Unajua water Table tuseme kama ni milkshake kwenye bilauri, kila mtu ananyonya kwa mrija sasa kama mmoja badala ya mrija anatumia bomba kunyonya utaona kwamba anaweza kuwamalizia wengine.
Kwa ushauri wangu watu waanze kuvuna maji ya mvua na kuweka kwenye matenki, itapunguza mafuriko na watu kuwasukumizia maji kutoka katika eneo lao na wao kujipatia fresh water kwa matumizi
Aisee kazi kubwa sana.Hivi unafikiri water table ni kama karai kuuubwa hivyo Dar au Nchi ipo juu ya karai moja lenye maji? hebu karudie tena kusoma
Wazo la kuvuna maji ya mvua ni zuri hata hivyo kwa miji iliyo bize sana kwa magari na viwanda.
Watu wanataka kumuangushia "Mama" kila jumba bovu🤸🤣To make it clear, izi too hazikuanzishwa ktk awamu ya 6 ....... 🤣🤣🤣
Nimekupata hata hivyo;Aisee kazi kubwa sana....
Nani kasema ni karai moja ? hata kama yapo makarai milioni moja yanatumia na watu wanne wanne mmoja kuvuta sana kwa matumizi makubwa impact yake ni kwa wengine na lazima ujue mito (rivers) na chemichemi zinatoka huko kwenye water table...., kwahio kwa kuweka cost ya kisima ni wewe kuchangia matumizi ya hio public property sababu hata kama kisima kipo kwako yale maji unavyonza huenda na jirani yako nyumba ya kumi angevyonza yale yale au ndio yanayotiririka kwenye mto fulani kule bondeni
🤣🤣🤣 Hawakawiii hawaaa Maana na jina wamempa Wana muita mamaa wa mitozo, sasa nikaona niwakumbushe mapemaaaaaaaWatu wanataka kumuangushia "Mama" kila jumba bovu🤸🤣
Naam sasa tumeanza kuongea lugha moja; Hakuna watu waliokuwa wanatumia maji vizuri kama wazee wetu yaani kwenye mito, Juu kabisa watu wanachota maji ya kunywa baada ya hapo kuoshea vyombo alafu kwa chini kuonga alafu kufua alafu mifugo kwa mbele kabisa huku yakiendelea kwenye safari yake mpaka ziwani... (hilo halina tatizo)Nimekupata hata hivyo;
Inamaana maji yakitoka kwenye public ( mto) jirani au mtu yeyote anatumia bure kabisa, achote, afulie afugie kabwawa ka samani na pengine ka bustani hapo sio tatizo;
ILA mtu akiyatoa ( akichimba) kwa gharama na kufanya matumizi pengine nusu ya hayo tayari imekuwa tatizo
Kwa mawazo yangu kumaliza tatizo la maji TANZANIA tusipobadilika na kulinda/kuhuisha vyanzo vya maji , tatizo litakuwa la milele....kwani ni sawa na kuziba nyufa tano zinatokea nyingine mpya tanoNaam sasa tumeanza kuongea lugha moja; Hakuna watu waliokuwa wanatumia maji vizuri kama wazee wetu yaani kwenye mito..., Juu kabisa watu wanachota maji ya kunywa baada ya hapo kuoshea vyombo alafu kwa chini kuonga alafu kufua alafu mifugo kwa mbele kabisa huku yakiendelea kwenye safari yake mpaka ziwani... (hilo halina tatizo)
Tatizo linaanza kwenye kuchepua ili amwagilizie je uchepuaji wake unaleta madhara kwa wengine ? Kama anafuga samaki na maji yanapita huenda isiwe mbaya sana sababu anayatumia na yanaendelea na safari ingawa kuna hatari hao samaki wakatoroka au kupelekea magonjwa ya samaki wake kuuguza samaki wa ziwani....
Kwahio all in all haya mambo ni kuyatumia kwa manufaa yako na ya jamii na kuangalia kama matumizi yako yana impact kwa wengine... Point yangu kuu ilikuwa sio sababu tu umeyachimba ukaona kwamba uchimbaji wako hauna impact kwa wengine..., Ndio maana nikasema kama inawezekana uvunaji wa mvua na kuweka kwenye matenki yako ni muhimu zaidi sababu tumeondoa ile natural sponge ya kuhifadhi maji (ardhi, bustani n.k.) na kuweka pavements kila mahali hivyo natural storage imepungua (hii neema ya mvua inakuwa karaha kwa mitaro kujaa na watu kusukumiziana maji yanayokusanywa na mapaa ya nyumba zao
Hizi tozo za visima zilianzishwa tangu mwaka 2009 ila huwa hazitekelezwi.To make it clear, izi too hazikuanzishwa ktk awamu ya 6
kwa uapatikanaji wa Maji hapa nyumbani unavyo sua sua, wangefutilia mbali tu hizo kodi kwa wanao chimba maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wabakiwe na wale wanaochimba kwa ajili ya biashara kwani Sio kila kodi ya Ulaya tucopyHizi tozo za visima zilianzishwa tangu mwaka 2009 ila huwa hazitekelezwi.
Mwaka fulani enzi za Jiwe, Kitila Mkumbo akiwa katibu mkuu wizara ya maji, alitaka kuzitekeleza, naye akahairisha sijui!
Sasa, huwa ni kwa nini sheria zinatungwa mpaka zinatungiwa kanuni ila hazitekelezwi? Kama hazitekelezeki si ni bora kuzifuta kuliko kukaa kimya na kuviziana?!
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app