TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

kama hujui kaka omba kujulishwa..
mfanyabiashara ya mitumba na EFD wapi na wapi????
mauzo ghafi na 14,000,000 zinapatikana wapi kwenye biashara ya mitumba??? nina wasiwasi wewe sio mfanyakazi, lakini ungekuwa ni mfanyakazi halafu uka jumlisha makato yako yooote ya kodi kwa mwaka then ukaenda kujilinganisha na mfanyabiashara anayelipa kiwango hichohicho cha kodi kwa mwaka!! then utaona tofauti ya kipato na kimaisha kati yako na mfanyabiashara. mfanyabiashara anayelipa kodi kwa kiwango ninacholipa mimi kwa mwaka ni tajiri mwenye mabilioni ya shilingi.
DAMN IT!!! after all, kodi za wafanyabishara hulipwa na wateja wao
Wengine mi najua wanashabikia kitu wasichokijua. Naelewa sana mgomo huu ni kwa vile utapunguza faida za hao bandugu. Point ya kununua suruali elf 50 kama ndio true value yake tutanunua tu na kama sio tutaachana nayo. Labda ieleweke kwa sasa TZ inasogelea kuwa na middle income earners wengi tu na ndio maana shopping malls zinaongezeka. Kwa maana hiyo zile impulse buying zinapungua na badala yake budget zitachukua nafasi. Means, ili niweze kununua suruali ya elf 50, nitafanya savings hata miezi miwili na for sure nitanunua only what is relevant. Labda ukisema kuongeza makundi kulingana na sales maana mauzo ya 14,000,000 kwa mwaka bado ni mfanyibiashara mdogo, TRA wajaribu ku adjust zile brackets na kila mmoja awe na rate yake. Otherwise tujivunie kulipa kodi maana nchi inaendeshwa kwa kodi. Wewe fanya sehemu yako na mengine waachie wengine.
 
NasDaz Tatizo watu mnachanganya mambo...badala ya kunitajia hiyo bei, ulitakiwa kwanza unitajie aina ya mashine wanazotumia! Unless wawe wame-change siku za karibuni otherwise hiyo be unayosema wewe ni ya ETR ambazo hazifanyo remote transmission na badala yake data zinakuwa stored kwenye fiscal memory. Wakati Kenyan ETR hazifanyi remote transmission, hizi zilizokuwa approved na TRA zinafanya remote data transmission automatically to TRA. Kwa upande mwingine, ukija hilo la $ 80 hapa ndo wala haliingii kabisa coz' this's not all about having EFD but EFD ambazo moja kwa moja zita-communicate ni TRA. Sasa hizo za $ 80 ni just for general use. Huwezi hiyo ya $ 80 leo hii ukainunua, kisha zika-transmit data to TRA. Ukitaka kufahamu vizuri hizi mashine, unatakiwa kuchukua mfano wa calculator. IKiwa umesoma sayansi hususani zama hizi, bila shaka umeshaitumia sana Scientific Calculator! Nadhani unafahamu, wakati unanunua hizi calculator isn't all about scientific calculator...ingawaje zote ni scientific lakini bei zinatofautiana kutegemeana na functions na mambo mengine kama hayo...lakini zote ni scientific calculators!}

NasDaz unaongea na engineer tena wa miaka 15 iliyopita... Suala la kufanya data transimmison haliwezi kubadilisha bei ya ETR/ EFD toka $80 mpaka $500... Kwa technologia ya sasa huo ni wizi mtupu...zipo fax machine kubwa na zenyeku transmit data kubwa mpaka picture zenye megabyte kubwa zinazouzwa chini ya $100.Acha kuwadanganya watu wasiojua sisi tunaosafiri tunaweza kukwambia EFD ambazo TRA agentswanazouzwa zinanunuliwa wapi na zinapatikana huko kwa kiasi gani... KATIKA HILI NAOMBA UTULIE USIJE UKAFUNGUA UJINGA WAKO...

{hili la sh.38,000/- nishalisema sana hadi linatia uvivu! Kwa hayo mengine wala sidhani kama yana msingi. IKiwa unataka kuuza nafaka lazima utanunua mizani; mbona hamgomi na kulazimisha kupima kwa makopo/pishi kama zamani? Hizo mizani zikiharibika hamsumbuki kumtafuta fundi? Ikiwa una baa, mnaweka viti na meza...kwanini msiweke mabenchi kama kwenye pombe za kienyeji? Kwanini nongwa iwe kwenye EFDs peke yake? Hakuna biashara isiyo na gharama ambayo burden moja kwa moja inaenda kwa mfanyabiashara!}
NasDaz hapa unazungumzia gharama za kuboresha biashara ya mfanyabiashara na sio gharama za kusaidia TRA wakusanye kodi... KUMBUKA GHARAMA ZA EFD MACHINE NA VIAMBATANISHI VYAKE NI KWA MANUFAA YA TRA NA SIO MTEJA. Kwa nini mteja aingie gharama zisizoleta tija kwenye biashara yake?
NasDaz KUHUSU LA 38,000 ... NAKUSHANGAA UNAKANUSHA WAKATI TAMKO LA TRA LINASISITIZA WATU WOTE WENYE REVENUE YA KUANZIA 38,000 KWA SIKU WANASTAHILI KUWA NA MACHINE...wewe unatowa wapi maneno yako... unawalisha TRA maneno ambayo hawajayasema.. na mfano wako wa wafanyabiashara wa kariakoo.. sio valid hapa kwani hawakulengwa wafanyabiashara wa kariakoo tu nii.. wamachinga wote mpaka mama nitilie...

{Ili hao wezi wasipate mwanya basi mnawajibu wote kutumia hizo mashine...mbona majibu unayo wewe mwenyewe!!}

@NasDaz Nakuhurumia kwa kuwa sio mfanyabiashara na wala hujui usumbufu uliopo kwenye machine hizi... Machine hizi pamoja na kulipia $500 sio reliable zina breaks=down ya ajabu na hii italeta usumbufu na mwanya kwa wafanyakazi wa TRA wasio waaminifu kuwabuguzi wafanyabaishara... suala la u smart hapa halina mashiko tunao wafanyabiashara wa elimu mbalimbali wengine hata kutumia tu hizi machine ni TATIZO.

{Na ndio maana kuna kitu kinaitwa Cash Book! Mfanyabiashara smart, lazima atakuwa na cash book ikiwa anaona kuna mapungufu huko kwenye mashine.}

@NasDaz Cash book zipo siku zote na zimekuwa zinaleta karo wakati wa ukadiliaji kodi kwani TRA hawakubali matumizi yasio na risiti... wakati wanajua huduma nyingi hasa za vijijini hazina risiti... umeshawahi kula chakula kijijini kwa mama nitilie ukapewa risiti?...TATIZ NILILOOANA NI KWAMBA HUNA EXPERIENCE YA KUFANYA BIASHARA HAT KUUZA GENGE UNAONGEA VITU NADHARIA!!!

