kwa biashara ya kawaida mauzo ya 38,000 sio mapato. These are sales not gross revenues. Mtu aliyeuza 38,000 amenunua hiyo bidhaa ili aiuze. kwa mahesabu ya kuinunua kwa kuiuza kwa faida ya asilimia 10, basi huyu bwana amenunua mzigo kwa dealer/distributor/wholesaler kwa 34,000 yeye anauza 38,000. mapato ya huyu bwana kwa siku ni 4,000 tu!!
kama kweli hii ndio cutoff ya TRA waache hawa jamaa walalamike, mfanaybiashara mwenye mapato ya 4,000/= kwa siku bado ni mtu wa kipato cha chini sana. Kwa nini? hii 4,000 inaitwa gross revenue. kwa maana kuwa baadae ataondoa gharama za umeme/kodi za pango la eneo la biashara etc/ Net revenue ya huyu bwana haiwezi kuzidi 2,000 kwa siku.
Hii anarudi nayo nyumbani, huko sasa anakutana na matumizi ya kila siku ambayo hata mfanyakazi anakuwa nayo. na yeye anatakiwa anunue umeme nyumbani, anunue maji, anunue chakula, watoto waende shule.huyu mtu kama hajaiba basi atafilisika baada ya kipindi kifupi, kwani atakuwa anakula kamtaji kadogo alikonako bila yeye kujua.
Tukirudi kwa wafanyakazi wanaolalamia PAYE, naomba niseme kuwa hii wanayokatwa wao mwisho wasiku wanapewa NET PAY. hii wanarudi nayo nyumbani.wakiwa makazini kwao, hawalipi kodi ya ofisini, hawalipii umeme ofisini, hawalipii hata hela ya mlinzi. Mapato ya mfanyakazi anayepata net pay ya 180,000 kwa mwezi ni zaidi ya mapato ya mfanya biashar aanayeuza 14M kwa mwaka. Hili liko wazi kwa yeyote ambaye hesabu hazimpigi chenga.kwani Mfanyabiashara kabla hajaenda nyumbani ana net income ya 2,000. mfanyakazi ana net income ya 6,000. ni zaidi ya mara tatu.
na wanaosema laki 600,000 kwa mwaka ni pesa kidogo, kun amtu yoyote anayelipwa 180,000 anayetumia laki 6 kununua kitu asichokihitaji na kisichomuongezea kipato chake kwa namna yoyote?
Serikali iongeze cuttoff point ya hayo mapato ya mwaka. Serikali ibuni njia mpya za kukusanya mapato. tumewasema wanategemea sigara na pombe basi wameona wahamie kwenye kukusanya kodi za watu ambao kodi zenyewe hazikusanyiki.tunarudi kulekule kwenye mambo ya kodi ya kichwa. wagawe hizo machine bure, wawaelimishe wafanyabiashara, kama zinafaida kwao, nina uhakika watazichukua.
TRA wanaona wafanyabiashara ni wezi kwa kuwa wao ni majambazi nambari wani, hivyo si ajabu.bahati mbaya hii mbinu yao haitaongeza mapato.waiobereshe.