Tozo za visima hazina uhalisia - mtazamo wangu

Nilikuwa nasoma jarida moja nikaona kuwa mtu akichimba kisima kwa ajili ya matumizi yake ya nyumbani anatakiwa kulipia kodi ya shs 8,300 kwa mwezi.

Wakati huo huo matumizi ya kawaida ya nyumbani kwa maji ya Dawasco hulipia kati ya 4000 na 10,000 hivi.
kwa namna nyingine ni kama vile watu wanalazimishwa wasichimbe visima badala yake walipie maji Dawasco (ambayo yameonekana kuwa pungufu)

Najua Dar inaweza kuwa na visima vidogo vidogo kwa mamia hata hivyo ni ukweli usiofichika kuwa, wenye hivyo visima wengi wao hawana uwezo wa kulipa hiyo tozo kwa sababu kwa utafiti wangu usio kuwa rasmi; wengi wanavyo visima kwa ajili ya matumizi ya usafi (kwani vingi vina chumvi) na pia waanao mfumo wa dawasco kwa ajili ya matumizi mengine

Pendekezo langu:
Kwa kuwa kisima amechimba mtu kwa gharama zake, analipia umeme kwa gharama zake, na ni kwa matumizi yake mwenyewe; kwa nini Serikali isiweke tozo rafiki kama shs elf mbili au tatu kwa mwezi na ilipwe kwa simu kuepuka usumbufu wa kukusanya?

Kwa wale wenye elimu ya biashara, soko linakoelekea ni kuwa na kodi rafiki/inayo endana na bidhaa, na mfumo rahisi kabisa wa kuikusanya tofauti na mfumo wa zamani uliokuwa unalenga watu wachache kodi kubwa ambapo gharama za kuikusanya zinazidi kodi yenyewe

MWISHO: NATAMANI MAJI KWA MATUMIZI YA NYUMBANI YAWE NI HUDUMA NA SIO MRADI WA KUKUSANYA MAPATO
serikali imeshindwa kunisogezea maji, nimetumia hela ya jasho langu kuchimba kisima, mfano cha 6m, siuzi yale maji, nimenunua pump inayotumia umeme wa tanesco, Serikali inapata wapi justification kuja kunidai pesa ya kodi ya maji tena, au mimi sijaelewa?
 
Back
Top Bottom