Mara zote huwa mnajisahau kwamba mnapotoa tuhuma kwa watumishi wa TRA kwamba wanadai rushwa; mnaacha kusema kwamba nanyi ni watoa rushwa wakubwa! Mnaenda kwa watumishi wa TRA huku mmebeba sura za kirushwa rushwa tu na kuwa easily approachable coz' mtoa rushwa anajulikana tu hata anavyo-approach desk lako!! Kwa kila mfanyakazi mshenzi mmoja wa TRA mla rushwa, pembeni yake kuna at least mfanyabiashara mshenzi mmoja mtoa rushwa.No justification katika kutoa rushwa kama ambavyo no justification ya mshahara mdogo kwa muomba rushwa! By the way, any smart business person lazima aangalie tax regulation za biashara anayotarajia kuifanya. Kama unauza nguo na kukwaza na kodi, badili bishara na kuuza mbepejeo za kilimo zisizo na kodi..

@NasDaz TATIZO NI LILELILE HUJAWAHI KUFANYA BIASHARA... ungekuwa unajua usumbufu wanaopata wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje wakati wa kulipa kodi usingeongea haya uliyoyasema... Kumbuka kodi haziko specified... kila siku kodi mpya inategemea afisa wa TRA ameamka vipi? ukianza kubishana naye mzigo unacheleweshwa na unachajiwa storage cost amabayo inaweza kuzidi kodi unayotaka kuikwepa... kwenye mazingira hayo hakuna pa kukimbilia... wanakwambia ukifanyiwa jambo nna afisa wa TRA ukamripoti ofisi za TRA .. KESI YA NGEDELE ANAPELEKEWA NYANI.... Unaweza ishia kuukosa mzigo wako ...kodi za TRA ZINATOA MWANYA MKUBWA KWAMAOFISA KUFANYA LOLOTE WATAKALO NA BADO ASIWE AMEVUNJA SHERIA...

{Yangekuwa na list ingekusaidia nini wakati TRA wanafanya mahesabu kwa kuangalia mauzo yako? Jambo la msingi ni wewe kuwa na cash book itakayokuwa na particular zote for your future use. Likewise, kama zamani ulikuwa unanunua mchele kwa sh.1000 na hulipi income tax na hivyo unauza hata kwa sh.1200; sasa unatakiwa kufahamu kwamba ukiuza utalipa income tax so, either huo mchele ununue chini ya sh.1000 au uuze zaidi ya 1,200/-. Msijifanye mnatuhurumia end users; kadanganyeni wengine.}

@NazDaz napata mashaka kama hat kodi zenyewe unazijua.. hapa hatuzungumzii Income TAX. tunazungumzia import tax na VAT Zinazolipwa pale customs na hakuna mfanyabiashara anayekwepa kulipa hili ... hapa tunazungumzia kodi ya mapato ambayo inalipwa kwa mwaka baada ya kutoa manunuzi na gharama za uendeshaji.... TATIZO LIPO KWAMBA EFD HAZISAIDII KUJUA GHARAMA ZA MANUNUZI WALA GHARAMA ZA UENDESHAJI... ndio ambapo kwenye matatizo makubwa...kwani wao wanaangalia revenues tu....

{Ni matumaini yangu kwamba haya hayana uhusiano na EFDs; sana sana yanawakilisha ile simulizi ya Mbwa Mwitu na Mwana Kondoo! Mbwa Mwitu kamjia juu Mwana Kondoo kwamba kwanini anachafua maji wakati anamuona yeye (mbwa mwitu) anakunywa maji! Mbwa Mwitu alitoa madai haya wakati yeye amekaa upande wa juu wa mto na Mwana Kondoo yupo kwa chini. Mwanakondoo akajibu, nayachafua vp wakati mimi nipo upande wa bondeni na wewe kwenye mwinuko? Mbwa Mwitu akakaza, "usibishe wewe, ilikuwa mwaka juzi ile!!! Mwana Kondoo akajibu, mbona mie nimezaliwa mwaka huu?! Mbwa Mwitu kv shida yake ilikuwa ni kitoeo; akaja na lingine...kama hukuwa wewe basi baba ako, kama si baba ako basi mama ako; kama c mama ako basi kaka ako, kama si......ili mradi tu Mmbwa Mwitu apate kitoweo! Mbwa Mwitu ana visa}

MFANO WA KITOTO... linapokuja suala la KODI masuala yote yanayohusu kodi yanachangia katika ukadiliaji wa kodi... kama mmeagiza mzigo wa pamoja kwa nini kusiwe na njia ya kuahinisha kila mwagizaji amenunua kiasi gani na kodi yake ni kiasi gani? kwani hili liapelekea baadhi ya wafanyabiashara walioagiza mzigo wa pamoja na hawana risiti za manunuzi wa import tax na VAT at customes kuonekana wanamauzo makubwa na kukata kodi ya mapato kubwa wakati wana matumizi ambayo wana shindwa kuyatolea maelezo kwa kukosa risiti..

Muonamambo
A town
 
Huyo mlaji ni nani kama sio wewe !? Kwa ushabiki unajitoa fahamu .unajila nyama yako mwenyewe .mwenzangu mzimaa kweli wewe !?

Kwa hiyo unataka kusema hao wafanyabiashara wanawatetea walaji?? Hawana lolote, labda kama wewe pia ni mwenzao! Wewe unajua sisi Wafanyakazi tunakatwa kiasi gani cha PAYE on a monthly basis??. Wangekuwa na huo huruma kwa mlaji si wangeshusha bidhaa zao?? Mbona wanalangua mara 2 mbili??

Wewe ndiye unaanza kujitoa faham na kutetea upuuzi! Kodi kwa maendeleo ya nchi!
 
NAZDAZ unaongea na engineer tena wa miaka 15 iliyopita
NAZDAZ unaongea na engineer tena wa miaka 15 iliyopita... Suala la kufanya data transimmison haliwezi kubadilisha bei ya ETR/ EFD toka $80 mpaka $500... Kwa technologia ya sasa huo ni wizi mtupu...zipo fax machine kubwa na zenyeku transmit data kubwa mpaka picture zenye megabyte kubwa zinazouzwa chini ya $100. Acha kuwadanganya watu wasiojua sisi tunaosafiri tunaweza kukwambia EFD ambazo TRA agentswanazouzwa zinanunuliwa wapi na zinapatikana huko kwa kiasi gani... KATIKA HILI NAOMBA UTULIE USIJE UKAFUNGUA UJINGA WAKO...

Mkuu wangu muonamambo, hizi mashine zipi za aina nyingi...siwezi kukulazimisha lakini huwezi kuchukua ile ya $80 kutoka china ikafanya 100% similar tasks kama zilizoidhinishwa na TRA. Hizi za TRA ni custom made na hata hawa supplier, si kwamba anaenda kununua popote anapojisikia yeye, bali kwa manufacturer aliyehidhinishwa na Commissioner wa TRA kwa kuangalia vigezo vilivyowekwa. Tafuta tangazo kwenye gazeti la serikali(government gazette No. 50, vol. 90 la december 14,2012. Humo ndimo wameweka vigezo vya mashine gani zinahitajika. By the way, hebu pitia hapa uone bei ya Kenya kwa mashine zenye sifa kama hapa ili tuone kama kuna tofauti kubwa: Fiscal Solutions / ETRs : Datecs DP 50 | Cecypo

NAZDAZ hapa unazungumzia gharama za kuboresha biashara ya mfanyabiashara na sio gharama za kusaidia TRA wakusanye kodi... KUMBUKA GHARAMA ZA EFD MACHINE NA VIAMBATANISHI VYAKE NI KWA MANUFAA YA TRA NA SIO MTEJA. Kwa nini mteja aingie gharama zisizoleta tija kwenye biashara yake?

