TPA: Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari kuanza kutekelezwa leo Julai 1, 2026 katika bandari zote za Bahari Kuu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,173
Reaction score
15,458
TAARIFA KWA UMMA..jpg
TAARIFA KWA UMMA. (1).jpg
UTEKELEZAJI WA ADA YA UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI

Jumatano, 01 Julai 2026

DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inapenda kuujulisha Umma kuwa mnamo tarehe 1 Julai 2026, ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (Port Infrustructure Development Fee -PID) itaanza kutekelezwa rasmi katika bandari zote za Bahari Kuu.

Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (PID) itatozwa kwa mizigo yote ya ndani itakayoingizwa kwa kupitia Bandari za bahari kuu, isipokuwa mizigo ya vimiminika (Liquid Bulk Cargo).

Aidha Ada hii imegawanywa katika makundi mawili kama ifuatavyo:-

a. Asilimia 4.5% ya kodi kwa mizigo yote ya ndani itakayoagizwa kwa kupitia Bandari za Bahari kuu.

b. Asilimia 1.5% kwa ajili ya malighafi ya viwandani pamoja na mizigo yote isiyotozwa Ushuru wa Forodha (Import Duty).

TPA inatoa shukrani kwa wadau wote kwa ushirikiano wao endelevu na inasisitiza kuwa utekelezaji wa Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (PID) unalenga kuimarisha miundombinu na kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa katika Bandari za Bahari Kuu nchini.

TPA pia inapenda kusisitiza kuwa, taarifa rasmi zinazohusu utendaji wa bandari, takwimu za shughuli za bandari, changamoto, maboresho na mipango ya maendeleo hutolewa na TPA kupitia njia rasmi za mawasiliano ambazo ni pamoja na Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo ghorofa ya 6 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre).

Njia nyingine za mawasiliano ni pamoja na simu ya bure: 0800-110032, Barua pepe: customercare@ports.go.tz, Tovuti: www.ports.go.tz, Mitandao ya kijamii: Instagram, X (Twitter) na Facebook kwa jina @tpa_tz.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
 
Hii nchi inahitaji overhaul kubwa sana maana maCCm yameshindwa kabisa kuongoza. Hapa tutarajie ongezeko la bidhaa zinazoingia kupitia Bandari Kuu, hamna namna.
 
HUyo DP yeye ni kukusanya hela tu?
 
Kodi nyingine hazitoshi kuendeleza hiyo miundombinu?
 
Mpaka sasa bado nawaza kazi ya DP WORLD kwa sababu kama mwekezaji hamna anachofanya zaid ya kuongeza gharama kwa wananchi.
Serikali inawekeza ili yeye achukue mapato bila kutoa hata senti yake.
Najiuliza huu uwekezaji ni wa aina gani?
 
Hata tozo kwenye lulu imeongezeka tena kimya kimya na kuwa 1500
 
UTEKELEZAJI WA ADA YA UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI

Jumatano, 01 Julai 2026

DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inapenda kuujulisha Umma kuwa mnamo tarehe 1 Julai 2026, ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (Port Infrustructure Development Fee -PID) itaanza kutekelezwa rasmi katika bandari zote za Bahari Kuu.

Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (PID) itatozwa kwa mizigo yote ya ndani itakayoingizwa kwa kupitia Bandari za bahari kuu, isipokuwa mizigo ya vimiminika (Liquid Bulk Cargo).

Aidha Ada hii imegawanywa katika makundi mawili kama ifuatavyo:-

a. Asilimia 4.5% ya kodi kwa mizigo yote ya ndani itakayoagizwa kwa kupitia Bandari za Bahari kuu.

b. Asilimia 1.5% kwa ajili ya malighafi ya viwandani pamoja na mizigo yote isiyotozwa Ushuru wa Forodha (Import Duty).

TPA inatoa shukrani kwa wadau wote kwa ushirikiano wao endelevu na inasisitiza kuwa utekelezaji wa Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (PID) unalenga kuimarisha miundombinu na kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa katika Bandari za Bahari Kuu nchini.

TPA pia inapenda kusisitiza kuwa, taarifa rasmi zinazohusu utendaji wa bandari, takwimu za shughuli za bandari, changamoto, maboresho na mipango ya maendeleo hutolewa na TPA kupitia njia rasmi za mawasiliano ambazo ni pamoja na Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo ghorofa ya 6 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre).

Njia nyingine za mawasiliano ni pamoja na simu ya bure: 0800-110032, Barua pepe: customercare@ports.go.tz, Tovuti: www.ports.go.tz, Mitandao ya kijamii: Instagram, X (Twitter) na Facebook kwa jina @tpa_tz.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
Kwa hio kumbe Waarabu wa DP World Hawana pesa kama tulivyoaminishwa na MAFISIEMU
 
Duh sasa izo tozo za mizigo za awali zinafanyiwa nini kama sio zitumike kuboresha iyo miundombinu daaaaa
 
WALE WAPUMBAVU WALIOKUWA WANASIFU UUZWAJI WA BANDARI ZETU KWA DP WORLD HII KODI HAIWAHUSU?UPUMBAVU KABISA.KILA SIKU KUONGDZA KODI TU
 
Back
Top Bottom