Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, Feb 13, 2016.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Feb 13, 2016
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,103
  Likes Received: 2,290
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JamiiForums,

  Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

  Karibuni sana.

  MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

  Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
   
 2. u

  ugalila JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2016
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 652
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....

  Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2016
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 14,098
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Kuna wafanyakazi wa TANROADS wanakuwa na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya Msata - Bagamoyo mida ya usiku, wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.

  Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.

  Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi.

  utaifakwanza
   
 4. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2016
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  asante sana mkuu. Hili kusema kweli ni jipu uchungu. Mamlaka inayohusika imesikia na wasipochukua hatua nao watatumbuliwa. Hapa kazi tu
   
 5. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2016
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,534
  Likes Received: 1,223
  Trophy Points: 280
  Njia ya Msata-Bagamoyo sehemu gani exactly mkuu!? Pia ukiweza hata utuwekee namba za hiyo gari hapa. Ahsante sana.
   
 6. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2016
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Asante sana sana mkuu.hii ni taarifa muhimu sana. Hatua zitachukuliwa haraka sana. Na je mkuu Huwezi kupata namba za hiyo hardbody? Ili kurahisishia mamlaka husika kutumbua.
   
 7. Hon Nkundwe

  Hon Nkundwe JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2016
  Joined: Nov 30, 2014
  Messages: 2,312
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Majibu yapo hila me nashauri tu swala la bomoa bomoa hili astishe
   
 8. u

  ugalila JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2016
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 652
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kutia moyo suala litashughulikiwa maana vifo vingne ni vya makusudi....

  Nakumbuka kuna dogo alikuwa amepimwa siku moja nyuma ila anaonekana kuzidiwa sana...ila wao hawajali kama ni mda wa kazi wanapga stori za michepuko yao na siasa waliniuzi kweli aisee na umati wa watu upo nje unasubiri majibu na vipimo ila wao hawaanzi kazi ni stori mbele
   
 9. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2016
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 4,160
  Likes Received: 4,194
  Trophy Points: 280
  Subiri jumatatu tutasoma mengi.

  Wahusika msifunge hii kitu tafadhalini. Huu ndio wakati wa ukweli na uwazi. Tuwekane sawa.

  Mtoa mada heshima kwako!
   
 10. koyola

  koyola JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2016
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 1,493
  Likes Received: 860
  Trophy Points: 280
  Jipu: Shinyanga barabara za lami mjini kujengwa na mkandarasi aliyejenga Bariadi, Shinyanga leo miezi 8 hakuna chochote zaidi ya kuchimbua.

  Hili nalo jipu
   
 11. u

  ugalila JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2016
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 652
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Jipu lipo barabara ya Makumbusho kituoni. Ni mbovu sana na mvua ikinyesha magari na vyombo vyote vya usafiri vinatuama sana na kuharibikia hapo, pia gari inabidi ziwashushie abiria njiani ili wakwepe hiyo barabara....

  Hili ni jipu kwa injinia wa wilaya ya kindoni anatakiwa awajibike hii barabara iweze kupitika kwani magari mengi yanashindwa kufika kituoni
   
 12. G

  GNA JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2016
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 246
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

  Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

  Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

  Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

  Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
   
 13. Mwana

  Mwana JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2016
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 4,879
  Likes Received: 1,306
  Trophy Points: 280
  Barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha SIMU 2000 ( mawasiliano) iwekwe lamiharaka ni kero kubwa.
  2. Kitua chamabasi yaendyomikoani Ubungo kijengwe haraka.
   
 14. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2016
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hili sio jipu bali ni chunusi. Waache waalimu wajiongezee kipato halali. Hawaibi na wazazi wa nataka watoto wao wapate elimu. Tafuta jipu ulilete hapa.
   
 15. k

  kingwana Senior Member

  #15
  Feb 13, 2016
  Joined: Oct 28, 2013
  Messages: 116
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pale temeke hospitali wakinamama imekuwa ni wimbo kila siku,
  Kuna majengo ya kawaida ya chini, haya yanaitwa ya walalahoi ile lile la ghorofa ni kutibiwa wale mahee hee....!!!
  Ifike kipindi tujiulize na haya mambo, watendaji wa serikali wanaangaliaje hela panapokutoa hiduma....!!!!!?
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2016
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 14,098
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Hawakai sehemu moja wanahama kila siku,kuhusu namba ya gari ni bora aulizwe manager tanroads anajua gari ya shift njia ile.Yaani wale wafanyakazi wote wanaokaa night shift njia ile wakamatwe na kufukuzwa kazi.Au wawekewe mtego
  utaifakwanza
   
 17. KILLERS KISS GUY

  KILLERS KISS GUY JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2016
  Joined: May 9, 2013
  Messages: 721
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  akiacha bomoa bomoa Mafuriko hayatawaacha, akiacha, akiacha walijenga maeneo ya wazi watoto wetu watakosa sehemu ya kuchezea. Nafikiri bomomoa ni halali maana tunawapenda ndugu zetu.
   
 18. Mulokozijr12

  Mulokozijr12 JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2016
  Joined: Oct 27, 2014
  Messages: 457
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 60
  Huu ni uzi wa whistle blowers kama hamna barabara malizaeni na mbunge wenu hapa leteni nondo za mijitu inayoliibia taifa kwa namna yoyote ile au kama unafahamu mtu aliyejipatia mali kiudanganyifu au wauza ngada huu ndo uwanja wenu
   
 19. k

  kamwamu JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2016
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 1,397
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Muda wa kuanza huduma hospitali au vituo vya afya vya umma ni tatizo. Usafi unafanywa kuanzia saa 2. Wodini ndo usiseme, kunanunuka, majibu yanasikitisha!
   
 20. mr gentleman

  mr gentleman JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2016
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 2,656
  Likes Received: 2,843
  Trophy Points: 280
  Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia. Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100. Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.

  Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.
   
Loading...