Kwani unapotumia risiti za kawaida vile vitabu hulipii? Kwa wale wanaotumia risiti za computer, ile PC na karatasi wanakuwa wamepata bure? Mbona husemi hizo gharama ni kwa manufaa ya TRA?

KUHUSU LA 38,000 ... NAKUSHANGAA UNAKANUSHA WAKATI TAMKO LA TRA LINASISITIZA WATU WOTE WENYE REVENUE YA KUANZIA 38,000 KWA SIKU WANASTAHILI KUWA NA MACHINE...wewe unatowa wapi maneno yako... unawalisha TRA maneno ambayo hawajayasema.. na mfano wako wa wafanyabiashara wa kariakoo.. sio valid hapa kwani hawakulengwa wafanyabiashara wa kariakoo tu nii.. wamachinga wote mpaka mama nitilie...

Nani amekanusha ndugu yangu wakati nimesema wazi kwamba ingawaje sheria inasema kwamba ni wale wenye annual sales turnover ya TZS 14m and above, lakini wengi hawa hawajaguswa coz' hiyo 14m ni moja tu ya vigezo tajwa! Mathalani, lengo la TRA kwa awamu hii ni kuwafikia wafanyabiashara 200K, ingekuwa hiyo 14m ndio kigezo pekee basi hao wafanyabishara 200K wangepatikana kwenye wilaya moja tu au mbili kwa hapa Dar es salaam. Halafu umeleta uongo uliovuka mipaka...usidanganye watu...kwenye mpango huu hao mama nitalie wala machinga hawajahusika. Si vizuri kusema uongo.

Nakuhurumia kwa kuwa sio mfanyabiashara na wala hujui usumbufu uliopo kwenye machine hizi... Machine hizi pamoja na kulipia $500 sio reliable zina breaks=down ya ajabu na hii italeta usumbufu na mwanya kwa wafanyakazi wa TRA wasio waaminifu kuwabuguzi wafanyabaishara... suala la u smart hapa halina mashiko tunao wafanyabiashara wa elimu mbalimbali wengine hata kutumia tu hizi machine ni TATIZO..

Hivi kwanini unadhani mie sifanyi biashara? Au ulitarajia niwaunge mkono ndipo uone nami nafanya biashara? BIashara zako unafanyia wapi? Kama Dar, nipo tayari kukupeleka ninakopatia mkate wa ziada....hizo mashine watu tumeanza kutumia tangu 2011. By the way, nyie mmezigomea, hiyo breakdown umeiona wapi? Kwani hivi sasa ni mara ya kwanza kwa mashine hizi kutumika? hivi una habari kwamba suppliers wengi wa Kenya ndio hao hao wana-supply Tanzania? Kwahiyo unataka kuniambia wanazopeleka Kenya hazina break-down lakini wanazoleta hapa ndizo zenye breakdown?

Cash book zipo siku zote na zimekuwa zinaleta karo wakati wa ukadiliaji kodi kwani TRA hawakubali matumizi yasio na risiti... wakati wanajua huduma nyingi hasa za vijijini hazina risiti... umeshawahi kula chakula kijijini kwa mama nitilie ukapewa risiti?...TATIZ NILILOOANA NI KWAMBA HUNA EXPERIENCE YA KUFANYA BIASHARA HAT KUUZA GENGE UNAONGEA VITU NADHARIA!!!

Yaani we ni mtu wa ajabu si kidogo...una-conclude kwamba I know nothing wakati hunifahamu? Kwa taarifa yako nimefanya sana biashara na bado nafanya...nikikuambia nimeanza kufanya biashara nikiwa umri gani unaweza usiamini.

TATIZO NI LILELILE HUJAWAHI KUFANYA BIASHARA... ungekuwa unajua usumbufu wanaopata wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje wakati wa kulipa kodi usingeongea haya uliyoyasema... Kumbuka kodi haziko specified... kila siku kodi mpya inategemea afisa wa TRA ameamka vipi? ukianza kubishana naye mzigo unacheleweshwa na unachajiwa storage cost amabayo inaweza kuzidi kodi unayotaka kuikwepa... kwenye mazingira hayo hakuna pa kukimbilia... wanakwambia ukifanyiwa jambo nna afisa wa TRA ukamripoti ofisi za TRA .. KESI YA NGEDELE ANAPELEKEWA NYANI.... Unaweza ishia kuukosa mzigo wako ...kodi za TRA ZINATOA MWANYA MKUBWA KWAMAOFISA KUFANYA LOLOTE WATAKALO NA BADO ASIWE AMEVUNJA SHERIA...

unachekesha sana unavyong'ang'ani kwamba sifahamu biashara!! Hivi what's so special katika kufanya biashara hadi uamini kwamba sijawahi kufanya biashara?! Lakini kwa upande mwingine, acha kukuza mambo....kila siku kodi mpya; kodi zipi? Anyway, niambie kodi ya siku za karibuni ambayo ni ngeni na haipo sehemu yoyote duniani. Hakuna kodi inayoingizwa sokoni bila kuidhinishwa na bunge.

TATIZO HAT KODI ZENYEWE HUZIJUI Income TAX inalipwa pale customs na hakuna mfanyabiashara anayekwepa kulipa hili ... hapa tunazungumzia kodi ya mapato ambayo inalipwa kwa mwaka baada ya kutoa manunuzi na gharama za uendeshaji.... TATIZO LIPO KWAMBA EFD HAZISAIDII KUJUA GHARAMA ZA MANUNUZI WALA GHARAMA ZA UENDESHAJI... ndio ambapo kwenye matatizo makubwa...kwani wao wanaangalia revenues tu..
..

Yaani wewe umejikita katika kuniambia kwamba sifahamu lolote wala chochote kwavile tu sikubalini na hoja zako! We ni mtu wa ajabu sana...lakini ni matumaini yangu tutaendelea kiungwana hivi hivi si kama mwenzako mmoja alipoona kashifa na kejeli hazitoshi, akaanza matusi.

Turudi huko kwenye hizo kodi ambazo mnazijua nyinyi tu na wengine wote hawazijui...yaani Income Tax na Kodi ya Mapato ni vitu viwili tofauti? Unalipa income tax customs kwa income ipi? Yaani ile kuleta mzigo tu; kinachofuata ni Income Tax hapo hapo?! Halafu Import Duty, Excise Duty na VAT unaenda kulipia wapi?

MFANO WA KITOTO.....
Sio mfano wa kitoto, hapo ndo sehemu yake...ni mfano uliobeba fasihi!

linapokuja suala la KODI masuala yote yanayohusu kodi yanachangia katika ukadiliaji wa kodi... kama mmeagiza mzigo wa pamoja kwa nini kusiwe na njia ya kuahinisha kila mwagizaji amenunua kiasi gani na kodi yake ni kiasi gani?
kwani hili liapelekea baadhi ya wafanyabiashara walioagiza mzigo wa pamoja na hawana risiti za manunuzi wa import tax na VAT at customes kuonekana wanamauzo makubwa na kukata kodi ya mapato kubwa wakati wana matumizi ambayo wana shindwa kuyatolea maelezo kwa kukosa risiti..

Hapa sijauelewa kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Ni vema kabla ya kuchangia ukasoma uzi mzima kama unahisi kuwa ujapata uelewa wa kutosha kuhusu VAT na Income Tax. Mana wachangiaji wengi wanachanganya hayo mambo wawili. Naomba niwaulize wafanyabiashara mnapokwenda kukadiliwa kodi uwa mnawaeleza TRA kuhusu faida mliyopata au mnapeleka vitabu vyenu vya mauzo ili mkadiliwe kodi ya mapato?
 
