TRA valuation system ya magari haiko fair

Mabolisozo mtaendelea kulia tu kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa unapangaje kununua gari bila kujua kodi yake hili litakuwa gari la kwanza kununua.......mbwembwe nyiiingiii...in msigwas voice
 
Hili la reli unanichanganya, tunajenga reli kwa kutumia mkopo wa exim bank china na hiyo reli inatakiwa ijiendeshe kibiashara iweze kurejesha mkopo, sasa unapokusanya tozo kwa wenye magari kwa ajili ya reli huo ni uonevu kabisa, niambie mkazi wa kinondoni anayefanya kazi azikiwe reli inamhusu nini? kama tumeweka kodi ya uchakavu ili watu wasilete gari kukuu mbona gari mpya bado inakodi kubwa kuliko hiyohiyo kukuu!
Exim bank hawatoi kiasi chote hata hyo ya kati serikali ya Japan haitoi yote...serikali yetu inachangia kwa kiasi flan vile vile inaweza kununua mabehewa na kadhalika(ninavyodhani) kumbuka kuna reli itajengwa ya kukutanisha na Nchi jirani..kuhusu ww kukaa kinondoni kwa mantiki ya reli kutokukuhusu ni suala la mipango ya serikali ni sawa na PAYE au MV licence unayolipia lakini maji anapelekewa mtu wa kibondo(maana yake wajibu wetu ni kulipa kodi matumizi ya kodi yanapangwa na serikali kwahyo tunaweza kupata benefit moja kwa moja au laaah)kumbuka hata ww ulipozaliwa ulikuwa hospitali na kodi ulikuwa hujalipa..
 
Kwanza niaze kwa kusema kuwa sina nia ya KULETA UCHOCHEZI! Maana siku hizi kila jambo linalosemwa au kuandikwa ambalo linalenga kutofautiana au kukosoa mfumo mpya wa uongozi wa nchi yetu basi linatafsiriwa kama uchochezi. Siku hizi hatuna budi kufunga midomo yetu na kumuacha Rais wetu afanye kazi yake.

Nirudi kwenye hoja iliyonileta. Sasa mimi nina malalamiko na TRA valuation system ya magari. Nimemwagizia mama yangu gari kutoa Japan. Gari yenyewe ni Volvo V50. Ni ya mwaka 2009 na ina mileage ya 30k. CIF ya gari hii ni $4,455 (approx. Tshs 9,701,000). Sasa sijui kwa kigezo gani kilichotumika, TRA’s assessment ime-value gari kwa $10,884 (approx. Tshs 23,727,120). Sasa kulingana na valuation ya TRA, nimechajiwa ushuru wa Tshs. 15,477,959. Hebu jaribu ku-imagine gari ununue kwa milioni 9, halafu TRA wakuchaji ushuru wa milioni 15! How fair is that? Gari ya mwaka 2009, ambayo sio chakavu, inawezaje kuchajiwa kodi 15m??? Halafu cha kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna room ya ku-negotiate.

Sasa basi, hivi ndivyo TRA walivyonipiga na ushuru wa kukatishana tamaa. Kulingana na invoice value ya gari (milioni 9), ushuru wake ni milioni 6. Hii ina maana, kama TRA wangetumia gharama nilizonunulia gari $4,455, basi ningechajiwa ushuru wa milioni 6 tu. Lakini kwa kuwa wamehamua ku-value gari, basi wameongeza nyongeza nyingine ya ushuru wa milioni 9. Hii ina maana kuwa, ile nyongeza ya valuation kutoka invoice value mpaka base value (milioni 23 – milioni 9 = milioni 14) ndiyo wameichaji ushuru wa milioni 9. So ushuru wa invoice value (milioni 6) + ushuru wa nyongeza iliyotokana na valuation (milioni 9) = ushuru wa milioni 15. Sijui niite huu ni uhuni au nini? Nakosa la kusema!

Kwa TRA kukomoa hivyo wanajaribu kutuma ujumbe gani? Tusiagize magari/vitu kutoka nje au ndo mambo ya ‘kumfanya kila Mtanzania haishi kama shetani”? Kwa style hii, kweli bandari yetu haitaacha kukauka?

Haya ni malalamiko yangu.

Kuhusu bei ya gari utakuwa umedanganya haina ubishi kuhusu hiyo bei, mtu yeyote anaweza check bei ya hiyo gari. Ila kuna mada ya msingi hapa, Kodi wanazotoza TRA ni kubwa hata kama wakivalue walichofanya huwezi toza kodi sawa na ununuzi na usafirishaji wa gari ina maana TRA anafaida Zaidi ya muuzaji. Hili suala sio la leo ni la muda mrefu sana.
TRA wenyewe wana bei zao kwenye system hawaangalii documents, mi huwa najiuliza aliyekaa akadesign hizo bei alikuwa na maana gani haswa
 
Ukweli ni kuwa hata logic ya kuzuia kuingiza gari la zamani haipo, maana kutokana na jinsi wanavyofanya ukokotozi wao, gari ya zamani kodi ni ndogo Zaidi ya jipya. Hizo kodi zipo kimaslai na sio kukataza kuingiza magari ya zamani
 
Hivi kile kitengo cha TRA-ELIMU KWA MLIPA KODI hakijaskia malalamiko haya? Mukuye mara moya bandungu banahitaji assistance
 
Duuuu pole sana mkuu hyo ndo system ilivyo hata ukiagiza gari jipya bei haiwezi kuwa chini sana na kigezo cha uchafuzi wa mazingira mi ndo huwa sikielewi kabisa maana kuna vitu vingi sana vinachafua mazingira sana kuliko hata hilo gar eg viwanda mbona hawavitoz kodi zaid ya bei ya kujengea daah mi nahisi kama nataka kuagza chuma labda nikajaribu bandari ya nchi jirani kunaweza kuwa n unafuuu fulani hivi.
 
Kwanza niaze kwa kusema kuwa sina nia ya KULETA UCHOCHEZI! Maana siku hizi kila jambo linalosemwa au kuandikwa ambalo linalenga kutofautiana au kukosoa mfumo mpya wa uongozi wa nchi yetu basi linatafsiriwa kama uchochezi. Siku hizi hatuna budi kufunga midomo yetu na kumuacha Rais wetu afanye kazi yake.

Nirudi kwenye hoja iliyonileta. Sasa mimi nina malalamiko na TRA valuation system ya magari. Nimemwagizia mama yangu gari kutoa Japan. Gari yenyewe ni Volvo V50. Ni ya mwaka 2009 na ina mileage ya 30k. CIF ya gari hii ni $4,455 (approx. Tshs 9,701,000). Sasa sijui kwa kigezo gani kilichotumika, TRA’s assessment ime-value gari kwa $10,884 (approx. Tshs 23,727,120). Sasa kulingana na valuation ya TRA, nimechajiwa ushuru wa Tshs. 15,477,959. Hebu jaribu ku-imagine gari ununue kwa milioni 9, halafu TRA wakuchaji ushuru wa milioni 15! How fair is that? Gari ya mwaka 2009, ambayo sio chakavu, inawezaje kuchajiwa kodi 15m??? Halafu cha kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna room ya ku-negotiate.

Sasa basi, hivi ndivyo TRA walivyonipiga na ushuru wa kukatishana tamaa. Kulingana na invoice value ya gari (milioni 9), ushuru wake ni milioni 6. Hii ina maana, kama TRA wangetumia gharama nilizonunulia gari $4,455, basi ningechajiwa ushuru wa milioni 6 tu. Lakini kwa kuwa wamehamua ku-value gari, basi wameongeza nyongeza nyingine ya ushuru wa milioni 9. Hii ina maana kuwa, ile nyongeza ya valuation kutoka invoice value mpaka base value (milioni 23 – milioni 9 = milioni 14) ndiyo wameichaji ushuru wa milioni 9. So ushuru wa invoice value (milioni 6) + ushuru wa nyongeza iliyotokana na valuation (milioni 9) = ushuru wa milioni 15. Sijui niite huu ni uhuni au nini? Nakosa la kusema!

Kwa TRA kukomoa hivyo wanajaribu kutuma ujumbe gani? Tusiagize magari/vitu kutoka nje au ndo mambo ya ‘kumfanya kila Mtanzania haishi kama shetani”? Kwa style hii, kweli bandari yetu haitaacha kukauka?

Haya ni malalamiko yangu.
Pole sana mkuu
 
Unatakiwa ununue gari mpya ambayo haichafui mazingira yetu hiyo ndiyo sababu!
Sasa gari mpya (ya miaka ya karibuni au hata mwaka huu) ushuru wake si ndio utakimbia jinsi ulivyo mkubwa...
TRA calculator yao wanaijua wenyewe, tungetegemea ukinunua gari latest basi ushuru uwe kidogo lakini ndio kwanza gharama ni ya kutisha...mwaka huu agiza gari za 2006 ndio ushuru wake upo chini kidogo
 
Ndio hivyo wanavyofanya. Na wmefanya hivyo kwasababu ya ujanja wa kibongo bongo kuzidi. Walipokuwa wana-calculate kwa kutumia bei ya manunuzi watu wakajiona ni wajanja, hivyo mtu akinunua gari kwa mfano dola 4000 anaongea na muuzaji anamwambia aandike 600 ili ushuru upungue. Hivyo ikabidi sasa watumie bei ya lile gari na model linapokuwa jipya halafu wanafanya depreciation kulingana na miaka gari lilivyotumika na kupata common price kwa magari yote yanayofanana. Huyo jamaa mwanzisha thread alikuwa bado anadhani zinatumika kanuni za zamani.
This makes sense na inabidi kila muagizaji acheck na TRA kwa kuwakilisha particulars[specs] za hilo gari kabla ya kuagiza ili aelewe gharama halisi ambazo itabidi alipe.
 
hapa suluhisho ni kutafuta jopo la wanasheria wa kodi wapambane na sheria na hiyo kalukuleta kandamizi. pia TRA watafute namna ya kuhakikisha watu hawachakachui hiyo CIF. haiwezekani waumize wananchi wengi kwasababu watu wachache walikosa uaminifu. kuna chama kinaitwa cha kutetea abiria, tukichangie pesa kitafute wanasheria.

pia tujiulize nchi nyingine za Africa zinafanyaje.
Mara nyingi sheria za kubana zinatokana na sisi wananchi kutumia vibaya mianya tunayopewa
 
Ninachoweza kuhisi hapa kwa uzoefu wangu wakuagiza magari Japan yawezekana gari uliloagiza la Volvo v50 halipo katika list ya database ya tarriff za TRA za kodi za magari hivyo wanachokifanya wao ni kukadiria ukichukulia hiyo gari inaonekana kwao TRA ni gari ya anasa basi lazima wakukamue,sasa nini chakufanya Muda wowote unapotaka kuagiZa gari baada ya kuliona kwenye mtandao kabla haujatuma hela nje jaribu kupitia calculator ya TRA kujua kama gari lako lipo katika list ya database yao kama halipo achana nalo maana likifika kodi wanakadiria tu kwa kukomoa.
 
Duuuu pole sana mkuu hyo ndo system ilivyo hata ukiagiza gari jipya bei haiwezi kuwa chini sana na kigezo cha uchafuzi wa mazingira mi ndo huwa sikielewi kabisa maana kuna vitu vingi sana vinachafua mazingira sana kuliko hata hilo gar eg viwanda mbona hawavitoz kodi zaid ya bei ya kujengea daah mi nahisi kama nataka kuagza chuma labda nikajaribu bandari ya nchi jirani kunaweza kuwa n unafuuu fulani hivi.
Kuagiza gari kutumia bandari za nchi ya jirani hakutakupa nafuu yoyote kwa sababu ukifika boarder lazima ukutane tena na TRA wakupigie hesabu zao na kwa kutumia calculator ile ile. Hivyo kwa TRA aliyepitisha bandari ya Mombasa na Dar es Salam wote sawa ila mmoja anatozwa akifika mpakani mwingine gari ikiwa bado bandarini.
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
Wewe Kuna magari hayakununuliwa mpaka msimu wake umeisha yalipaki showroom tuu.. usifikiri mbele kama bongo showroom zipo chache na fashion inabaki hiyo hiyo
 
Kuagiza gari kutumia bandari za nchi ya jirani hakutakupa nafuu yoyote kwa sababu ukifika boarder lazima ukutane tena na TRA wakupigie hesabu zao na kwa kutumia calculator ile ile. Hivyo kwa TRA aliyepitisha bandari ya Mombasa na Dar es Salam wote sawa ila mmoja anatozwa akifika mpakani mwingine gari ikiwa bado bandarini.
Duuuu hatri san hiii kumbe ndo hivyo tena
 
Kwanza niaze kwa kusema kuwa sina nia ya KULETA UCHOCHEZI! Maana siku hizi kila jambo linalosemwa au kuandikwa ambalo linalenga kutofautiana au kukosoa mfumo mpya wa uongozi wa nchi yetu basi linatafsiriwa kama uchochezi. Siku hizi hatuna budi kufunga midomo yetu na kumuacha Rais wetu afanye kazi yake.

