TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

petroli.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, alibainisha hayo jana mkoani Dar es Salaam, akitafsiri kwamba ni hali inayoiweka nchi katika hali ya hatari endapo hatua zinazokwenda kuchukuliwa hazitafanikiwa.

“Hivi karibuni kumekuwa na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi. Kwa sasa hivi mafuta yaliyopo ndani ya nchi yanatosha kwa siku 15 tu. ikitokea chochote kama meli haitakuja ndani ya wiki mbili, nchi itakuwa haina mafuta. Hii siyo nzuri kwa usalama wa nchi,” alisema.

Dk. Mataragio alikuwa anazungumza wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uelewa kwenye eneo la miradi ya kimkakati ya mafuta na gesi.

Alisema kumekuwa na ongezeko la bei na serikali ikaamua kufanya uchunguzi kujua sababu za bei kupanda, huku akifafanua hatua za dharura za sasa ni kwamba TPDC imeshaagiza mafuta ambayo yanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote.

"Kwenye soko la dunia mafuta yanashuka lakini huku kwetu bei inapanda. Hata yakishuka, hatuoni unafuu, mwaka huu mafuta yalishuka sana bei yakaenda mpaka sifuri lakini sisi bado bei ipo juu," alisema.

Dk. Mataragio alisema ushiriki wa TPDC kwa sasa utasaidia bei ya mafuta isipande kwa sababu wao watakuwa wanayanunua moja kwa moja bila kuwa na njia za mkato.

"Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari, nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari, wanachukua mafuta kutoka hapa, tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Zambia," alisema.

Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Mkongo wa Juu TPDC, Gaston Canuty, alisema shirika hilo lipo katika mikakati yake ya kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini na limeanzisha mchakato wa kumpata mbia watakayeshirikiana naye kuagiza mafuta.

Mhandisi Aristides Katto kutoka TPDC, akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye vituo vya kuuzia magari, alisema tangu shirika lianzishwe mwaka 2004, takribani asilimia 60 ya umeme katika gridi ya taifa unatokana na gesi.

“Nyumba zaidi ya 600 zimeunganishiwa gesi, magari zaidi ya 600 makubwa na madogo yameunganishiwa gesi na mengi ambayo yameunganishiwa ni zinazofanya biashara ya UBA na BOLT.

"Futi za ujazo bilioni 596 ndizo zilizotumika hadi mwezi Juni mwaka huu. Kati yake, viwandani ni asilimia 19.1303, umeme asilimia 80.8479, taasisi, magari na nyumbani asilimia 0.0218,” alibainisha.

Katto alisema tangu shirika hilo lilipoanza hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, nchi imeokoa dola za marekani bilioni 17.07 (sawa na trilioni 39.1) ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje ya nchi.

Vilevile, alisema kampuni binafsi 10 zimepewa ruhusa ya kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari na moja tayari imeshakamilisha kujenga kituo eneo la TAZARA.

Kuhusu kituo cha gesi kwa mabasi ya mwendokasi, alisema wanatarajia kufungua zabuni ya kutangaza hilo leo na mkandarasi atakayepatikana atakijenga

Gazeti la Nipashe
Jinsi kauli ilivyotolewa inaweza kusababisha taharuki kwenye jamii, watu wakaanza kuhifadhi mafuta majumbani na hata kuweza kusababisha majanga ya moto. Kwani upungufu huo umegundulika leo tu ambapo kabla ya hapo wahusika waliamini mafuta yatatosha kwa muda mrefu zaidi? Pamoja na hayo, siku 15 ni nyingi kwa wahusika kuweza kuchukua hatua za tahadhari badala ya kutia wananchi wasiwasi. Badala ya mhusika kutangaza kama alivyofanya, ingebidi awe ameishatafuta suluhu ya tatizo na baadaye ndiyo anawatangazia umma kwamba kuna tatizo hili na tumefanya kadha wa kadha kukabiliana na taizo hilo.
 
TPDC inatafuta Wadau ili wasaidiane kuagiza mafuta? Mbona huku ni kurudi nyuma ya maamuzi ya kulifanya Shirika hili liagize mafuta lenyewe na kupunguza gharama za mafuta kwa mlaji wa mwisho. Hapo lazima kuna jambo, si bure.
 