Kimweri,
ume-challenge ili mradi tu u-challenge au unaamini ulikuwa na base za ku-challenge? What do you mean unaposema mfanyakazi mwenye salary ya TSh. 180K hiyo ni net salary? Unless kama unataka kuniambia hujawahi kuajiriwa maishani mwako otherwise think twice. Na hata kama hujawahi kuajiriwa, tafuta salary slip(S.L) ya yeyote kisha iangalie. Juu kabisa ya S.L panaandikwa Basic Salary...ndiyo hiyo 180K. Chini yake wana-list non-taxed income ambayo ni 10-15%. Normally hii ni kwa ajili ya NSSF na wenzake. Wakishakata hiyo 10-15% from 180K, kinachobaki ni taxed income kwa ajili ya PAYE. Kinachobaki ndiyo Net Salary mfanyakazi anayoenda nayo nyumbani! So how come unasema kwamba hiyo 180K ni net pay? Ningekuelewa endapo ungesema KCC sio 180K otherwise ulichosema ni completely FALSE.

Hiyo hoja ya 38K kwa siku nimeshasema sana hapa! Tusijitie upofu na kujifanya hamnazo...narudia, tusijitie upofu na kujifanya hamnazo ili mradi tuweze kupinga kwavile ndicho tunachopenda kufanya! Wale wanaogoma pale Kariakoo si kweli hata kidogo kwamba ndio wanaofanya mauzo ya sh. 38,000/- kwa siku. Sh.38,000/- ni mchele 10kg@1500+maharage 10kg/2000+unga 15kg@1000=50,000/-....yaani tayari kuna excess ya sh. 12K. Maduka kama hayo yapo mitaa ya ndani ndani huku uswahilini ambayo in most cases yana sifa zifuatazo....mteja anasimama dirishani huku akigonga nondo kwa sarafu kwavile muuzaji yupo chumbani; haya ni yale maduka yanayouza mafuta ya taa na ya kula ya mia mia; haya ni yale yanayouza majani kwa sh.50/-, haya ni yale maduka ambayo wanakuwa na vidaftari vya kuandika waliochukua sukari robo kilo na kuahidi watalipa next time...in most cases, maduka haya ni yale yanayohudumia wakazi ambao wapo within 100m radius. Tuwe wakweli, hata kama TRA wamesema ni kwa ajili ya wafanyabiashara wenye annual sales ya TSh. 14m; hawa wengi wao hawajaguswa...

Yakhe, kama ukitazama nilichoandika utaona kwamba nimeongelea mtu anayepata Net pay ya 180,000. Sijaongea Basic pay ya 180,000.

Hoja yangu iko simple ndugu, kama TRA mnatambua kuwa 14M annual sales ni duka l amaharage na mchele, basi ongezeni kiwango cha wafanyabiashar awanaohitaji kutumia hizi mashine.

RUDI KASOME nilichoandika. DO NOT skim it.

ukijadili hoja usirukie kwenye conclusion kama haujaelewa kilichosemwa na mtoa hoja.

Pili: kama hawa wa 14M hawatozwi VAT, then hakuna haja ya kugombana sana na hawa watu, incentive ya kukusanya mapato kutoka kwa hawa watu haileti maana ya kibiashara. mtu mwenye sales turnover ya 14M inamaana ana gross profit before operational expenses ya around 1.4-2M kwa mwaka, ukiondoa gharama za uendeshaji wa Biashara,gross profit inakuwa si zaidi ya 200,000. sasa hii ndio TRA wanatakiwa wachukue asilimia zao kwa mwaka. huyu mtu faida yake(net profit) haiwezi kuzidi 100K kwa mwaka, HUYU mtu huwezi kumunulisha mashine ya laki 6. UNAMUONEA.

Mshukuru mungu wafanya biashara wengi wanafanya BIASHARA za mazoea, lakini wengi wanapata hasara kubwa sana, ndio maana ni wafanyabiashara wachache sana wanamudu biashara kwa muda mrefu, na wanaomudu ni wale wezi/matapeli. UKIFANAY biashara kwa kufuata mchanganuo niliouweka hapo juu lazima ufilisike, in 2 years.

Sasa wewe unavyosema watu wa Kariakoo wamnauza zaidi ya 38K, HAO TRA kiherehere cha kuweka minimum requirement ya 14M wamekitolea wapi?au wewe una-data zaidi yao? kwa maan hii inabidi waje hadi magengeni kwetu wafunge machine.

SHIDA huyo Mpuuzi wa TRA aliyetembea nchi za wenzetu akaona kila kitu kina electronic receipt akili zake chache, UMEME nchi nzima 20% coverage, umeme unawaka less than 50% of the productive time mwaka mzima, leo hii unamlazimisha mtu ategemee hiki kitu,kweli? kuna mpuuzi hata mmoja wa TRA anayeendesha gari bila kuweka mafuta? sasa wafanyabiashara wakae wategemee dubwana ambalo litahitaji high maintenace(generator) wakati mitaji yenyewe ya milioni 2?
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD. TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona. Nakupongeza sana kwa kuwasaidia tra mahesabu. Labda watafunguka akili.
 
NAZDAZ unaongea na engineer tena wa miaka 15 iliyopita... Suala la kufanya data transimmison haliwezi kubadilisha bei ya ETR/ EFD toka $80 mpaka $500... Kwa technologia ya sasa huo ni wizi mtupu...zipo fax machine kubwa na zenyeku transmit data kubwa mpaka picture zenye megabyte kubwa zinazouzwa chini ya $100. Acha kuwadanganya watu wasiojua sisi tunaosafiri tunaweza kukwambia EFD ambazo TRA agentswanazouzwa zinanunuliwa wapi na zinapatikana huko kwa kiasi gani... KATIKA HILI NAOMBA UTULIE USIJE UKAFUNGUA UJINGA WAKO...

Mkuu wangu muonamambo, hizi mashine zipi za aina nyingi...siwezi kukulazimisha lakini huwezi kuchukua ile ya $80 kutoka china ikafanya 100% similar tasks kama zilizoidhinishwa na TRA. Hizi za TRA ni custom made na hata hawa supplier, si kwamba anaenda kununua popote anapojisikia yeye, bali kwa manufacturer aliyehidhinishwa na Commissioner wa TRA kwa kuangalia vigezo vilivyowekwa. Tafuta tangazo kwenye gazeti la serikali(government gazette No. 50, vol. 90 la december 14,2012. Humo ndimo wameweka vigezo vya mashine gani zinahitajika. By the way, hebu pitia hapa uone bei ya Kenya kwa mashine zenye sifa kama hapa ili tuone kama kuna tofauti kubwa: Fiscal Solutions / ETRs : Datecs DP 50 | Cecypo

Watanzania sisi ni watu wa- ajabu, yani wewe unapewa njia rahisi y akitu flani, unaona sifa kwa kuwa serikali imeamua kufuata njia ya kipuuzi inayo-inflate bei. transmission moja ya TRA ya mahesabu ya siku nzima haizidi 64KB,kwa viwango vya sasa vya data, hii si zaidi ya 25MB kwa mwaka. Naamini EATELI na VODAKOM hii bando ya 25MB wanauza around 100-200TZS kwa retail price, kwa maana ya kuwa serikali ingeweza kuuziwa kwa bei ndogo zaidi. sasa wewe gharama za TZS 100 kwa mwaka ziongeze bei hadi 70000K? unaona sifa kujiuzia kidubwasha ambako huko kilichotoka kinauzwa bei chee kisa uliomba customization?kweli?mashine kuwa aghali sio kosa la wafanyabiashara, ni upuuzi wa serikali, dunia ya sasa ya kufuata austerity hakuna atakayekusifia ukinunu EFD printer ya $50 kwa $500. unaonekana ----- mtozeni. siwashangai lakini hawa kwenye procurement hata bei ya mkungu wa ndizi wanaweka laki 1.