Nirudi kwenye hoja iliyonileta. Sasa mimi nina malalamiko na TRA valuation system ya magari. Nimemwagizia mama yangu gari kutoa Japan. Gari yenyewe ni Volvo V50. Ni ya mwaka 2009 na ina mileage ya 30k. CIF ya gari hii ni $4,455 (approx. Tshs 9,701,000). Sasa sijui kwa kigezo gani kilichotumika, TRA’s assessment ime-value gari kwa $10,884 (approx. Tshs 23,727,120). Sasa kulingana na valuation ya TRA, nimechajiwa ushuru wa Tshs. 15,477,959. Hebu jaribu ku-imagine gari ununue kwa milioni 9, halafu TRA wakuchaji ushuru wa milioni 15! How fair is that? Gari ya mwaka 2009, ambayo sio chakavu, inawezaje kuchajiwa kodi 15m??? Halafu cha kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna room ya ku-negotiate.

Sasa basi, hivi ndivyo TRA walivyonipiga na ushuru wa kukatishana tamaa. Kulingana na invoice value ya gari (milioni 9), ushuru wake ni milioni 6. Hii ina maana, kama TRA wangetumia gharama nilizonunulia gari $4,455, basi ningechajiwa ushuru wa milioni 6 tu. Lakini kwa kuwa wamehamua ku-value gari, basi wameongeza nyongeza nyingine ya ushuru wa milioni 9. Hii ina maana kuwa, ile nyongeza ya valuation kutoka invoice value mpaka base value (milioni 23 – milioni 9 = milioni 14) ndiyo wameichaji ushuru wa milioni 9. So ushuru wa invoice value (milioni 6) + ushuru wa nyongeza iliyotokana na valuation (milioni 9) = ushuru wa milioni 15. Sijui niite huu ni uhuni au nini? Nakosa la kusema!

Kwa TRA kukomoa hivyo wanajaribu kutuma ujumbe gani? Tusiagize magari/vitu kutoka nje au ndo mambo ya ‘kumfanya kila Mtanzania haishi kama shetani”? Kwa style hii, kweli bandari yetu haitaacha kukauka?

Haya ni malalamiko yangu.

Mkuu pole sana na pia hongera kwa kulisema hili hapa
Hawa TRA sijui huwa wanawaza nini
Mtu umenunua gari una invoice ya lilikotoka na umelipia bank kwa transfer bado wanaleta UZAMANI wao wa ku uplift
Hivi mbona bei ya shati kariakoo na mlimani city yaweza kutofautiana wakati shati ni lile lile!! Kwa nini wao waamini bei ya mlimani city tu?
Pia waziri na majamishna kuteuliwa KISIASA na kusahau WELEDI ni tatizo kubwa wanakuwa hawajui wafanyacho zaidi ya kufyata mkia na kufuata maagizo yasiyo na uhalisia ya kisiasa
 
Kwa Mtz wa kawaida anayehitaji usafiri kwa bei rahisi kwa magari anayoona yanafanana mfano passo ya 2003 na ya 2009 kimtazamo sioni tofauti yake hajalo asilimia anajali figure so atachukua ya 2003 coz anaona he/will pay less
Sie tunaangalia figure hayo ya asilimia hayanihusu maana mie nataka ninunue kwa bei rahisi, halafu hiv ile calculator yao wanaifata kwelii maana nataka niagize gari ya 2005 sababu total import tax ndogo kuliko ya 2007, maana calculator inasema ya 2005 ni 2300ud ya cif 2200 na ya 2007 ni 3200usd,ni ya cif 4000, hapo ki % 2007 ina % ndogo ila kifigure ni bei kubwa sanaa
 
Back
Top Bottom