Aaagh, kwanini siku zote walikuwa hawaagizi na kuweka akiba?, ili pakitokea upungufu ndio wayaingize sokoni. Wawe na reserve kama za NFRA, ili kustabilize soko panapotokea uhaba
 
wafuasi wa Chadema kama kawaida yao na tabia zao za kigaidi za kutaka nchi iwe ktk taharuki na shida,
muda wote wao wanataka habari mbaya ziikumbe Tanzania.
kweli nimeamini wafuasi wa mboe wana chembe chembe za kihalifu.

ukiwafuatilia wafuasi wa mboe utagundua mara zote kunapokuwa na tatizo kama nchi basi huwa wao wana shangilia sana.
hawa watu ni hatari sana, mwaka 2025 hawafai hata kupata kiti kimoja cha ubunge.
 
Wewe utakuwa mwalimu
Yes, mtu yeyote yule mwenye ujuzi, maarifa na taaluma ya mambo mtambuka jina sahihi la kumwita ni Mwl, kwa sababu anakuelimisha.

Acha nyeeer nyeeeee na mihemuko. Sema usikike upatiwe jibu toshelezi.

Ujue mimi baba yako we bwana mdogo
 
wafuasi wa Chadema kama kawaida yao na tabia zao za kigaidi za kutaka nchi iwe ktk taharuki na shida,
muda wote wao wanataka habari mbaya ziikumbe Tanzania.
kweli nimeamini wafuasi wa mboe wana chembe chembe za kihalifu.

ukiwafuatilia wafuasi wa mboe utagundua mara zote kunapokuwa na tatizo kama nchi basi huwa wao wana shangilia sana.
hawa watu ni hatari sana, mwaka 2025 hawafai hata kupata kiti kimoja cha ubunge.
Kwani mkurugenzi wa tpdc alietoa hizi taarifa ni mwana CHADEMA?
 
Sometimes hauna haja ya kuongea ila muda wenyewe utaongea na yanazidi kutokea, kuna mwana siasa mmoja alisema "acha legacy yake ijitetee ",sijui alizani Legacy ni mtu au mzimu wa Magu akasahau Muda utaongea.
Watu badala ya kufanya kazi wanahangaika kuharibu na kuonesha Hayati hajafanya chochote! Hata mradi wa umeme wanataka kuubaribu?! Kweli watu wana roho mbaya kiasi hiki? Unawaathiri Watanzania wote ili ionekane adui yako hajafanya chochote! Inasikitisha sana
 
Yes, mtu yeyote yule mwenye ujuzi, maarifa na taaluma ya mambo mtambuka jina sahihi la kumwita ni Mwl, kwa sababu anakuelimisha.

Acha nyeeer nyeeeee na mihemuko. Sema usikike upatiwe jibu toshelezi.

Ujue mimi baba yako we bwana mdogo
Aisee namanga-kitonga umenifurahisha sana umeona wadau wanakosea sana umeanza kusahihisha yani
😂😂😂
 
Ila mafuta ulikuwa unapata, vp sasa hivi uwazi upo? Je mafuta yapo ya uhakika?,so impact ya kukosekana kwa mafuta ina ambatana na upandaji wa gharama za maisha, sasa bora kipi uwazi bila mafuta au uficho na mafuta ya kutosha.
Kwahiyo kipindi cha mwendazake maisha yalikuwa rahisi?
 
HIi ni man-made/organized chaos, nahisi kunawatu wana test mitambo
 
HIi ni man-made/organized chaos, nahisi kunawatu wana test mitambo
 
Aisee namanga-kitonga umenifurahisha sana umeona wadau wanakosea sana umeanza kusahihisha yani
. Sisi wahenga ni vyema tukawapa mawaidha hawa bwana wadogo wapate walau ufahamu.

Wanaandika kama wanakimbizwa. Wakienda intaviu baada ya kuandika barua wanakuwa hawaeleweki kuanzia barua yenyewe hadi intaviu.

Wakikosa kazi wanaanza lawama kama kahaba anavyomlaumu mteja wake kumkojolesha (hawapendi kukojoleshwa aslani).

Acha watuite walimu,ndio maana alikuwepo Great/Legend Teacher Hon. Julius K. Nyerere.
 
Back
Top Bottom