NAZDAZ hapa unazungumzia gharama za kuboresha biashara ya mfanyabiashara na sio gharama za kusaidia TRA wakusanye kodi... KUMBUKA GHARAMA ZA EFD MACHINE NA VIAMBATANISHI VYAKE NI KWA MANUFAA YA TRA NA SIO MTEJA. Kwa nini mteja aingie gharama zisizoleta tija kwenye biashara yake?

Kwani unapotumia risiti za kawaida vile vitabu hulipii? Kwa wale wanaotumia risiti za computer, ile PC na karatasi wanakuwa wamepata bure? Mbona husemi hizo gharama ni kwa manufaa ya TRA?

Hakuna mfanya Biashara anyefanya kitu kisichokuwa na manufaa kwake, kama ukikuta kaweka PC dukani kwake, hiyo ni kwa faida yake sio TRA. huna sababu ya kumwambia kwa kuwa umeweza kununua PC basi nunua na AC. Sio kazi yako, kwenye nchi za wenzetu zenye open market unafukuzwa at point blank.

hii ni kweli 100%
tena wengine ukinunua mzigo kwao wanakuomba uwaruidishie risit endapo utafika salama unapopeleka
mzigo.hiyo risti anapewa mtu mwingine

Sasa hapo unailaumu Serikali?..Mtu anaejua kuwa una akili timamu halafu anakushauri ujinga na ukaukubali,,Anakudharau sana..Ukipewa risiti ya laki 7 kwa mauzo ya mil 7 ujue hakuna Mjinga zaidi yako!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu wangu, umesema jambo sahihi kabisa...ili kutoa mzizi wa fitina wapewe bure though am certain bado watakataa coz' base ya madai yao haipo kwenye bei bali ni kwamba hawataki tu hizi mashine kv wanafahamu udanganyifu wao utakuwa unaelekea]

Tatizo kubwa na la msing hapa ni zaidi ya Machine za EFD ni mfumo mzima wa kodi... Wafanyabiashara wana madai zaidi ya machine za EFD ambazo kwa sababu za makusudi serikali chini ya TRA ndio inachokishililia.. IKUMBUKWE Wafanyabiashara hawa ni walipa kodi wazuri wa kodi zao walizokuwa wanakadiliwa.

Madai ya wafanya biashara ni haya..

  1. Kwanza ni BEI ya machine ulikinganisha na BEI ya soko ya machine husika kwa soko la sehemu nyingine duniani.. kenya tu mashine zinapatikana kwa chininya TZS 350,000. ukienda china na kwingineko ni chini ya $80.
  2. Gharama kubwa na usumbufu unaotokana na machine hizo ukilinganisha na cash flow za mlengwa yaani mfanyabiashara anayeingiza 38,000 Kwa siku... Gharama za karatasi moja ni 6000 na gharama za maintenance ambazo ni zaidi ya laki 3 kwa mwaka na usumbufu wa kuripoti TRA NA KWA WAKALA kila machine inapoaharibika...
  3. Utaratibu wa faini kwa amabaye atashindwa kutumia machine hizo unatoa mwanya kwa wafanayakazi wasio waaminifu wa TRA( ambao ni wengi) na Askari waliozoea Rushwa kuleta taabu kwa wafanyabiashara.
  4. Machine za EFD hazionyeshi gharama za manunuzi na gharama za uwendeshaji ambapo hapo hasa ndio penye tatizo kubwa... Gharama nyingi za manaunuzi ama hazina risiti ama zina risiti ambazo hazilingani na gharama halisi... HILI LITAPELEKEA mfanyabiashara kutozwa kodi kubwa kuliko hanavyostahili kutokana na kukosekana na kumbukumbu za manunuzi.
  5. Mfumo mzima wa biashara ama zimetoka nje ya nchi ambazo ulipiwa kodi custom.. kodi ya import duty and VAT...Au zimenunuliwa kwa wakulima na wavuvi ama wafugaji ambao hawatoi risiti...Kwa zinazopita Customs ukadiliaji umekuwa shida kubwa... mzigo huo huo amabo haupishani hata miezi mitatu unaweza kuwa na kodi tofauti na tena yenye tofauti ya kutisha ... hii imeleta mianya ya rushwa kwa watumishi wa TRA na kupelekea wafanyabiashara kulipa malipo mengi yasiokuwa na risiti... amabayo yatakuja kumfanya alipe malipo mengi ya kodi ya mapato.
  6. Kodi zinazotozwa na TRA Customs hazinlingani na thamani halisi ya bidhaa zinazoingizwa na kushawishi wafanaya biashara kukubali kutoa rushwa ili angalau aweze kuuza bidhaa yake kwa gharama nafuu.
  7. kwa mazao yanaotka kwa wakulima mengi hayana risiti na kwa stahili hii mfanyabiashara atalazimaika kulipa zaidi kodi za mapato.
  8. Kwa ujumla mfumo mzima wa kodi unatakiwa kuangaliwa upwa ili uwe wazi na unaoshawishi wafanyabiashara kulipa kodi stahiki na kupunguza mianya ya Rushwa .... GHARAMA Nyingi za uendeshaji hazina risiti na hili ni tatizo la kuangalia ..
  9. Mfumo hauruhusu uingizaji wa mzigo wa pamoja ( sharing importation) ambapo kila mfanyabiashara aliyeshare container atalipa stahiki yake na mzigo wake kuwa na thamanai ya manaunuzi...
  10. kwa ujumla kufanya baishara Tanzania hasa kwa sekta zisizo rasmi zimekabiliwa na kodi nyingi zisizo na kichwa wa miguu... kodi za pango... kodi ya takataka.. kodi za fire... kodi za mabango... kodi za hamashauri... nk nk...

Tubadilike nchi ni yetu sote... sekta hii nayo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa... iundwe tume maalumu ya kurekebisha mfumo mzima wa ulipaji kodi na kuwaka fair ness kwa pande zote.... na kusitisha zoezi la EFD

Muonamambo

A town

Naona kila mtu anasema amefanya 'UTAFITI' juu ya hii EFD lakini sifahamu kama ni kweli wamefanya au wamesikia tu watu wakizungumza tu mabarazani..

