TRA valuation system ya magari haiko fair

Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
Usiwe mbishi wenzetu gari wanatumia kutokana na toleo sio mpaka gari lizeeke. Gari ndani ya mwaka inatoka toleo jingine kwa hiyo mtu anauza na kuchukua model mpya. Usifikiri kwao gari wanatumia mpaka kiti cha dereva kinakuzoea kama huku kwetu.
 
Sawa Barbosa nimekuelewa.

Ok nimeibiwa. Sasa kwanini Serikali inaniadhibu zaidi?

Kwani kwa TRA kuongeza thamani ya gari ni kunaashiria kuwa gari ni chakavu au lina thamani kubwa? Nimeuziwa gari kwa $4,455 na TRA wamelithaminisha $10,880. Kitu kinachothaminishwa zaidi ya bei/uhalisia kinamaanisha hicho kitu kina hadhi kubwa au ni chakavu? Labda unipe ufafanuzi hapa ili nijifunze.
Msamehe hajui atendalo huyo.
 
Ahsante DN kwa ufafanuzi.

Lakini sasa kwanini TRA wameniadhibu, kwa kitu ambacho sikuwa na control nacho? Mimi nimeliona gari na nikalipenda. Nikauliza bei nikapewa na nikaikubali. Sasa kwanini TRA wamehamua kuniadhibu zaidi kwa kunipiga ushuru ambao hauna uhalisia kwa bei niliyolipa? Ni kwamba hawaamini kuwa nimelipa hiyo bei ama? Kama ni hivyo, kwanini wasingenipa nafasi ya kuwasilisha documents ambazo zinaweza kuthibitisha/kutothibitisha kuwa nimelipa kiasi ninachosema nimelipa?
Mkuu unaweza ku appeal kwa kuambatanisha vielezo vyako kuna kamati inajadili vitu kama hivyo muombe agent wako afanye hivyo na uattach documents zote kama tt copy na mawasiliano kati yako na muuzaji.
 
"Barbarosa, post: 17412954, member: 284899"]Hiyo ni gari KUU KUU na hapo unadanganya/umedanganywa haiwezekani gari ya miaka zaidi ya 8 iwe imetembea km 30 000 tu!
Huo ni uongo mweupe hizo km inazimaliza kwa mwaka mmoja tu na isitoshe kama ni kweli imetembea km 30 000 haiwezi ikauzwa
Dola 4 500 hilo haliwezekani, hivyo TRA wetu wako sawa kabisa kwa maana wewe ni muongo/ umedanganywa![/QUOTE]
Ofisini kwetu tulinunua Hilux pick up mwaka 2012 ikiwa brand new, na mwezi uliopita imeenda service ya 65000 km, na gari inapiga ruti za vijijini. So mi naona wewe ndo umekurupuka...
 
Hawafati culculator sometime....wana uplift bei utapata bleed ya macho bure
Kwa ufahamu wangu TRA wanaifuata sana Ile calculator yao. Wanaweza kufanya makosa assessment ikatoka kubwa lakini ukiobject wanarekebisha.
Cha kujadili hapa kingekuwa kama ilè calculator yao inaendana na uhalisia wa ununuaji wa gari.
 
Last month Mimi niliagiza Kluger ya mwaka 2005. CIF price ilikuwa US$ 5,200. TRA walinitwanga kodi ya TShs. 13,900,000/= na hakukuwa na room ya kunegotiate. Nilitii na kulipa bila shuruti.

Lipa tu mkuu. Tunahitaji sana pesa ili tuanze ujenzi wa viwanda haraka iwezekanavyo
 
Usiwe mbishi wenzetu gari wanatumia kutokana na toleo sio mpaka gari lizeeke. Gari ndani ya mwaka inatoka toleo jingine kwa hiyo mtu anauza na kuchukua model mpya. Usifikiri kwao gari wanatumia mpaka kiti cha dereva kinakuzoea kama huku kwetu.


Sijakuelewa unachomaanisha, unaweza kufafanua kama ukipenda!
 
Huyu sijui barbarosa ata aelewi anachopost humu, calculator ya TRA haiangalii km gari ngapi imetembea, bali ukubwa wa engine, mwaka iliyotengenezwa, aina ya gari plus model, aina ya mafuta inayotumia. TRA ni kweli ile calculator imewekwa kutukomoa ata mm nimewahi ona magari mengi kodi ni kubwa kuliko bei ya gari, alafu cha ajabu gari mpya inachajiwa kodi kubwa kuliko ya zamani ya model sawa, mfano kodi ya Toyota raum ya mwaka 2009 ni kubwa kuliko raum ya mwaka 2006, sasa wana discourage vipi uchakavu na uchafuzi wa mazingira? Nchi zingine ni vice versa.
 
Back
Top Bottom