Tozo za visima hazina uhalisia - mtazamo wangu

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,512
4,128
Nilikuwa nasoma jarida moja nikaona kuwa mtu akichimba kisima kwa ajili ya matumizi yake ya nyumbani anatakiwa kulipia kodi ya shs 8,300 kwa mwezi.

Wakati huo huo matumizi ya kawaida ya nyumbani kwa maji ya Dawasco hulipia kati ya 4000 na 10,000 hivi.
kwa namna nyingine ni kama vile watu wanalazimishwa wasichimbe visima badala yake walipie maji Dawasco (ambayo yameonekana kuwa pungufu)

Najua Dar inaweza kuwa na visima vidogo vidogo kwa mamia hata hivyo ni ukweli usiofichika kuwa, wenye hivyo visima wengi wao hawana uwezo wa kulipa hiyo tozo kwa sababu kwa utafiti wangu usio kuwa rasmi; wengi wanavyo visima kwa ajili ya matumizi ya usafi (kwani vingi vina chumvi) na pia waanao mfumo wa dawasco kwa ajili ya matumizi mengine

Pendekezo langu:
Kwa kuwa kisima amechimba mtu kwa gharama zake, analipia umeme kwa gharama zake, na ni kwa matumizi yake mwenyewe; kwa nini Serikali isiweke tozo rafiki kama shs elf mbili au tatu kwa mwezi na ilipwe kwa simu kuepuka usumbufu wa kukusanya?

Kwa wale wenye elimu ya biashara, soko linakoelekea ni kuwa na kodi rafiki/inayo endana na bidhaa, na mfumo rahisi kabisa wa kuikusanya tofauti na mfumo wa zamani uliokuwa unalenga watu wachache kodi kubwa ambapo gharama za kuikusanya zinazidi kodi yenyewe

MWISHO: NATAMANI MAJI KWA MATUMIZI YA NYUMBANI YAWE NI HUDUMA NA SIO MRADI WA KUKUSANYA MAPATO
 
Unajua water Table tuseme kama ni milkshake kwenye bilauri, kila mtu ananyonya kwa mrija sasa kama mmoja badala ya mrija anatumia bomba kunyonya utaona kwamba anaweza kuwamalizia wengine.

Kwa ushauri wangu watu waanze kuvuna maji ya mvua na kuweka kwenye matenki, itapunguza mafuriko na watu kuwasukumizia maji kutoka katika eneo lao na wao kujipatia fresh water kwa matumizi
 
Hivi unafikiri water table ni kama karai kuuubwa hivyo Dar au Nchi ipo juu ya karai moja lenye maji? Hebu karudie tena kusoma
Wazo la kuvuna maji ya mvua ni zuri hata hivyo kwa miji iliyo bize sana kwa magari na viwanda.
 
Nchi yangu Tanzania ilikuaje ad uruhusu kuvalishwa juba na skirt oooh Tanzania.

Amani iwe nanyi.
 
Hivi unafikiri water table ni kama karai kuuubwa hivyo Dar au Nchi ipo juu ya karai moja lenye maji? hebu karudie tena kusoma
Wazo la kuvuna maji ya mvua ni zuri hata hivyo kwa miji iliyo bize sana kwa magari na viwanda.
Aisee kazi kubwa sana.

Nani kasema ni karai moja ? hata kama yapo makarai milioni moja yanatumia na watu wanne wanne mmoja kuvuta sana kwa matumizi makubwa impact yake ni kwa wengine na lazima ujue mito (rivers) na chemichemi zinatoka huko kwenye water table, kwahio kwa kuweka cost ya kisima ni wewe kuchangia matumizi ya hio public property sababu hata kama kisima kipo kwako yale maji unavyonza huenda na jirani yako nyumba ya kumi angevyonza yale yale au ndio yanayotiririka kwenye mto fulani kule bondeni
 
Aisee kazi kubwa sana....

Nani kasema ni karai moja ? hata kama yapo makarai milioni moja yanatumia na watu wanne wanne mmoja kuvuta sana kwa matumizi makubwa impact yake ni kwa wengine na lazima ujue mito (rivers) na chemichemi zinatoka huko kwenye water table...., kwahio kwa kuweka cost ya kisima ni wewe kuchangia matumizi ya hio public property sababu hata kama kisima kipo kwako yale maji unavyonza huenda na jirani yako nyumba ya kumi angevyonza yale yale au ndio yanayotiririka kwenye mto fulani kule bondeni
Nimekupata hata hivyo;

Inamaana maji yakitoka kwenye public ( mto) jirani au mtu yeyote anatumia bure kabisa, achote, afulie afugie kabwawa ka samani na pengine ka bustani hapo sio tatizo;

ILA mtu akiyatoa (akichimba) kwa gharama na kufanya matumizi pengine nusu ya hayo tayari imekuwa tatizo

Mimi sijakataa tozo, ila nimeshauri iwe rafiki na ilipike kwa urahisi; kodi ikiwa kubwa mwisho gharama za ukusanyaji zinakuwa kubwa kuliko kodi yenyewe.

Iweje tozo iwe kubwa kuliko ya Dawasco ambayo, imeajiri mamia ya wafanyakazi , magari, magenerator nk?

Kama wanabisha tozo sio kubwa walete data hapa wanakusanya kiasi gani unaweza kuta ni 12% na hapo ni baada ya kuzungusha magari na watu wakifuatilia ina maana karibia hela yote imeshia huko

Ni mtazamo wangu!
 
Watu wanataka kumuangushia "Mama" kila jumba bovu🤸🤣
🤣🤣🤣 Hawakawiii hawaaa Maana na jina wamempa Wana muita mamaa wa mitozo, sasa nikaona niwakumbushe mapemaaaaaaa

Watakavyo jadili vyovyote vila ila wakumbuke izi too hazikuanzishwa na awamu ya 6

Japo ni hoja, kwa Maana Kuna kitu kinaitwa payment for eco system services kwa kuwa Hawa wenye visima Wana vuna maji ambayo ni huduma ya asili Basi ni vyema kulipia.
 
Nimekupata hata hivyo;
Inamaana maji yakitoka kwenye public ( mto) jirani au mtu yeyote anatumia bure kabisa, achote, afulie afugie kabwawa ka samani na pengine ka bustani hapo sio tatizo;
ILA mtu akiyatoa ( akichimba) kwa gharama na kufanya matumizi pengine nusu ya hayo tayari imekuwa tatizo
Naam sasa tumeanza kuongea lugha moja; Hakuna watu waliokuwa wanatumia maji vizuri kama wazee wetu yaani kwenye mito, Juu kabisa watu wanachota maji ya kunywa baada ya hapo kuoshea vyombo alafu kwa chini kuonga alafu kufua alafu mifugo kwa mbele kabisa huku yakiendelea kwenye safari yake mpaka ziwani... (hilo halina tatizo)

Tatizo linaanza kwenye kuchepua ili amwagilizie je uchepuaji wake unaleta madhara kwa wengine ? Kama anafuga samaki na maji yanapita huenda isiwe mbaya sana sababu anayatumia na yanaendelea na safari ingawa kuna hatari hao samaki wakatoroka au kupelekea magonjwa ya samaki wake kuuguza samaki wa ziwani.

Kwahio all in all haya mambo ni kuyatumia kwa manufaa yako na ya jamii na kuangalia kama matumizi yako yana impact kwa wengine... Point yangu kuu ilikuwa sio sababu tu umeyachimba ukaona kwamba uchimbaji wako hauna impact kwa wengine..., Ndio maana nikasema kama inawezekana uvunaji wa mvua na kuweka kwenye matenki yako ni muhimu zaidi sababu tumeondoa ile natural sponge ya kuhifadhi maji (ardhi, bustani n.k.) na kuweka pavements kila mahali hivyo natural storage imepungua (hii neema ya mvua inakuwa karaha kwa mitaro kujaa na watu kusukumiziana maji yanayokusanywa na mapaa ya nyumba zao
 
"serikali ni kikundi cha wajanja/wahuni wachache waliojimilikisha rasmali na wa watu wote ndani ya eneo fulani la kiutawa yaani nchi. Watu hawa humnyonya sana mwananchi kiasi cha kumfanya alipie hata vile vilivoletwa na Mungu/Nature-wanawalipisha kodi kwa vitu visivyo na ulazima wa kulipishwa kodi.