1. Watu wanachanganya kati ya
Electronic Cash Register (ECR)
Na Electronic Fiscal Device
(EFD). Hizi ni mashine aina
mbili tofauti kimadhumuni
Hizo ECR unaweza nunua
popote na kuzitumia, na ndizo
hizo ukienda China watu
huzikuta na kuja kuleta madai
ya bei.
EFD huwezi ikuta dukani
kiholela na kuinunua ili
uitumie sababu inatengenezwa
kwa matakwa maalum ya kila
nchi husika,na si kila
mtengenezaji anatengeneza

2. Kuhusu Kenya,
kwanza hakuna EFD kenya ipo
chini ya 600000 TZS.
Pili EFD za kenya zipo tofauti
kiutendaji ukilinganisha na za
hapa,Wao walikuwa wa kwanza
kutumia hizi mashine,
na ilikuwa haina mfumo wa
kutuma Z Report kwenda KRA,
sisi tulichofanya kwa za kwetu
ni kuziongezea uwezo wa
kutuma hiyo Z Report kila siku
kwenda TRA
(hapa ushamuongezea kazi ya
ziada mtengenezaji » bei
itapanda),,
baada ya sisi kufanya hili KRA
iliikubali TRA na wakaja
kujifunza,Na wao siku si nyingi
wataanza zoezi upya liwe
kama la TRA.

3. Kila nchi inaagiza itengenezewe
EFD vile inavyotaka iwe, ndiyo
maana hata bei hazifanani

4. Ushauri:
Hizo kodi nyingine
wafanyabiashara wanazolipa
inabidi wakae na wanaowatoza
kujua jinsi gani ya kuweza
kuzipunguza, mfano kodi ya
jengo,takataka,zimamoto,n.k

Mnazunguka mbuyu tu hizo mashine zinajulikana bei na mpaka zinakotengenezwa na softiware iliyotumika hivyo kutaka kuwaibia watu sio rahisi.
Mkiendelea kupotosha tutaweka kila kitu tuwavue nguo msifikiri watanzania ni wajinga ama awafuatilii.
 
NDO maana Uganda,rwanda hawana bandari ila bidhaa bei rahisi kama dubai.

_kuhusu hizo machine kama mwisho wa mwaka watu wengi huwa wanauza dead stock kwa bei ya hasara,yaani bei chini ya waliyonunulia je,hiyo machine itatambuaje hilo?
_kama kuna TRA humu anijibu
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.

Kwa uwezo wangu sihitaji kujuwa yote hayo uliyoandika. Ninachoamini ni kwamba, ulipoanzisha biashara ulijiandaa. Ukatafuta nyumba au chumba au sehemu, ukaweka grill, ukatengeneza fremu, n.k. Hiyo ndo sehemu ya mtaji. Sikushauri ununue EFD kwa kutumia faida yako. Hiyo utaipata baadaye. Sasa hapoTRA wanasema nunua na EFD machine unakataa.

Kwa nini unakataa? Gharama zote ulikubali lakini EFD hutaki, kwa nini?

Wafanyabiashara wengi wa tz elimu ni tatizo na kadri unavyoshuka chini, elimu pia ni down. Kwao faida ni kukwepa TRA. TRA nao elimu kuunga unga tu. Hili limekuwa kundi kubwa linalohongana pesa na kuelekezana kukwepa kodi kila siku.

Nunueni EFD, lipeni kodi. Hao watu wa serikali wanaobugia kodi zetu, tutapambana nao mbeleni.
 
Yakhe, kama ukitazama nilichoandika utaona kwamba nimeongelea mtu anayepata Net pay ya 180,000. Sijaongea Basic pay ya 180,000.

Hoja yangu iko simple ndugu, kama TRA mnatambua kuwa 14M annual sales ni duka l amaharage na mchele, basi ongezeni kiwango cha wafanyabiashar awanaohitaji kutumia hizi mashine.

RUDI KASOME nilichoandika. DO NOT skim it.

ukijadili hoja usirukie kwenye conclusion kama haujaelewa kilichosemwa na mtoa hoja.

Pili: kama hawa wa 14M hawatozwi VAT, then hakuna haja ya kugombana sana na hawa watu, incentive ya kukusanya mapato kutoka kwa hawa watu haileti maana ya kibiashara. mtu mwenye sales turnover ya 14M inamaana ana gross profit before operational expenses ya around 1.4-2M kwa mwaka, ukiondoa gharama za uendeshaji wa Biashara,gross profit inakuwa si zaidi ya 200,000. sasa hii ndio TRA wanatakiwa wachukue asilimia zao kwa mwaka. huyu mtu faida yake(net profit) haiwezi kuzidi 100K kwa mwaka, HUYU mtu huwezi kumunulisha mashine ya laki 6. UNAMUONEA.

Mshukuru mungu wafanya biashara wengi wanafanya BIASHARA za mazoea, lakini wengi wanapata hasara kubwa sana, ndio maana ni wafanyabiashara wachache sana wanamudu biashara kwa muda mrefu, na wanaomudu ni wale wezi/matapeli. UKIFANAY biashara kwa kufuata mchanganuo niliouweka hapo juu lazima ufilisike, in 2 years.

Sasa wewe unavyosema watu wa Kariakoo wamnauza zaidi ya 38K, HAO TRA kiherehere cha kuweka minimum requirement ya 14M wamekitolea wapi?au wewe una-data zaidi yao? kwa maan hii inabidi waje hadi magengeni kwetu wafunge machine.

SHIDA huyo Mpuuzi wa TRA aliyetembea nchi za wenzetu akaona kila kitu kina electronic receipt akili zake chache, UMEME nchi nzima 20% coverage, umeme unawaka less than 50% of the productive time mwaka mzima, leo hii unamlazimisha mtu ategemee hiki kitu,kweli? kuna mpuuzi hata mmoja wa TRA anayeendesha gari bila kuweka mafuta? sasa wafanyabiashara wakae wategemee dubwana ambalo litahitaji high maintenace(generator) wakati mitaji yenyewe ya milioni 2?
Hujaongelea basic salary vipi? Suala la salary ya TZS 180K halipi kwenye main thread bai mimi ndo nimelileta! Na good enough, post uliyoni-quote wewe ndiyo hiyo ambayo nmezungumzia suala la 180K. So, kutokana na utaratibu basi nawe 180K unayozungumzia itakuwa ndiyo hiyo hiyo ambayo niliizungumzia b4 ndio maana ukafanya quotation ili ujenge yako. Sentensi yangu ilisema: mfanyakazi anayelipwa Sh.180,000/- kwa mwezi, mapato yake ghafi kwa siku ni sh.6000/-...sasa unakataa vipi unaposema hukuzungumza suala la basic salary wakati post uliyo-quote na kuijibu ndivyo inavyosema?

Hoja yako kwamba ikiwa kiwango ni 14M basi idadi ya wafanyabishara iongezwe ni kwamba hujaangalia vigezo vingine. This's not all about annual sales turnover ya 14M bali kun vigezo....mathalani, mfanyabiashara ni lazima awe na phyiscal address ya biashara yake. Lakini vilevile ukumbuke kwamba, kusema wenye turnover ya 14M ndio wanaotakiwa hamaanishi kwamba ndo basi tena kila anayefika hiyo level lazima atumie mashine; hapa tungekuwa tunazungumzia masuala ya price regulation, hiyo 14M tungei-category kama Price Floor! Vilevile, kuweka kiasi cha chini namna hiyo ilikuwa ni namna tu ya kuwabana wafanyabishara. Kwa kawaida, wafanyabiashara huwa hawataji mapato yao halisi ili waweze kukadiriwa kodi stahiki...na hii ndiyo sababu ya yote haya! Ni very common mfanyabishara kukuambia kwamba mauzo yake kwa mwaka ni sh.10million wakati ukilithaminisha duka lake lina-worth millions of t.sh. Sasa, ili kumbana mtu kama huyu ni lazima uweke floor ya chini kabisa coz' hata alisema anauza sh.30K kwa siku wakati anauza sh.100K, bado utamdaka tu kutokana na lowest floor iliyowekwa!

