Nchi haina maji, wananchi msichimbe visima Bila vibali, ukichimba maji usiuze Bila leseni

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,119
Nchi yetu ina mambo yanakusikitisha Shana yanayofanywa na watoa maamuzi

Kwanza, tunakubaliana wote kwamba maeneo mengi hayana maji Ila chini ya ardhi kuna maji ambayo wenye fedha wanaweza kuchimba visima.

Pili, tunakubaliana wazi kwamba serikali inazo sheria zinazowakataza wananchi kuchimba visima Bila kibali cha mamlaka ya maji ya eneo husika.

Tatu, tunakubaliana wote kwamba gharama za kuchimba kisima hazina ruzuku ya serikali na maji yakipatikana yanatumiwa na watu wengi kukuza uchumi WA familia.

NNE. Tunakubaliana wote kwamba pamoja na serikali kutochangia chochote kwenye uchimbaji WA kisima ukianza kuuza maji hakuna mtumishi WA mamlaka ya maji anayesubiri urudishe gharama za uwekezaji wako wanaanza kukutoza kodi

Tano, tunakubaliana wote kwamba mitambo ya kuchimba visima NI ghali.

Sita, tunakubaliana wote kwamba serikali inao uwezo wakuondoa Kodi kwenye mashine za kuchimba visima vijijini na kuwapa incentives wachimbaji WA visima ikiwemo kubariki usambazaji maji wawekezaji waweze kurejesha gharama uwekezaji.

Saba, naomba tukubaliane kwamba nchi haina tatizo la maji Bali ina tatizo la ufikiri wa watoa maamuzi. Saudia wanatengeneza mvua Tanzania tunakataa kutumika Kwa maji yaliyopo maeneo yetu

Fikra za kirasimu, fikra za Tozo na Kodi, fikra za kutegemea wazungu zinatunyima maji.

Niwatakie maji mema mnaonielewa
 
Yes wameona hakuna namna ya kuwanyonya Basi wanaweka sheria. Ni sawa niwe na mitambi yangu niwe na uwezo wa kuwauzia umeme wananchi wote wa hapa magadrisho USA river bado wataweka Sheria ili wapate namna ya unyonyaji wa kunyonya mnyonge
 
Back
Top Bottom