Mhhh!! basi tuanze na hiyo avatar yako, naomba uweke ya Mswahili utoe hiyo ya Hugo Chavez. Waswahili muache unafiki wenu huu na mkubali mna mapungufu. Kutumia Kingereza kina umuhimu wake tena pakubwa na haimanishi kwa anayekitumia kwamba hana uzalendo. Kama nilivyosema hapo awali, sisi Wakenya tunaenzi lugha zetu za asili na huwa tunaziongea kama Kikikuyu, Kijaluo n.k. halafu pia tunatumia lugha za kuletwa kama Kiswahili, Kingereza na kadhalika.
Kingereza tunakipenda kwa ajili ya umuhimu wake kwa biashara za kimataifa
- Akaja Mghana, Mnigeria, Mzibambwe, Msouth n.k. sitaumiza kichwa jinsi ya kuwasiliana naye, tunaongea tu kama watu tuliojuana zamani, tunapiga deals bila kuhangaika jinsi ya kuwasiliana.
- Utafiti wa Kisayansi umedhihirisha kwamba kwa kujifunza lugha zaidi haswa Kingereza, kuna manufaa mengi ikiwemo uwezo wa fikira pevu, soma huu hapa
http://eacea.ec.europa.eu/llp/studi...ualism_to_creativity/compendium_part_1_en.pdf
- Kingereza kina utajiri wa maneno, haswa kwa wataalamu, ukiandika ripoti au kufanya utafiti, maneno yapo ya kila aina.
Yaani orodha ni ndefu, nikiamua kuandika manufaa yote hapa. Kuna Watanzania wengi wanaolijua hili na wamewaweka watoto wao kusomea Kenya au kwenye international schools za Bongo zenye walimu kutokea Kenya na Uganda, wakati walala hoi wamejaza watoto wao kwenye shule za saint Kayumba, huku wakidanganywa kuwa huo ndio uzalendo.
Kiswahili mimi nakiongea sana, lakini nakipenda tu kama ninavyopenda lugha zote zingine. Na huwa najifunza lugha nyingi sana, nikiwa Bongo huwa najifunza kuongea Kinyakyusa, Kichaga, Kipare na Kihaya ila inakua ngumu maana Watanzania wengi hawapendi kujifunza lugha zao za asili eti huo ni ushamba. Halafu nikiwa Kenya huwa najifunza Kiluhya (mke wangu Mluhya), Kikamba, Kijaluo, Kinandi n.k. Halafu lugha yangu ya sili Kikikuyu huwa naipenda sana na nikienda kijijini huwa najumuika na jamaa kwa kilugha. Mjini nikiingia kwenye biashara na kazi yangu, basi Kingereza nakipa kipaumbele ikifuatiwa na Kiswahili.