Hoja yako kwamba kv hawalipi VAT basi haina haja ya "kugombana" nao naona hoja yako ime-base kwenye imagination figure na sio realistic. Kusema kwamba wanaohusika ni wale wenye sales turnover ya 14M doesn't necessarily mean kwamba at the end of the year, final figures ndizo hizo ulizoweka wewe! Isitoshe, nimeshaelezea suala la TZS 14M huku nikiendelea kusisitiza kwamba wale ambao kiukweli kabisa hapo ndipo wanapocheza wala hajwajagusa otherwise target isingekuwa wafanyabishara 200K.

Kwamba wafanyabishara wengi wanafilisika hilo ni jambo la kawaida sana duniani na ndio maana wataalamu mbalimbali wa biashara duniani wanakubaliana many businesses fails within one year with many other failing before they start! Vinginevyo, dunia hii ingekuwa na matajiri kila kona coz' watu wengi sana duniani wamewahi kufanya biashara angalau mara moja katika maisha yao hususani kwenye third world countries...ukifanya bishara kwa kumuona NasDaz anafanya bila kufahamu ni namna gani nafanya, you'll always fail...hili ndilo tatizo la wafanyabishara wengi...

Kwamba kihelehele cha TRA ni nini wakati benchmark ni 14M tayari nimeshakueleza why you need to say 14M...kwamba waje basi hadi magengeni jibu ni kwamba hawawzi kuja coz' kigezo si 14M pekee!

Kwamba umeme coverage ni 20%, let me just say kwamba inatia uchungu kwa kweli, even after 50 years of independence! However, am very sorry to say that, that's not condition sufficient enough not to use EFDs. Vijijini siku kuna simu; huko huko wanakochaji simu zao ndiko huko huko wakachaji hizo EFDs...no escapism hapa! But the good side of this stuffs ni kwamba, huko wengine wanakochajia simu zao ndiko huko huko kwa hao wafanyabiashara! Bush kwe2 hakuna umeme, halafu wafanyabiashara wengi wanao-qualify katika ile list halisi ya wafanyabishara 200K; wote ama wana majenereta au wanatumia solar...hata umeme wa solar unachaji mashine hizi; tutafute lingine!

Nimalizie tu kusema kwamba huyo "MPUUZI" wa TRA unamuonea coz' kama wabunge wasingepitisha sheria ya matumizi ya EFDs, basi zisingetumika!

Wasalaamu, tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa...tusitafute visingizio. Timiza wajibu wako ili uwe na uwezo wa kudai haki yako!
 
Watanzania sisi ni watu wa- ajabu, yani wewe unapewa njia rahisi y akitu flani, unaona sifa kwa kuwa serikali imeamua kufuata njia ya kipuuzi inayo-inflate bei. transmission moja ya TRA ya mahesabu ya siku nzima haizidi 64KB,kwa viwango vya sasa vya data, hii si zaidi ya 25MB kwa mwaka. Naamini EATELI na VODAKOM hii bando ya 25MB wanauza around 100-200TZS kwa retail price, kwa maana ya kuwa serikali ingeweza kuuziwa kwa bei ndogo zaidi. sasa wewe gharama za TZS 100 kwa mwaka ziongeze bei hadi 70000K? unaona sifa kujiuzia kidubwasha ambako huko kilichotoka kinauzwa bei chee kisa uliomba customization?kweli?mashine kuwa aghali sio kosa la wafanyabiashara, ni upuuzi wa serikali, dunia ya sasa ya kufuata austerity hakuna atakayekusifia ukinunu EFD printer ya $50 kwa $500. unaonekana ----- mtozeni. siwashangai lakini hawa kwenye procurement hata bei ya mkungu wa ndizi wanaweka laki 1.
Yaani hilo suala la transmission ulivyolizungumzia kirahisi rahisi is like mtu anashuka pale Julius Nyerere International Airport, anachukua simu yake anaweka SIM Card ya MTN South Africa kisha anatuma message huku akiamini kabisa message itatumwa!!
Hakuna mfanya Biashara anyefanya kitu kisichokuwa na manufaa kwake, kama ukikuta kaweka PC dukani kwake, hiyo ni kwa faida yake sio TRA. huna sababu ya kumwambia kwa kuwa umeweza kununua PC basi nunua na AC. Sio kazi yako, kwenye nchi za wenzetu zenye open market unafukuzwa at point blank.[/B]
Inaelekea unaupenda sana huu mtindo wa ku-temper hoja za mtu! Awali nilisema gross 6000/- wewe ukaweka net 6000/-...ama kweli kama ulivyotamka hapo juu; Watanzania ni watu wa ajabu sana!! Hivi huoni kama kuna tofauti kati ya mfanyabisha kununua PC na mfanyabishara kuwa na PC dukani kwa ajili ya risiti na Invoice? Hizo sentensi mbili kwako zina maana moja?! Aisee...! And to be honest, mtu anayesema kwamba hizi mashine hazina faida yoyote kwa mfanyabiashara basi ni dhahiri mtu huyo atakuwa hana uelewa na how SME and financial sectors operate.
 
Yaani hilo suala la transmission ulivyolizungumzia kirahisi rahisi is like mtu anashuka pale Julius Nyerere International Airport, anachukua simu yake anaweka SIM Card ya MTN South Africa kisha anatuma message huku akiamini kabisa message itatumwa!!

You have no idea about how well i understand what i just wrote, to make your life simple, there is no getting around the fact that using Vodacom SIM card in any machine does not increase it's price by 10,000 fold. basi zile nokia Tochi kariakoo zisingeuzwa 50,000

Hakuna kitu special kilichofanyika ndani ya hizo machine, i can configure those ports to communicate with vodacom servers while am half asleep and drunk. that is distributed data networks 101.any one who has ever coded a line of java in tehir life will tel you that. UPUUZI wanaouchaji TRA sio wa kuushabikia.atleast not from me, or anyone with 1% knowledge of such implementation.

Inaelekea unaupenda sana huu mtindo wa ku-temper hoja za mtu! Awali nilisema gross 6000/- wewe ukaweka net 6000/-...ama kweli kama ulivyotamka hapo juu; Watanzania ni watu wa ajabu sana!! Hivi huoni kama kuna tofauti kati ya mfanyabisha kununua PC na mfanyabishara kuwa na PC dukani kwa ajili ya risiti na Invoice? Hizo sentensi mbili kwako zina maana moja?! Aisee...! And to be honest, mtu anayesema kwamba hizi mashine hazina faida yoyote kwa mfanyabiashara basi ni dhahiri mtu huyo atakuwa hana uelewa na how SME and financial sectors operate.

Nimeweka Net ya 6000 kwa sababu nimejenga hoja yangu, kuonesha kuwa kuwa mtu anayelipwa 180,000 kwa mwezi bado anakipato kikubwa.
shida yako ndugu unataka nifikirie kama wewe, hiyo ni ngumu kidogo, kama sio ngumu sana.TUKO tofauti.

kwa kuwa unapenda watu wafate mkumbo, let me catch your wago for just a bit. Mpokea mshara gros ya 180,000 HALIPI PAYE. Kwani Taxable income yake ni 162,000 ambayo inafall chini ya kiwango cha serikali cha kukusanya PAYE. Unajua kwa nini?hata serikali na uroho wake wa kuonea wafanyakazi inamhurumia huyu hohehahe mpokea 180,000.sasa huyu akichukua hii 162,000 anabakia na 5,400 kwa mwezi, bado ni maradufu ya 2,000 anayobaki nayo mfanyakazi. Bado huyu anafaida ya kuwekewa hiyo 18,000*2 kila mwezi na mwajiri wake kama pensheni. Mfanyabiashara hana yote hayo.akitaka kujiunga kwa hiari, hana wa kumuongezea hiyo half anayopata mfanyakazi, na inakula kwenye ile 2,000 kwa siku anayopata.

Either way you spin it 14M a year revenue is nothing to boast about. Ndio maana wabongo wakisikia mtu analipwa $100,000 a year US wanaona huyu jamaa atakuwa tajiri sana, not knowing kuwa,this $100,000 is going to incure over 80$ expenses, leaving this poor broke with just a net of about $2000 a month as a cushion, in a country where insurance costs $1000, and a simple hospital procedures can run you $10,000.

Yakhe faida ya Machine kwa Mfanyabiashara, haiji kwa KUWA TRA wamezichagua. if i were to do SWOT analysis y ahivyo vidubwasha ningevitupa kama optiona ya 100,kati ya option za kumpa faida mfanya biashara.

It all comes down to a simple thing, you do not force how people keep their records in the free market. all you can force them to do is in what format they bring that record to you.HOW they keep it, none of you efn business.
 
Narudia, wewe ni kilaza...nimekuuliza kama gharama zipi coz' kila unapotoa gharama fulani; unabaki na kitu fulani na ndio maana hata huko kwenye profit kuna profit b4 and after tax depending umetoa gharama ipi na ipi...na kukuonesha ulivyo kilaza wala hufahamu TRA reference yao ni nini...wao reference yao ni annual sales turnover...but in addition to that, acha tabia za kichoko jukwaani...huna sababu za kila wakati kurudia rudia "we wa 'versity" huo ni ushamba. Au kimekuchoma sana kusema nimepiga namba hadi 'versity? we wa wapi wewe?

Kumbe unajijua wewe ni choko halafu unataka kusingizia wengine? Hizo namba ulizopiga hadi 'versity' ndio zipi wewe? Hesabu nilizokuwa nazungumza hapa zinahusu kujumlisha na kutoa tu, nazo zimekushinda bado unajigamba na economics uchwara za 'versity'. Umethibitisha ukilaza wako vya kutosha, walioona wameona. Endelea kupiga 'namba hadi versity', sisi huku tunaendelea na maisha. Waziri Mkuu umemsikia?
 
Yakhe, kama ukitazama nilichoandika utaona kwamba nimeongelea mtu anayepata Net pay ya 180,000. Sijaongea Basic pay ya 180,000.

Hoja yangu iko simple ndugu, kama TRA mnatambua kuwa 14M annual sales ni duka l amaharage na mchele, basi ongezeni kiwango cha wafanyabiashar awanaohitaji kutumia hizi mashine.

RUDI KASOME nilichoandika. DO NOT skim it.

ukijadili hoja usirukie kwenye conclusion kama haujaelewa kilichosemwa na mtoa hoja.

Pili: kama hawa wa 14M hawatozwi VAT, then hakuna haja ya kugombana sana na hawa watu, incentive ya kukusanya mapato kutoka kwa hawa watu haileti maana ya kibiashara. mtu mwenye sales turnover ya 14M inamaana ana gross profit before operational expenses ya around 1.4-2M kwa mwaka, ukiondoa gharama za uendeshaji wa Biashara,gross profit inakuwa si zaidi ya 200,000. sasa hii ndio TRA wanatakiwa wachukue asilimia zao kwa mwaka. huyu mtu faida yake(net profit) haiwezi kuzidi 100K kwa mwaka, HUYU mtu huwezi kumunulisha mashine ya laki 6. UNAMUONEA.

Mshukuru mungu wafanya biashara wengi wanafanya BIASHARA za mazoea, lakini wengi wanapata hasara kubwa sana, ndio maana ni wafanyabiashara wachache sana wanamudu biashara kwa muda mrefu, na wanaomudu ni wale wezi/matapeli. UKIFANAY biashara kwa kufuata mchanganuo niliouweka hapo juu lazima ufilisike, in 2 years.

Sasa wewe unavyosema watu wa Kariakoo wamnauza zaidi ya 38K, HAO TRA kiherehere cha kuweka minimum requirement ya 14M wamekitolea wapi?au wewe una-data zaidi yao? kwa maan hii inabidi waje hadi magengeni kwetu wafunge machine.

SHIDA huyo Mpuuzi wa TRA aliyetembea nchi za wenzetu akaona kila kitu kina electronic receipt akili zake chache, UMEME nchi nzima 20% coverage, umeme unawaka less than 50% of the productive time mwaka mzima, leo hii unamlazimisha mtu ategemee hiki kitu,kweli? kuna mpuuzi hata mmoja wa TRA anayeendesha gari bila kuweka mafuta? sasa wafanyabiashara wakae wategemee dubwana ambalo litahitaji high maintenace(generator) wakati mitaji yenyewe ya milioni 2?

Asante ndugu yangu. Hawa akina TRA NasDaz na wenzie wanapaswa waje warudie kusoma hii post yako kisha wasome tena iliyoanzisha thread, ndiyo hoja hasa wanayoikwepa. Kinachoudhi zaidi ni kuwa wanakwepa hoja halafu wanaleta majibu ya kuudhi na wakati mwingine matusi kabisa.

Lakini nashukuru mheshimiwa Waziri Mkuu amelisikia hili na ametoa agizo jana. Kwa maelekezo yale ya mheshimiwa PM jana, kuna matumaini.
 
Last edited by a moderator:
Kwa uwezo wangu sihitaji kujuwa yote hayo uliyoandika. Ninachoamini ni kwamba, ulipoanzisha biashara ulijiandaa. Ukatafuta nyumba au chumba au sehemu, ukaweka grill, ukatengeneza fremu, n.k. Hiyo ndo sehemu ya mtaji. Sikushauri ununue EFD kwa kutumia faida yako. Hiyo utaipata baadaye. Sasa hapoTRA wanasema nunua na EFD machine unakataa.

Kwa nini unakataa? Gharama zote ulikubali lakini EFD hutaki, kwa nini?

Wafanyabiashara wengi wa tz elimu ni tatizo na kadri unavyoshuka chini, elimu pia ni down. Kwao faida ni kukwepa TRA. TRA nao elimu kuunga unga tu. Hili limekuwa kundi kubwa linalohongana pesa na kuelekezana kukwepa kodi kila siku.

Nunueni EFD, lipeni kodi. Hao watu wa serikali wanaobugia kodi zetu, tutapambana nao mbeleni.

EFD haipaswi kuwa gharama ya mfanyabiashara maana himsaidii kazi, inasaidia kazi ya TRA ambao wana bajeti tayari kutoka kwenye kodi wanazokusanya kwetu. Kuniambia niwanunulie EFD ni sawa na kusema pia tuwanunulie magari na vitendea kazi vingine, hiyo ni dhuluma na wizi wa mchana. EFD haimuongezei tija mfanyabiashara bali inawarahisishia TRA kazi, kwa hiyo ni jukumu la TRA kugharamia hizo EFD, vinginevyo ni WIZI MTUPU.
 
Back
Top Bottom