Ndugu nina swali dogo sana kwako kama hizo nchi ulizoziorodhesha na kuziita ,,english speaking countries" sasa, Je, ni kwanini Wakenya, Waganda & Co. wakienda kusoma Marekani wanatakiwa kufanya mtihani wa Lugha ya Kiingereza TOEFL ambao kirefu chake yake ni test of english as Foreign Language? Kwa maana kama wangekuwa ni English speakers maana yake ni kwamba wasingehitaji kufanya huo Mtihani, hivyo naomba uniambie ni kwanini lazima wafanye huo Mtihani?
haha,
Sio TOEFL tu hata Uingereza wana requirement ya IELTS, na kama kawaida Kenya ipo kwenye nchi zisizozungumza kingereza kama lugha ya kwanza.
Take an Exam | British Council
Wakenya wakitaka kuja UK Kusoma lazima wapitie
hapa.Halafu mwembwe nyengine ndio zinafuata, sasa huyu kikuyu anataka danganya watu kuwa Kenya Kiingereza ni lugha ya kwanza. Yani anachokiongea ni sawa na kusema Ujerumani kiingereza ni lugha ya kwanza, kwa kuwa wajerumani wengi wanaongea kiingereza ukikutana nao barabarani. Hata soni hana.
Wakenya wanataka kuaminisha watu(Tanzania) kuwa lugha yao ya kwanza ni kiingereza kwa kuwa hawana kitu chengine cha kulinganisha/kutofautisha. Wanaoamini hizi propaganda za kipuuzi ni wale wasiowahi kuitembea dunia na wasiojua kuwa kwenye lugha ya kiingereza kuna wazungumzaji wa asili (waingereza,wamarekani ,n.k) na wazungumzaji wengine, kwenye hili kundi, Tanzania, Kenya, Ujerumani, Malaysia, China n.k wote tuko kundi moja.
Uwezo wa kuongea lugha ya kiingereza kwenye hili kundi la pili haupimwi kwa kutazama utaifa wa mtu, bali uwezo wake binafsi kupitia mitihani ya kiingereza kama IELTS na TOEFL. Ukiona mtu anakuletea hadithi za mimi mkenya hivyo naongea kiingereza kukuzidi, jua huyo hakuna kitu.ni porojo tu.Kama ni kampuni au ofisi, mwambieni awaletee matokeo yake ya IELTS ili muyachambue.
http://www.ielts.org/institutions/test_format_and_results/ielts_band_scores.aspx
Uwezo wa kungea lugha haupimwi kwa mbwembwe, bali kwa matokeo ya mtihani wenye vigezo na vipimo mahususi.
Mfano,
http://www.ielts.org/researchers/analysis-of-test-data/test-taker-performance-2012.aspx
Ukichambua taarifa za mwaka 2012, utagundua kuwa Ingawa wajerumani hawafahamiki kama nchi yenye kuongea Kiingereza, matokeo yao ya IELTS kwa wastani yako juu (7.2) kuliko Kenya, Kinchi kinachotupigia kelele kutwa kucha humu kuwa lugha yao ya kwanza ni kiingereza, hawa vizibo matokeo yao, wastani ni (6.8).
Sasa ukitumia tafsiri ya IELTS wenyewe huu ni wastani wa "Competent user" yaani mtumiaji anayejitahidi, kwa maana halisi.
The IELTS 9-band scale
Each band corresponds to a level of English competence. All parts of the test and the Overall Band Score can be reported in whole and half bands, eg 6.5, 7.0, 7.5, 8.0.
Band 9: Expert user: has fully operational command of the language: appropriate, accurate and fluent with complete understanding.
Band 8: Very good user: has fully operational command of the language with only occasional unsystematic inaccuracies and inappropriacies. Misunderstandings may occur in unfamiliar situations. Handles complex detailed argumentation well.
Band 7: Good user: has operational command of the language, though with occasional inaccuracies, inappropriacies and misunderstandings in some situations. Generally handles complex language well and understands detailed reasoning.
Band 6: Competent user: has generally effective command of the language despite some inaccuracies, inappropriacies and misunderstandings. Can use and understand fairly complex language, particularly in familiar situations.
Band 5: Modest user: has partial command of the language, coping with overall meaning in most situations, though is likely to make many mistakes. Should be able to handle basic communication in own field.
Kumbuka kuwa asilimia kubwa ya wafanya mtihani huo wanaangukia hapo kwenye kundi la "Band 6". Ambako huko ndani kuna kina Italia, Ufaransa, Naijeria,Urusi, Taiwani,n.k, sasa hebu niambie umeshawahi kumsikia mtaiwani au mrusi akijiita muongea kiingereza kama lugha ya kwanza??jibu ni Hakuna.
Hawa ndugu zetu wa Kenya wana matatizo makubwa sana.Yani walichowafanya waingereza itachukua miaka mingi sana kujitambua, na kuacha tabia za kujipendekeza, na kujikweza.
Natumai ukitokea mzozo wa kuwa Kenya ni nchi inayozungumza kiingereza, mtapitia hili bandiko kuwakumbusha hawa ndugu zetu kuwa, kwa kuwa watanzania tumekaa kimya haimaanishi kuwa ni hatujui ujanja ujanja wanaoutumia kuishi mjini.