BoT angalie hizi lipa namba za mitandao ya Simu zinaumiza wananchi

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,129
2,982
Mfumo jumuishi wa kifedha ni jambo zuri katika kukua uchumi wa nchi na matumizi ya mifumo rasmi ya kifedha.

Kuruhusiwa mitandao ya simu kutoa huduma za kifedha ilikuwa ni nia njema ya BoT kuongeza watumiaji katika mfumo jumuishi wa kifedha.

Lakini kwa sasa imegeuka kuwa kichaka cha kukusanya fedha kutoka wa wananchi huku yakipewa majina tofauti.

Tumelia sana kuhusu tozo zile zilizowekwa na serikali. Achilia mbali gharama za kutoa fedha na kutuma fedha. Bila kujali parameters zingine, bado ni gharama kubwa sana maana hzi sio huduma za mara moja tu. Ni endelevu kwa kila mwenye simu lazima atajikuta katika matumizi ya fedha kupitia simu.

Limekuja hili sasa la lipa namba. Binasfi, pamoja na kuwa na changamoto na Tigo hadi kufikia kuachana na laini yao, lakini wanaonekana kuwa walau na nafuu kwa kulinganisha na voda.

Nimeuweka uzi huu, BoT isaidie kuyabana haya makampuni yote ya simu, maana mteja kuamua kuweka hela katika simu ni faida kwa hizi kampuni ambazo hatuzichaj gharama yeyote ya kuweka fedha zetu.

Kwa mfano ukilipa 40,000 tigo kwa tigo ni 1,000
Lipa kwa voda -voda kiasi hiko ni 1,200

Sasa balaa uki cross mtandao, kwa kiasi hiko ukitumia tigo kwa lipa namba ya voda ni 2,350..

Hizi ni gharama kubwa sana kwa watumiaji wasiopenda kubeba cash kufanya malipo.

Benki kuu ya Tanzania iingilie kati na kulazimisha haya makapuni kuwa na gharama ndogo bila ya kujali unatumia mtandao gani.
 
Back
Top Bottom