Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JamiiForums

Official Robot
Nov 9, 2006
6,092
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
9,311
2,000
Wana Jf

Nadhani kila mtu apendi wizi, anapenda kula kwa jasho halali. Kama hivyo basi hakuna budi kuanzisha thread ya kuwataja wana mtandao wa makosa tajwa na takukuru ifuatilie waliotajwa ili warudishe mali ya umma. Mfano waliouza NMC , RTC TIPPER , UDA na wengine waliohua mashirika makusudi . vile vile waliotapeli viwanja wazi, viwanja vya shule za umma, walijimilokisha magari ya serikali au kujiuzia kwa bei chee na hasa mtu yeyeto aliyehujumu nchi kwa manufaa yake. Tuzingatie tusijaze uongo bali ushahidi wa kutosha hata kama mali zimeandikishwa kwa watu wengine.
Labda kama utamtaja Mbowe Hao Takukuru watafatilia lakini si vinginevyo
 

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
362
1,000
Wasaidie kwa kupeleka maelezo hukohuko ofisini kwao. Ukileta majina huku kwa hisia ama chuki tu ni kuchafua watu.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
31,805
2,000
Hakuna taasisi hata moja ya umma inayofanya kazi kwa weledi zaidi ya kufanya wanachotaka watawala. Hizo taasisi zote zinafanya kazi kwa double standard. Kwa hiyo kama ni kutaja watakaochukuliwa hatua ni walio kinyume na watawala basi.
 

goggles

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,438
2,000
Wana Jf

Nadhani kila mtu apendi wizi, anapenda kula kwa jasho halali. Kama hivyo basi hakuna budi kuanzisha thread ya kuwataja wana mtandao wa makosa tajwa na takukuru ifuatilie waliotajwa ili warudishe mali ya umma. Mfano waliouza NMC , RTC TIPPER , UDA na wengine waliohua mashirika makusudi . vile vile waliotapeli viwanja wazi, viwanja vya shule za umma, walijimilokisha magari ya serikali au kujiuzia kwa bei chee na hasa mtu yeyeto aliyehujumu nchi kwa manufaa yake. Tuzingatie tusijaze uongo bali ushahidi wa kutosha hata kama mali zimeandikishwa kwa watu wengine.
Kuna siku 1 nilikuwa kijj ki1 kinaitwa Masurura wiliaya ya Butiama kwa mishe zangu, ikawa nimekaa na wenyeji grossary 1 hiv 2napata 1 moto 1 baridi, bila uoga bwana m1 ambae anamiliki lorry ya kusomba mchanga anajisifia kuwa anapokea pesa ya TASAF. Pesa ambayo walengwa ni maskini. Hii iliniuma sana.

TAKUKURU fuatilieni wanufaika wa TASAF kjjn hapo mtalibaini hilo. Lakini isiwe ndiyo nimewapa dill, make nimeona mtumishi mwenzenu Cosmas Batanyita alikuwa ni mpokea rushwa na siyo mzuia rushwa. Bila shaka na wengine wa aina yake wapo.
 

parts

JF-Expert Member
Mar 31, 2018
874
1,000
Waulize kwanza walisoma na kuifanyia kazi ripoti ya CAG?. Kama hawakufanya hvyo, ukimya wao ulimaanisha nini?.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,906
2,000
Kwa ujumla tu hilo jambo haliwezakani! Na sababu zipo nyingi tu. Wadau wataendelea kuzitaja.
 

Chereko

Member
Jul 20, 2009
54
95
Kama kuna mashirika ambayo nahisi yanahitaji kupitiwa na kasi ya upepo wa JPM ni NSSF na DAWASCO - wanyonge wanadhalilika sana kutokana na utendaji mbovu
 

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,448
2,000
Tunaomba msaada kwa Waziri mwenye dhamana na utoaji wa LESENI ZA UDEREVA.
Huku Mkoani NJOMBE ni tatizo sana katika suala hilo.
Mikoa mingine wanapata Leseni kwa muda unaotakiwa, lakini huku NJOMBE wengine tumelipia tangu mwezi MAY, 2019 mpaka sasa haijulikani tutapata lini Leseni zetu.
Tunaomba msaada kwani hatujui tatizo ni nini.
 

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,448
2,000
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoikubali sana kazi inayofanywa na Serikali ya awamu hii chini ya Mh. J.P.M,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na kazi hii, kuna tatizo kidogo kwa upande wa Watumishi wa Umma hasa kuhusu suala la stahiki zao.
Ni kwamba, kuna Watumishi(walimu) wenye sifa zinazofanana lakini wanatofautiana MADARAJA na MISHAHARA yao kati ya Halmashauri na Halmashauri, Wilaya na Wilaya, Mkoa na Mkoa ndani ya Nchi moja.
Tatizo jingine ni hili linaloendelea sasa la upandishaji MADARAJA kwa awamu.
Hakuna jambo linaloumiza kama hilo unapokuta mwenzio/wenzio wenye sifa za kiutumishi kama zako wanapanda DARAJA na kuongezewa MSHAHARA, halafu wewe unabaki tu kuwa mtazamaji. Mbaya zaidi watu hawa mpo STAFF moja.
Ki ukweli inauma sana.
MAPENDEKEZO;-
(1)Walimu wote wenye sifa zinazofanana wapewe mishahara inayofanana ili kuondoa MATABAKA ndani ya Nchi moja.
(2)Walimu wote wanaostahili kupandishwa madaraja, wapandishwe kwa pamoja na wala siyo kwa awamu.
Ahsante.
 

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,448
2,000
Tanzania kama M/Kiti wa SADC tuna wajibu mkubwa sana na kinachoendelea Afrika Kusini hivi sasa.
Hatuwezi kuacha Waafrika wenzetu kutoka nje ya A.Kusini wakinyanyaswa na hata kuuawa na Waafrika wenzetu bila kukemea vitendo vya kinyama.
Nafikiri tunapaswa kutoa kauli yenye uzito unaotakiwa kwa Serikali ya A.Kusini ili kuwaenzi wazee wetu(Mwenyezi Mungu awarehemu) Julius.K.Nyerere na Nelson .M.Mandela waliopinga vikali ubaguzi.
 

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,222
2,000
Ni wakati muafaka kwa Serikali kufanya OPERESHENI MAALUMU ya kuzikagua Halmashauri zote Nchini ili kubaini Madudu yanayofanywa na Watendaji.Alichokiona Mh Waziri Mkuu ktk ziara ya Mkoani Morogoro ndio lipo katika Halmashauri zote.Wananchi tunaumia kwani ni Kodi zetu hizo.Mh.Rais hebu zitupie jicho la Uchunguzi Halmashauri zako Utayaona Madudu mengi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom