kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,176
- 16,864
- Thread starter
- #61
Yaani hao independent investigators tuwalete waje tuwaonyeshe magofu ya sheli, mwendokasi, ofisi za serikali, malori, mahakama, vituo vya polisi, TRA, na ATM vilivyochomwa na waliopigwa risasi?Kwa 'rubbish🤮' hizi polisi wameshindwaje kuwakamata hao unaowaita CHADEMA, kwanini serikali inaogopa independent investigators ili kama kweli hawakuhusika basi watakuwa wamesafishika kwa majority ya raia na kimataifa pia. Wanaficha nini? Wanaogopa nini kisijulikane? Wanamlinda nani asiumbuke? Je polisi na serikali kwa ujumla kuyaficha hayo yote wanawalinda CHADEMA au wanajilinda wenyewe na viongozi wao?
Kumbuka baadhi ya waliopigwa risasi walikuwemo hata askari, nani aliua askari wale?. Kama ukileta watu kutoka nje kuja kuchuguza matukio yale miongoni mwao watajipenyeza wale waliofadhili mapinduzi yale wanaozitaka rasilimali zetu; tunalijua hilo kaka, sisi sio maboya. Kule Iran wajumbe wa shirika la nguvu za atomic waliokwenda kuchunguza mradi wa nuclear wa Iran walipenyezwa watu wa Mossad waliotoa siri kwa Israel zilizorahisisha kushambuliwa kwa mitambo ya kurutubisha Uranium.
Kaka endelea kula ndizi kazi ya usalama na ulinzi waachie wataalam waliosomea kazi hiyo. Wachunguzi kutoka nje wapeleke kwa mkeo kujua kama anakusaliti au la, lakini sio mambo ya nchi hii.