Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JamiiForums

Official Robot
Nov 9, 2006
6,064
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,670
2,000
Awakate mishahara hadi 50% tujenge mareli,mabandari,maeapoti,mastigilaz goji nk. Tuwanyooshe hawa watumishi wanaiponda ccm.
 
omari londo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
1,812
2,000
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
Ajiuzulu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stable

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
234
500

Binafsi nashauri aangalie swala la watendaji hasa wakuu wa idara namna wanavyopatikana.
Kumekuwa na undugu sana katika jambo hili. Watoto wa maskini wanakaimishwa miaka nenda rudi bila marupu rupu wala kifuta jasho afu unakuta mtu ana ndugu yake pale utumushi au tamisemi basi analetwa na kuthibitishwa fasta..
Kimsingi hii imekuwa haina tija sana kwa taasisi za umma.
Nakumbuka Mh Rais alisititiza kuwa mtu ateuliwe kwa utendaji wake wa kazi pamoja na nidham yake katika kazi.

Pili Mh aangalie utofauti wa mishahara kati ya watumushi wa mashirika ya umma, watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu.

Mwisho. Mh aangalie aina mpya ya ulaji wa watumishi wa umma. Unakuta mradi wa milioni 78. Unafuatiliwa eti na wakaguzi kutoka mfano..CAG, TAMISEM, PPRA, WIZARA YA FEDHA, RAS, PCCB. na ikumbukwe hao wote wana approach tofauti tofauti.gharama za mafuta, matengenezo ya magar. Wengine night siku 10, wengine 7, wengine watahitaji fedha kidogo ili wasiandike hoja, yan vurugu ni nyingi hasa huko halmashauri. Mwisho wa siku gharama ya ufuatiliaji ni M 156 na gharama za mradi ni M 78. Jumla ya gharama za usimamizi na mradi ni M200+.

Nadhan ifikie wakat dhan ya value for money iwe isiwe ya maneno..iwe katika vitendo.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
29,080
2,000
Arudishe ule Ukali wake Na kufoka foka wa 2015-2016
Sio kwamba hataki bali pumzi imekata. Wakati ule alikuwa na mihemko ya madaraka na aliamini ataifanya Tz kuwa nchi tajiri, alifikia mpaka mahali akawa anasema mwisho wa sisi kuvaa mitumba ni 2019 kisha tutawapelekea wazungu. Ila saa hii anaona umebaki mwaka mmoja hakuna linalomdhibitishia kwamba anaweza shinda kura kihalali bila kuiba, huku akiwa hakopesheki na kwenye misaada alishalikoroga.
 
busara kwanza

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
241
250
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
Watumishi wa umma ndio engine ya serikali ya kuwapelekea maendeleo wananchi lakini mkulu amewapuuza,anawadharau amewanyima haki zao,wamezalilishwa bila kufuata utaratibu na watumishi kwa kuwa wanajua bila wao mambo hayaendi sawa sawa wameamua kukaa pembeni na kutulia kimya ndo maana mambo hayaendi poa kama ukitazama nje ya box na kama vp afute tu mishahara yenyewe ili awafurahishe wananchi mambumbu na wanyonge wanayoyasubiri maendeleo kwa hamu kiukwel kila kitu kwenye awamu hii hakitokamilika kama akiendelea kuiburuza engine hii kwa ushaur wa mm kwenye hiyo mei mos yao akawakejeli,awatishe,awatukane apendavyo ili ss wanyonge tupate maendeleo
 
busara kwanza

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
241
250
Binafsi nashauri aangalie swala la watendaji hasa wakuu wa idara namna wanavyopatikana.
Kumekuwa na undugu sana katika jambo hili. Watoto wa maskini wanakaimishwa miaka nenda rudi bila marupu rupu wala kifuta jasho afu unakuta mtu ana ndugu yake pale utumushi au tamisemi basi analetwa na kuthibitishwa fasta..
Kimsingi hii imekuwa haina tija sana kwa taasisi za umma.
Nakumbuka Mh Rais alisititiza kuwa mtu ateuliwe kwa utendaji wake wa kazi pamoja na nidham yake katika kazi.