Mbaya zaidi watu hawa hujilimbikizia mali hizo huku wao wenyewe wamejiwekee misamaha ya kodi hadi kwenye mishahara yao, viwanda na mashamba" Profesa mmoja mwenye PhD ya heshima alisikika huko Costa Rica
 
Naam sasa tumeanza kuongea lugha moja; Hakuna watu waliokuwa wanatumia maji vizuri kama wazee wetu yaani kwenye mito..., Juu kabisa watu wanachota maji ya kunywa baada ya hapo kuoshea vyombo alafu kwa chini kuonga alafu kufua alafu mifugo kwa mbele kabisa huku yakiendelea kwenye safari yake mpaka ziwani... (hilo halina tatizo)

Tatizo linaanza kwenye kuchepua ili amwagilizie je uchepuaji wake unaleta madhara kwa wengine ? Kama anafuga samaki na maji yanapita huenda isiwe mbaya sana sababu anayatumia na yanaendelea na safari ingawa kuna hatari hao samaki wakatoroka au kupelekea magonjwa ya samaki wake kuuguza samaki wa ziwani....

Kwahio all in all haya mambo ni kuyatumia kwa manufaa yako na ya jamii na kuangalia kama matumizi yako yana impact kwa wengine... Point yangu kuu ilikuwa sio sababu tu umeyachimba ukaona kwamba uchimbaji wako hauna impact kwa wengine..., Ndio maana nikasema kama inawezekana uvunaji wa mvua na kuweka kwenye matenki yako ni muhimu zaidi sababu tumeondoa ile natural sponge ya kuhifadhi maji (ardhi, bustani n.k.) na kuweka pavements kila mahali hivyo natural storage imepungua (hii neema ya mvua inakuwa karaha kwa mitaro kujaa na watu kusukumiziana maji yanayokusanywa na mapaa ya nyumba zao
Kwa mawazo yangu kumaliza tatizo la maji TANZANIA tusipobadilika na kulinda/kuhuisha vyanzo vya maji , tatizo litakuwa la milele....kwani ni sawa na kuziba nyufa tano zinatokea nyingine mpya tano
Naaanisha; Chemchem zinakauka kwa mamia kila mwaka sababu zinafahamika na hakuna mtu anaye jali wala kuchukua hatua za kimkakati hadi itokee zima moto....
Kungeanzishwa kampeni ya wilaya/tarafa/kata/vijiji/vitongoji vyote kupanda miti maalum ya maji maeneo yote yenye chemchem au yaliyokuwa na chemchem ndani ya miaka 10 iliyopita na kusimamiwa kikamilifu; hii kero yote ya maji mbona ingebakia historia na hivyo uchimbaji wa visima ungebakia kwa watu wachache.
Hivi kuna mtu ana enjoy kuchimba kisima kwa mamilioni ya pesa na pengine kupata maji yenye Chumvi?
 
To make it clear, izi too hazikuanzishwa ktk awamu ya 6
Hizi tozo za visima zilianzishwa tangu mwaka 2009 ila huwa hazitekelezwi.

Mwaka fulani enzi za Jiwe, Kitila Mkumbo akiwa katibu mkuu wizara ya maji, alitaka kuzitekeleza, naye akahairisha sijui!

Sasa, huwa ni kwa nini sheria zinatungwa mpaka zinatungiwa kanuni ila hazitekelezwi? Kama hazitekelezeki si ni bora kuzifuta kuliko kukaa kimya na kuviziana?!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
kwa uapatikanaji wa Maji hapa nyumbani unavyo sua sua, wangefutilia mbali tu hizo kodi kwa wanao chimba maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wabakiwe na wale wanaochimba kwa ajili ya biashara kwani Sio kila kodi ya Ulaya tucopy
Tunaweza kuwa na kodi zingine tofauti kulingana na mazingira yetu...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom