Tanzania kuwa kituo kikuu cha mafuta Afrika Mashariki

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Derick Mosha amesema TPDC inatarajia kupeleka gesi katika nchi za Kenya, Uganda na Zambia na pia kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia mafuta ili Tanzania iwe kituo kikuu cha mafuta kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

1689884261910.png
Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ulioandaliwa kwa ushirikiano na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Aidha serikali kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) linakusudia kuhakikisha usafiri wote umma zikiwemo daladala, bajaji, bodaboda pamoja na mabasi na malori yanatumia gesi asilia badala ya mafuta ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Ili kufanikisha hilo TPDC inatarajia kujenga vituo vya kutosha vya kujaza gesi ambapo kituo kikuu kitajengwa eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam ujenzi ambao utachukua miezi nane kukamilika.
 
Back
Top Bottom