TRA valuation system ya magari haiko fair

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
127
Kwanza niaze kwa kusema kuwa sina nia ya KULETA UCHOCHEZI! Maana siku hizi kila jambo linalosemwa au kuandikwa ambalo linalenga kutofautiana au kukosoa mfumo mpya wa uongozi wa nchi yetu basi linatafsiriwa kama uchochezi. Siku hizi hatuna budi kufunga midomo yetu na kumuacha Rais wetu afanye kazi yake.

Nirudi kwenye hoja iliyonileta. Sasa mimi nina malalamiko na TRA valuation system ya magari. Nimemwagizia mama yangu gari kutoa Japan. Gari yenyewe ni Volvo V50. Ni ya mwaka 2009 na ina mileage ya 30k. CIF ya gari hii ni $4,455 (approx. Tshs 9,701,000). Sasa sijui kwa kigezo gani kilichotumika, TRA’s assessment ime-value gari kwa $10,884 (approx. Tshs 23,727,120). Sasa kulingana na valuation ya TRA, nimechajiwa ushuru wa Tshs. 15,477,959. Hebu jaribu ku-imagine gari ununue kwa milioni 9, halafu TRA wakuchaji ushuru wa milioni 15! How fair is that? Gari ya mwaka 2009, ambayo sio chakavu, inawezaje kuchajiwa kodi 15m??? Halafu cha kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna room ya ku-negotiate.

Sasa basi, hivi ndivyo TRA walivyonipiga na ushuru wa kukatishana tamaa. Kulingana na invoice value ya gari (milioni 9), ushuru wake ni milioni 6. Hii ina maana, kama TRA wangetumia gharama nilizonunulia gari $4,455, basi ningechajiwa ushuru wa milioni 6 tu. Lakini kwa kuwa wamehamua ku-value gari, basi wameongeza nyongeza nyingine ya ushuru wa milioni 9. Hii ina maana kuwa, ile nyongeza ya valuation kutoka invoice value mpaka base value (milioni 23 – milioni 9 = milioni 14) ndiyo wameichaji ushuru wa milioni 9. So ushuru wa invoice value (milioni 6) + ushuru wa nyongeza iliyotokana na valuation (milioni 9) = ushuru wa milioni 15. Sijui niite huu ni uhuni au nini? Nakosa la kusema!

Kwa TRA kukomoa hivyo wanajaribu kutuma ujumbe gani? Tusiagize magari/vitu kutoka nje au ndo mambo ya ‘kumfanya kila Mtanzania haishi kama shetani”? Kwa style hii, kweli bandari yetu haitaacha kukauka?

Haya ni malalamiko yangu.
 
Hiyo ni gari KUU KUU na hapo unadanganya/umedanganywa haiwezekani gari ya miaka zaidi ya 8 iwe imetembea km 30 000 tu!
Huo ni uongo mweupe hizo km inazimaliza kwa mwaka mmoja tu na isitoshe kama ni kweli imetembea km 30 000 haiwezi ikauzwa
Dola 4 500 hilo haliwezekani, hivyo TRA wetu wako sawa kabisa kwa maana wewe ni muongo/ umedanganywa!
 
Barbabosa,

Kama kudanganya basi aliyedanganya ni yule aliyeniuzia. Mimi nimenunua gari online, na hiz ndizo details nilizopatiwa. Na hiyo valuation na kodi husika ilikokotolewa ka kutumia TRA Valaution Calculator. Ninavyozungumza hivi hata Shipping docs za hiyo gari zijazishika mkononi. Vinginevyo ninaweza kukutumia docs za manunuzi hujionee mwenyewe details za gari na manunuzi.

Ahsante kwa kunichallenge though...
 
Duh!Kuna umuhimu wa kuwauliza kwanza tra kabla ya mtu kuagiza gari ili ujue kabisa watakavyokutoza.Hizi gharama zinatisha na zinavunja moyo kabisa.

Yes. Hata mimi nimeshuri hivyo. Kwamba siku hizi ni muhimu kukokotoa kodi jinsi itakavyokuwa kabla hujaagiza gari. TRA Calculator inapatikana online.
 
Barbabosa,

Kama kudanganya basi aliyedanganya ni yule aliyeniuzia. Mimi nimenunua gari online, na hiz ndizo details nilizopatiwa. Na hiyo valuation na kodi husika ilikokotolewa ka kutumia TRA Valaution Calculator. Ninavyozungumza hivi hata Shipping docs za hiyo gari zijazishika mkononi. Vinginevyo ninaweza kukutumia docs za manunuzi hujionee mwenyewe details za gari na manunuzi.

Ahsante kwa kunichallenge though...

Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
 
Yes. Hata mimi nimeshuri hivyo. Kwamba siku hizi ni muhimu kukokotoa kodi jinsi itakavyokuwa kabla hujaagiza gari. TRA Calculator inapatikana online.
Pole jamaa yangu. Ushauri ungepitia website ya TRA wanaonyesha bei ya gari kulingana mwaka wa kutengenezwa na siyo bei uliyonunulia. Wanatumia retail selling price ambayo hiyo V50 ni kati ya dola 60,000 mpaka 67,000. Hapo ndiyo kukokotoa kunaanzia hapo na dhamani ya gari yako haitumiki uliyonunulia na itakuwa retail selling price kutoka kwenye list ya TRA na hapo unajikuta unalipa VAT peke yake karibu dola 8000. Kama alivyoshauri jamaa hapo before kuagiza angalia online calculator ya TRA
 
Hakika kodi ipo juu balaa, ofisi walitaka kununua gari suv ndogo tu, mwaka 2011 na cif 5300$ kadirio la kodi kutoka tra ilikiwa TZS 19,756,001/=
 
Hii ya TRA ni hatari balaa juzi mi niliwauliza gari Toyota Land Cruiser Prado ya 2002,4200cc nikaambiwa kodi ni sh milioni 19.6 hapo nikabroo mapigo,nikasema ngoja waendelee kuagiza wenye pesa
Hapa kazi tu!!
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom