Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...


JamiiForums

JamiiForums

Official Robot
Joined
Nov 9, 2006
Messages
5,105
Points
2,000
JamiiForums

JamiiForums

Official Robot
Joined Nov 9, 2006
5,105 2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
 
Super Sub Steve

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
13,591
Points
2,000
Super Sub Steve

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2011
13,591 2,000
Zimesalia siku 30 kabla ya maadhimisho ya mei mosi 2019, Je, Mheshimiwa Rais ambaye ndiye mgeni Rasmi wa Maadhimisho, unapendekeza atatue kero IPI ili kuifanya mei mosi 2019 ya kipekee na yenye maana kwa watumishi wa umma kuelekea uchumi wa viwanda?. Toa maoni yako na wahusika watamfikishia. Mimi kwa upande wangu nashauri amuagize CAG kukagua payroll za Taasisi za umma ili kubainisha Viwango vya mishahara kama vinaendana na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi na majukumu dhidi ya mishahara yao na kama wenye vyeo Fulani wanavistahili au LA, tukianza na maafisa Elimu nchi nzima, aafisa kilimo, wakurugenzi na wakuu was wilaya, makatibu tawala n.k na uwajibikaji wao ukilinganisha na maslahi manono wayapatayo
We jamaa unataka aanze tena mambo ya uhakiki Mie nataka atie Mpunga wa kutosha kuliko hata ule aliowekeza kwenye SGR na Dreamliner au Stieglier gorge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwisho2016

mwisho2016

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2016
Messages
532
Points
500
mwisho2016

mwisho2016

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2016
532 500
Traffic barabarani wanavyopendelea, je Rais hajui? Wanavuta magari ya watu wengine njia moja. Kwa kweli inaumiza Sana.

Viongozi wanashindwa kuelewa humu barabarani Kuna magari yamebeba matatizo mengi, akizuia magar akisimamisha eti tu amvute mtu anayemjua, sio ubinadamu.

Junction ya ubungo is going tighten next few months. Those guys knows how to not cause jam, traffic kwa nn hamuwaachii watu wa flay over watumie mbinu..njia zao
 
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
17,487
Points
2,000
Age
76
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
17,487 2,000
Acha kushusha hadhi ya rais. Unataka awe anaongoza magari yeye badala ya trafiki.

Ujinga upo kwa trafiki.
 
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
1,928
Points
2,000
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
1,928 2,000
Hao traffic wanasimamiwa na nani ? Wanafuatiliwa na nani kwenye majukumu yao .
 
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
17,487
Points
2,000
Age
76
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
17,487 2,000
Amekuuliza wewe mkuu, Rais anavyombo vingi mtandao mkubwa, kuliko hata huyo anayeongoza..Hii KERO barabarani raia wanainyamazia tu
Pumbavu kweli.

Mnataka hata suala la uongozaji wa magari liongelewe na rais.

Wapuuzi nyie.
 
C

chapwa24

Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
8
Points
45
C

chapwa24

Member
Joined Apr 10, 2019
8 45
Nasikia Magufuli atakuwa Mbeya Meimosi mwaka huu, tunaomba shughulikia chuo cha utumishi Mbeya ili wanafunzi na waalimu waishi kwa haki. kwa ufupi, matatizo yafuatayo ndio uozo katika chuo hicho, hili lipo wazi kwa watu wote waliowahi kupitia chuo hicho.

1. Waalimu wanavujisha mitihani sana kwa wanafunzi, hasa wa kike. Kuna wanafunzi tunawajua kabisa hawana akili, wanafaulu kwasababu wanafanya ngono na waalimu, waziwazi. Mwanafunzi yeyote akiulizwa hili anajua, kwa wale wasio na mahusiano na waalimu ambao hawataki kupewa matokeo ya chupi, waende wapi sasa? wapigania haki za binadamu pia ingilieni hili.

2. Waalimu wanafanya ngono na wanafunzi wa kike hadi wanagombaniana. Hakuna maadili

3. Futilia mbali waalimu wabovu na wa kuazima, hawakisaidii chuo.

4. Mkuu wa chuo hana nguvu wala maamuzi dhidi ya waalimu au wanafunzi. hadi wanafunzi tunajua ugumvi wa kimapenzi kati ya waalimu kugombania mabinti wa kike na kuvujisha mitihani lakini hakuna hatua zinachukuliwa.
 
D

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Messages
1,376
Points
2,000
D

Daisam

JF-Expert Member
Joined May 23, 2016
1,376 2,000
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri anayehusika. TANESCO ni moja kati ya MAJANGA makubwa kabisa ya kitaifa. Jambo dogo tu la kutumia dakika chache tu kulitatua unaweza ukafuatilia TANESCO hata zaidi ya majuma kadhaa.
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuwasaidia watanznia wa kipato cha chini katika eneo hili, naomba nchi yetu iwe na Mashirika ya usambazaji umeme zaidi ya mawili.
Hiyo itakuwa ni dawa pekee itakayowakomboa watanzania wengi kutoka katika Janga kuu hili la TANESCO.
Kutoka Makambako, Njombe.
 

Forum statistics

Threads 1,285,040
Members 494,423
Posts 30,848,041
Top