Pili Mh aangalie utofauti wa mishahara kati ya watumushi wa mashirika ya umma, watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu.

Mwisho. Mh aangalie aina mpya ya ulaji wa watumishi wa umma. Unakuta mradi wa milioni 78. Unafuatiliwa eti na wakaguzi kutoka mfano..CAG, TAMISEM, PPRA, WIZARA YA FEDHA, RAS, PCCB. na ikumbukwe hao wote wana appriach tofauti tofauti.gharama za mafuta, matengenezo ya magar. Wengine night siku 10, wengine 7, wengine watahitaji kidogo eti wasiandike hoja, yan vurugu ni nyingi hasa huko halmashauri.

Nadhan ifikie wakat dhan ya value for money iwe isiwe ya maneno..iwe katika vitendo.
Unayempa ushauri huo nani ndugu yangu huyuhuyu baba wa ubaguzi,chuki,kukomoa n.k?
 
shebination

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
375
1,000
Kama ninavyowashauri kila siku naomba awaeleze wajiajiri kwenye shughuli nyingine Za kiuchumi wasitegemee mishahara pekee mbona wengine Hatuna mishahara tunalima bustani na mambo yanaenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,192
2,000
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
Maumivu tu
tapatalk_1553924402704.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stable

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
234
500
Unayempa ushauri huo nani ndugu yangu huyuhuyu baba wa ubaguzi,chuki,kukomoa n.k?
Mkuu anaweza akachukua mazuri kama ameyaona. Lakini pia ujumbe huu unaenda mbali zaidi hata kwa hao wenye mamlaka za uteuzi.
Wananyanyasa sana hawa watumishi wasio kuwa na wakuwatetea.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,487
2,000
Asirekebishe chochote. Aendelee tu kuwanyima watumishi wa umma haki zao za msingi na mwisho wa malipo ya hiyo dhuluma ataipata hapa hapa duniani. Yeye hawezi kujua maisha wanayopitia wafanyakazi wa nchi hii kwa sababu halipi kodi, kila kitu anafanyiwa; kiufupi yupo peponi. Siku zote aliyeshiba hawezi kumjua mwenye njaa.
 
stable

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
234
500
Aje na hoja ya salary standardization

Ni aibu sana yaani wote mmesoma masters ya education lakini mkija kwenye malipo ya kazi unakata tamaa.

Alieajiriwa Udsm kwa Mfano, ataanza na 2.4Milioni, alieajiliwa Chuo cha Ualimu likely wanaweza kufika 1.3Milion. Njoo kwa Walimu wa kawaida unaweza kupewa increment 2 ambazo hazivuki hata elfu 70000/=.

Sasa hapo nashindwaga hata kushangaa masters ukiwa chuoni sheria na utaratibu za kudahili ni zilezile, vigezo vya kuwa awarded hiyo masters ni hivyo hivyo na ajira unapangiwa na mwajiri wako hujipangii maana kama ni hivyo ningechagua kwenye green pasture.

Hii huwa inatukatisha tamaa sana na wakati mwingine hata ukirudi kazini na masters yako no body cares.

Mi nadhani ikiwekwa mishahara kwa kuangalia academic merits itasaidia hata usipopata cheo ambavyo ni vigumu kuvipata utalipwa unachostaili.

Ndio tupo tunakodoa macho na hiyo salary standardization likely inaweza kuondoa hii tofauti. Academic merits kiwe kigezo cha kwanza kulipwa mishahara na katu isiwe vyeo au kada mtu anayoifanyia kazi. Maana vyeo kuna watu wamo kwenye nafasi fulani by chance hata kada pia ndugu ulishatuathiri hapo nyuma.

Ila kusoma ni kujiendeleza na effort binafsi ambazo zinahitaji uwezo wako upstairs na kujitoa kuacha mambo mengine uboreshe career yako. Kwenye ualimu mambo hayapo hivyo hii kada inahitaji jicho la ziada
Sio ualimu tu ndugu yangu..hata sekta nyingine hii kitu imeshamiri.
Pia ile dhana ya kusema eti degree ya kwanza ndio kila kitu, nadhan serikali ibadilishe muundo au mtazamo na ianze kutambua degree ya pili na hata ya tatu katika utendaji wa kazi. Nadhanii hii itahamasisha watumishi wengi kujiendeleza kinasomo.

Eti unakuta mtu ana degree ya pili, bado kimshahara ni kile kile.. dah inakatisha tamaa sana
 
MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
578
1,000
Kujenga nchi yataka moyo. Namshauri rais wetu mpendwa kutokuongeza hata senti moja kwa watumishi mpaka mikoa yote iunganishwe kwa rami na vijiji vyote nchini vipate umeme wa REA. Baaba ya hayo sasa ruksa kuongeza mishahara na marupurupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkwala

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
1,002
2,000
Binafsi nashauri aangalie swala la watendaji hasa wakuu wa idara namna wanavyopatikana.
Kumekuwa na undugu sana katika jambo hili. Watoto wa maskini wanakaimishwa miaka nenda rudi bila marupu rupu wala kifuta jasho afu unakuta mtu ana ndugu yake pale utumushi au tamisemi basi analetwa na kuthibitishwa fasta..
Kimsingi hii imekuwa haina tija sana kwa taasisi za umma.
Nakumbuka Mh Rais alisititiza kuwa mtu ateuliwe kwa utendaji wake wa kazi pamoja na nidham yake katika kazi.

Pili Mh aangalie utofauti wa mishahara kati ya watumushi wa mashirika ya umma, watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu.

Mwisho. Mh aangalie aina mpya ya ulaji wa watumishi wa umma. Unakuta mradi wa milioni 78. Unafuatiliwa eti na wakaguzi kutoka mfano..CAG, TAMISEM, PPRA, WIZARA YA FEDHA, RAS, PCCB. na ikumbukwe hao wote wana approach tofauti tofauti.gharama za mafuta, matengenezo ya magar. Wengine night siku 10, wengine 7, wengine watahitaji fedha kidogo ili wasiandike hoja, yan vurugu ni nyingi hasa huko halmashauri. Mwisho wa siku gharama ya ufuatiliaji ni M 156 na gharama za mradi ni M 78. Jumla ya gharama za usimamizi na mradi ni M200+.

Nadhan ifikie wakat dhan ya value for money iwe isiwe ya maneno..iwe katika vitendo.
Unakaimu miaka mingi,mwisho wa siku analetwa mtu kutoka kusiko julikana anakabidhiwa madaraka na stahiki zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
9,200
2,000
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
Aondoke
 
stable

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
234
500
Unakaimu miaka mingi,mwisho wa siku analetwa mtu kutoka kusiko julikana anakabidhiwa madaraka na stahiki zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kumbuka huyo mtu uwezo wake unakuwa mdogo, hivyo unajikuta kazi zile zile unaendelea kufanya...
Yeye hajui hata aanzie wapi na aishie wapi!! Dah inauma sana. Wanyonge wanaumizwa sana katika ofisi za umma.
Mh Rais anavyosemaga wanyonge pengine afike mbali hata kwa watumishi wa chini ambao hawana wa kuwasemea.
Yan haiwezekan mtu anakaimishwa miaka zaidi ya mwaka afu analetewa tena mtu kukaimu nafasi ile ile. Why??

Na sheria inasema mtu anatakiwa kukaimu kwa miezi sita tu...kama hafai basi wafanye haraka kuleta mtu kujaza nafasi hiyo, na siyo kusubiri mwaka au miaka kupita.
 
Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
14,950
2,000
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
We jamaa unataka aanze tena mambo ya uhakiki Mie nataka atie Mpunga wa kutosha kuliko hata ule aliowekeza kwenye SGR na Dreamliner au Stieglier gorge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom