Binafsi nashauri aangalie swala la watendaji hasa wakuu wa idara namna wanavyopatikana.Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
Kumekuwa na undugu sana katika jambo hili. Watoto wa maskini wanakaimishwa miaka nenda rudi bila marupu rupu wala kifuta jasho afu unakuta mtu ana ndugu yake pale utumushi au tamisemi basi analetwa na kuthibitishwa fasta..
Kimsingi hii imekuwa haina tija sana kwa taasisi za umma.
Nakumbuka Mh Rais alisititiza kuwa mtu ateuliwe kwa utendaji wake wa kazi pamoja na nidham yake katika kazi.
Pili Mh aangalie utofauti wa mishahara kati ya watumushi wa mashirika ya umma, watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu.
Mwisho. Mh aangalie aina mpya ya ulaji wa watumishi wa umma. Unakuta mradi wa milioni 78. Unafuatiliwa eti na wakaguzi kutoka mfano..CAG, TAMISEM, PPRA, WIZARA YA FEDHA, RAS, PCCB. na ikumbukwe hao wote wana approach tofauti tofauti.gharama za mafuta, matengenezo ya magar. Wengine night siku 10, wengine 7, wengine watahitaji fedha kidogo ili wasiandike hoja, yan vurugu ni nyingi hasa huko halmashauri. Mwisho wa siku gharama ya ufuatiliaji ni M 156 na gharama za mradi ni M 78. Jumla ya gharama za usimamizi na mradi ni M200+.
Nadhan ifikie wakat dhan ya value for money iwe isiwe ya maneno..iwe katika vitendo.