gani gari limetengenezwa

3. Engine Capacity

Hivyo kwa kutumia Retail price ya gari na mwaka gari limetengenezwa (ili kujua depreciation) wanapata bei elekezi ya wakati gari limeingia nchini.

Hivyo ukiagiza gari bei chini ya bei elekezi (Custom CIF) , TRA huwa wanapandisha hadi ifikie ile bei elekezi.

So, hata ukipewa gari bure japan ushuru upo pale pale.

Na kwa upande wa pili wa shilingi, ukiagiza gari kwa bei ambayo ipo juu ya bei elekezi.. jamaa wanachukua kama ilivyo.. 🙂
yaani kiasi kilicho Kikubwa ndicho kitatumika kwenye kukokotoa.
 
USHAURI:

kabla ujaagiza gari, tembelea kwenye ile calculator yao.. Na pia kwenye mwaka pale jaribu kucheza napo kwa kujaribu miaka tofauti tofauti unaeza ukaokoa million kadhaa

Kwa mfano, Mwaka jana Rav 4 kili time ya mwaka 2001 ilikua ina kodi kama 7.8m na wakati kili time ya mwaka 2000, 2002, 2003 hadi 2005 zilikua kodi juu. (9mil - 10mil)

Harrier new model ya mwaka 2005 kodi ilikua cheap (12mil) kuliko ya mwaka 2003, 2004, 2006... (15mil)

Kama utaweza kupata lile liorodha la "retail price" ya kila gari kwa kila mwaka utajua uagize gari ya mwaka gani for the same car model.
 
Mimi huwa sina mpango wa kuagiza gari nje, huwa navizia humuhumu zinazouzwa na watu binafsi
 
Back
Top Bottom