Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer (mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.

Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya.
 
Uchimbaji wa maji wakati flani ni bahati nasibu. Wanaweza kupima maji na wakaona kuna maji.

Lakini wakati wa kuchimba wanaeeza kuyafikia lakini wasiweze kuyapandisha juu...wanadai yamekimbilia kwenye miamba.

Kazi kwetu tulipoteza 20m, maji yalichimbwa vizuri, wakayafikia, wakati wa kuyasafisha na wafitishe mabomba, hayakuweza kupanda juu.

Hasara hii tuliibeba kwasababu tulitumia wapimaji tofauti na wachimbaji.

PIli...wanadai mafuta mengi yanatumika kwa siku katika kuchimba wastani wa 500k/siku.

Tatu...gharama za mabomba kununuana ..kufitisha
 
Kazi ya uchimbaji visima imejaa udalali mkubwa wa kupindukia, ukitaka kuchimbiwa kisima kwa bei ambayo ni rahisi na halali bila ya kuwepo mtu wa katikati hakikisha unachimbiwa na kampuni ya mwenye mashine au unafanya biashara noja kwa moja na mmiliki wa mashine ya uchimbaji.
 
Kazi ya uchimbaji visima imejaa udalali mkubwa wa kupindukia, ukitaka kuchimbiwa kisima kwa bei ambayo ni rahisi na halali bila ya kuwepo mtu wa katikati hakikisha unachimbiwa na kampuni ya mwenye mashine au unafanya biashara noja kwa moja na mmiliki wa mashine ya uchimbaji.
Sahihi
Nilichimba Kisima Kutumia Mmiliki Wa Gari Mwenyewe
Gharama Ikawa Tofauti Na Niliowakuta Ofisini Ambao Nao Ni Madalali
 
Nishapitia changamoto Kama iyo,
Nilichogundua hizo Bei Ni upigaji TU.

Tatzo la dar,Udalali mwing Sana
Kampuni nyng za visima hapa dar Zina mawinga wengi Sana, inayopelekea Bei kua juu mno, kila winga ana shea Yake.

Tumia kampuni za visima zinazofanya kazi zao mikoani, Bei zao huwa chini Sana na kazi zao huwa Ni uhakika Sana.

Nmechimba visima 2 Hapa hapa dar (mita 35,kingine mita 48).
Hakuna Hata kimoja kilichozidi mil 5 kwa kila kitu, na vyote vinatoa maji mwaka mzima uhakika bila kukauka isipokua kimoja maji yake Yana chumvi.

Na wanatoa warranty ya miaka 2 Kisha kuna bima ya matengenezo, service zote unawapigia wanakuja kufanya kazi endapo kisima kikisumbua.

Option ambazo kwa kampuni nyng za dar, kuzipata Ni ndoto mno
 
Back
Top Bottom